mkusanyiko wapongezaji Ikulu unahamasisha udokozi na kugoma kujiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mkusanyiko wapongezaji Ikulu unahamasisha udokozi na kugoma kujiuzulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KALABASH, Apr 27, 2012.

 1. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Miaka ya hivi karibuni kumeibuka utamaduni wa utiriri watu kukusanyika Ikulu siku ya wateule hususan mawaziri manaibu wao na makatibu wakuu wanapoapishwa. Atakuwepo mke/mume watoto wajukuu shangazi majirani marafiki na wengineo. Muda si mrefu hata watumishi wa ndani watajumuishwa kuwepo ikulu kumpongeza baba/mama kwa kuteuliwa kuwa waziri. Huu ni mwendelezo wa ile dhana ya "AMEULA" inayotumiwa mitaani na kwenye magazeti fulani wakati ukweli ni kwamba mteule huyo amebebeswha mzigo wa kuwatumikia wananchi. Matokea yake ni kwamba mara tu mteule huyo anapokalia kiti atafanya kila njia kukidhi mategemeo ya wale waliomzunguka na muda mwingi atatumia kupanga mikakati ya wizi udokozi wa mali ya umma rushwa etc na hata inapofikia kutakiwa kuachia ngazi inakuwa vigumu kila anapofikiria hao waliofika kumpongeza na matarajio yao kwake. Mikusanyiko hii Ikulu ya kupongezana haikuwepo awamu ya kwanza na sijui ilianza lini. Imefika wakati tubadilike.
  Nawasilisha.
   
 2. N

  NICE LAMECK JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli wengi wamekuwa wakifanya sherehe binafsi za mamilioni akijua sasa anakamata Wizara anaenda kuwa milionea.
   
 3. L

  LOVI MEMBE JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,121
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  huu nao ni uchuro wa serkali dhaifu hasa udhaifu wa maono wa kuona walioteuliwa ni kama wameula kutoka kwa kikwete mwnyewe
   
 4. L

  LOVI MEMBE JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,121
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  proponent wa kupongezana ni kikwete so i think he has cultivated this precedence by himself. what you see are just outcomes
   
 5. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu ulichosema ni kweli. Ingependeza wewe au wa JF wengine mngetoa ushauri nini kifanyike kurekebisha hili jambo. Kumbuka hivi karibuni watateuliwa mawaziri wengine na ngoma vifijo na vigegelegele vya kupongezana vitahamia ikulu tena kuendeleza utamaduni ule ule wa "WAMEULA"
   
Loading...