Miaka ya hivi karibuni kumeibuka utamaduni wa utiriri watu kukusanyika Ikulu siku ya wateule hususan mawaziri manaibu wao na makatibu wakuu wanapoapishwa. Atakuwepo mke/mume watoto wajukuu shangazi majirani marafiki na wengineo. Muda si mrefu hata watumishi wa ndani watajumuishwa kuwepo ikulu kumpongeza baba/mama kwa kuteuliwa kuwa waziri. Huu ni mwendelezo wa ile dhana ya "AMEULA" inayotumiwa mitaani na kwenye magazeti fulani wakati ukweli ni kwamba mteule huyo amebebeswha mzigo wa kuwatumikia wananchi. Matokea yake ni kwamba mara tu mteule huyo anapokalia kiti atafanya kila njia kukidhi mategemeo ya wale waliomzunguka na muda mwingi atatumia kupanga mikakati ya wizi udokozi wa mali ya umma rushwa etc na hata inapofikia kutakiwa kuachia ngazi inakuwa vigumu kila anapofikiria hao waliofika kumpongeza na matarajio yao kwake. Mikusanyiko hii Ikulu ya kupongezana haikuwepo awamu ya kwanza na sijui ilianza lini. Imefika wakati tubadilike.
Nawasilisha.
Nawasilisha.