Mkurugenzi Wilaya ya Bunda asamehe pesa ya kujenga nyumba yake............. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi Wilaya ya Bunda asamehe pesa ya kujenga nyumba yake.............

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sajenti, Apr 27, 2010.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mkurugenzi mtendaji (DED) wa wilaya Bunda mkoani Mara Bw. Cyprian Oyeir ameelekeza kuwa pesa zilizotengwa kwa ujenzi wa nyumba yake ya kuishi Sh. 90ml zipelekwe katika kuboresha sekta ya elimu wilayani humo.

  Bw. Oyeir alichukua uamuzi huo kufuatia kushuka kwa elimu katika wilaya hiyo hali iliyomfanya kujikuta akifikia uamuzi huo uliowashangaza baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo. Pesa hizo ambazo kimsingi zingeweza kujenga takribani nyumba 13 (kwa thamani ya Sh. 6.9m) za kuishi walimu, zimepekwa katika shule za sekondari za Bunda na Nansimo ambapo zitawezesha kuboreshwa kwa miundo mbinu katika shule hizo na pia kuanzishwa kwa madarasa ya kidato cha tano na sita jambo lililoshindikana kufanyika kwa muda mrefu.

  Serikali ilikuwa na mkakati wa kujenga nyumba za kuishi walimu Tanzania zipatazo 21,936, lakini hadi hivi sasa ni nyumba 277 tu zilizoweza kujengwa ikiwa ni wastani wa asilimia 1 ya mpango mzima....
   
 2. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,025
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Anamuiga Jaji Mkuu Augostin Ramadhan, ingawa ni kuiga kwema. Hongera zake
   
 3. jossey1979

  jossey1979 Senior Member

  #3
  Apr 28, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwa mtazamo wangu. Hapa Serikali inabidi ione aibu!!
  serikali haikujua nini kipewe kipaombele, Nyumba ya DED au kuboresha Elimu!
  Yeye binafsi ameona Elimu ndio ipewe kipaombele.
   
 4. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Hivi hata huo msamiati kipaumbele wanaujua kweli?? mi naona mambo yanajiendea tu vululuvululu....
   
 5. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ofkoz hii pesa kwenda kwenye elimu tunampa bigup DED yuko juu lakini
  elimu nako kuna mchwa wakali tena wenye hasira na pesa za walipa kodi
  wetu sijui kama zitakuwa salama lakini tupige moyo konde tunaweza shinda
  hii vita dhidi ya mafisadi.
   
Loading...