Mkurugezi wa sheria na Haki za Binaramu Tz Dk Helen Bisimba aishtaki Tz ICC kuvuja haki za binadamu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugezi wa sheria na Haki za Binaramu Tz Dk Helen Bisimba aishtaki Tz ICC kuvuja haki za binadamu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Oct 13, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=2]Serikali 'yaburuzwa' ICC[/h]


  Na Beatrice Shayo  13th October 2012


  [​IMG]
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dk. Helen Kijo Bisimba, akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu tamko lao kwa mauaji ya mwandishi wa Chanel Ten, Daud Mwangosi.


  Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimewasilisha malalamiko kwa mjumbe Maalum wa Umoja wa Kimataifa kwa ajili ya mauaji ya raia yanayofanywa na vyombo vya dola nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk. Helen Kijo –Bisimba, alisema kuna matukio mbalimbali yamefanywa na dola na kwamba hakuna hatua zilizochukuliwa na serikali.

  Alisema wamemtaka mjumbe huyo kufanya uchunguzi na kuchukua hatua zinazostahili dhidi ya serikali ya Tanzania.

  Pia alisema wamewasilisha malalamiko hayo kwa Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya ya Makosa ya Jinai (ICC), kumuomba afanye uchunguzi na kuona hatua anazoweza kuchukua dhidi ya serikali.

  Alisema mauaji kwa raia yanayofanywa na vyombo vya dola yanazidi kuongezeka na kuhatarisha usalama wa wananchi.

  Alisema wamewasilisha matukio mbalimbali ambayo yamefanyawa na vyombo vya dola katika mamlaka hizo ili hatua ziweze kuchukuliwa ikiwemo tukio la kuuawa kwa aliyekuwa mwandishi wa habari wa Chanel Ten, Daudi Mwangosi.

  Pia alisema suala hilo wamelipeleka kwenye Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na haki za watu katika kikao chake cha Oktoba mwaka huu huko Ivory Coast na kuitaka ichunguze na kuchukua hatua ikiwemo kulipeleka suala hili katika mahakama ya Afrika.

  Bisimba alisema taarifa hiyo wameiwasilisha kwa wadau mbalimbali wa haki za binadamu ikiwemo Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu (FIDH) na ofisi za Umoja wa Mataifa.

  Alisema kufuatia tukio la kuuawa Mwangosi, hakuna hatua za kuridhisha zilizochukuliwa licha ya kutolewa kwa ripoti tatu zilizofanya na timu maalum ya uchunguzi.

  Timu hizo ni zile za Baraza la Habari Tanzania (MCT), Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na kamati iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Emanuel Nchimbi.

  Alisema kituo chake kinasikitishwa na ripoti iliyotolewa na kamati ya Nchimbi ambayo imeweka wazi mapungufu mengi ya serikali kwenye mauaji yanayofanywa dhidi ya raia.

  Hata hivyo, alisema serikali haijajenga mfumo wa kujichunguza na kujiwajibisha yenyewe na kwamba katika tukio hilo, imeonyesha haikuwa na nia ya dhati kuchunguza mauaji yaliyofanywa na jeshi la polisi.

  Alisema wanachokitaka nikuona uwajibikaji wa viongozi wa serikali na vyombo vya dola waliohusika ikiwemo kujiuzulu, kuachishwa kazi na kufikishwa mahakamani kwa wale wote waliohusika katika mauaji mbalimbali yaliyotokea.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. kvelia

  kvelia JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Big up sana sasa serikali ijiandae
   
 3. R

  Ruppy karenston JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mama Bisimba namwaminia,very strong woman. Big up mama, let the world know whats realy happening here
   
 4. C

  Chibolo JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 2,971
  Likes Received: 1,390
  Trophy Points: 280
  Safi sana mama wa ukweli bi.Simba,hivi Nchimbi na Mwema bado wamekalia ofisi zetu? Waliopo kwenye system tujuzeni!
   
Loading...