Mkurugenzi Wilaya ya Mbozi lipa makato ya PSSSF ili wastaafu walipwe mapunjo yao

mulongu

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
572
545
Nasikitika Sana kuona WASTAAFU wengi bado hawajalipwa MAPUNJO yao na PSSSF kutokana na ucheleweshwaji wa makato yao waliyokatwa kabla ya kustaafu.

Najiuliza ni uzembe gani unaofanyika serikalini hata baada ya miaka miwili tangu wastaafu lakini bado malipo hayo hayajafanyika na porojo nyingi za tuko kwenye mchakato mwaka Mzima.

Kumbukeni hawa watu walikatwa kutoka kwenye mishahara yao hivyo hakuna haja ya kuwacheleweshea stahiki yao au mnataka wafe waache kufuatilia?

Yawezekana hawana sehemu ya kupazia sauti zao na ndio maana mkurugenzi halipi kipaumbele.

Kupitia JF naamini ujumbe utawafikia na mamlaka Husika zitalifanyia kazi.

Wenu
Mulongu
 
Back
Top Bottom