Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,224
- 26,039
Amani iwe nanyi wadau!
Naomba niende moja kwa moja kwenye mada. Leo Kuna mkutano muhimu wa Chama Kikuu cha Upinzani CHADEMA, ambapo macho na masikio ya watanzania wapenda demokrasia na wapenda maendeleo yapo kwenye mkutano huu wa CHADEMA. Moja ya ajenda kuu kwenye mkutano huu ni kumpitisha mgombea wa kiti cha uraisi atakaewakilisha Chadema kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu hapo October 2020.
Tofauti na ilivyokuwa kwenye mikutano wa Chama cha Mapinduzi ambapo Vyombo vya Habari vikubwa vya Tanzania yaani Azam Tv, Clouds Tv, ITV, TBC , Star Tv ukiondoa Channel Ten( Ambao hawa ni channel ya Chama cha mapinduzi) walikuwa wanarusha habari za mikutano ya CCM tena moja kwa moja. Vyombo hivi vilienda mbali kurusha hadi uchaguzi wa kura za maoni za wabunge wa CCM KWENYE Mikutano hii ya Chadema vyombo hivi vya habari vimeacha kwa makusudi kurusha habari za Chama hiki kikuu cha upinzani Tanzania. Sio tu kurusha live Ila hata kwenye pages zao havijaonekana kutoa updates za vikao hivi kama ilivyokuwa katika vikao vya CCM.
Ni vyombo vya habari vichache kama JamiiForums, Mwanahalisi Online, Watetezi Tv pamoja na Dar Mpya ambavyo viko live na vinatoa updates za mikutano ya Chadema. Vyombo vingine vibavyorusha matukio haya ni vya nje navyo ni DW na BBC SWAHILI, Hongereni sana maana historia itakayoandikwa mwaka huu hapo October kwenye uchaguzi Mkuu itawakumbuka.
Napenda kuviambia vyombo hivi vilivyojitoa ufahamu kwa kuwasupport CCM inayoelekea kufa kwa kuwanyima airtime Chadema kuwa baada ya October 2020 wasije sema kuwa wamekumbuka shuka asubuhi. Vijifunze kuwa huru, kutoa taarifa kwa usawa na kuvitreat vyama vyote vya siasa kwa usawa kwa sababu ya kesho ni Mungu tu anayajua.
Napenda kuwaambia pia TCRA pia ambao leo baada ya kuona vikao vya chadema vitaangaliwa mtandaoni kwa live streaming wakaamua kuhujumu kwa kupunguza nguvu ya internet kuwa nao Mungu amewaona. Tundu Lissu ni mpango wa Mungu.
Napenda kusema kwa kumalizia kuwa, Chadema ipo sawa, Chadema iko tayari, Chadema ni Nuru. Naiona Nuru kuu hapo October 2020.
Hongera Tundu Antipas Lissu. Huu ni mwanzo tu. Mungu anaenda kudhuhilisha ukuu wake kwako kwa kukupa rasmi uongozi wa nchi ya Tanzania hapo October 2020. Jiandae