Mkurugenzi wanyamapori afukuzwa kazi

Ukweli husemwa:

Hivi unafikiri huyo Obeid ana nguvu/mamlaka gani? Kuruhusu DEGE LA KIJESHI kuingia nchini na kuondoka bila vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi kujua?!! Kama ni ufisadi wa kutorosha wanyama nje ya nchi, I bet my neck Obeid ametolewa kama mbuzi wa kafara. Haiwezekani KAMWE ndege ya kijeshi kuingia katika anga letu bila CDF kujua au Commander in Chief of the armed forces kujua.

Sikuelewi unacholalamikia ni kipi?. Tumeona watu wengi tu ambao mimi nitawaita mashujaa na wenye misimamo katika majukumu ya kazi zao wanaamua kuachia madaraka pale wanaona utendaji wa kazi zao unaingiliwa kwa mashinikizo.

Huyu ni mwizi wa mali za nchi yetu na waziri amepewa mamlaka kisheria ya kumfukuza na amemfukuza. Swala la kufikishwa mahakamani si la waziri peke yake bali linahusisha vyombo vya dola.

Kufukuzwa ni hatua ya kwanza kuelekea kwenye full justice.

Kwa nini tusiwe na subira kidogo kuona kama atapelekwa mahakamani au la .
 
Twataka alieruhusu ile ndege kutua na kusubiria pale wanyama week nzima!

Mkuu yaani hapa ni kiini macho tu. Imesharipotiwa kwenye magazeti kuwa wale wanyama waliingia KIA kwa gari maalum kupitia lango maalum huku wakisindikizwa na FFU wenye mitutu ya bunduki. Je Ni huyo Mkurugenzi wa wanyamapori aliyewaamuru hao FFU kusindikiza hao wanyama? Come on Kagasheki.
 
kuburuzwa mahakama ipi? tanzania ukiiba mali ya umma unasimashwa kazi au unahamishiwa idara nyingine,ref jairo,
Hawa hawakusimamishwa, wamefukuzwa ikimaanisha kuwa wameonekana (na kuthibitika) kuwa wana makosa makubwa
 
Mtu kushangilia hatua hii ni kutoona upeo kamili wa skandali hili. Hapa ni zaidi ya "wizi" wa kawaida wa maliasili. Huu sio ujangili wa kawaida. Ni ngazi ya Ikulu (na Usalama wa Taifa) tu ndio wanaoweza kuondoa wingu hili. Na wana watu sehemu zote zilizohusika na mwondoko mzima.


Hivyo, Kuanzia watendaji wakuu Wizarani hadi ngazi za Ikulu hawana budi kuanguka na kisha Ikulu ikatolea ufafanuzi wa sakata zima na hata, ikibidi, kutuahidi kwamba hujuma ya aina hii (kwa maliasili na usalama wa nchi yetu) haitajirudia tena.

Manake ni kama hatuna nchi vile bali mkusanyiko wa watu maslahi binafsi tu. Ukiunganisha na mapya kama ya kupepeza bendera ya nchi kwenye meli za Iran - hatuna nchi hapa!

We certainly need to rein in the guys at the very top. Nini kuishia kumtimua kazi Mkurugenzi wa Wanyama Pori na watendaji wenzake?


Ingekuwa ni Mgomo wa walimu, madaktari au maandamano ya CHADEMA, hao uliowataja hapo juu lazima wangefunguka, kwenda kuongea na wazee wa Darisalamu. Ila kwa sababau lilikuwa swala la kuchukua chako mapema, ndio maana kimya.... mbuzi wa kafara tu ndio unawasikia
 
Hivi unafikiri huyo Obeid ana nguvu/mamlaka gani? Kuruhusu DEGE LA KIJESHI kuingia nchini na kuondoka bila vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi kujua?!! Kama ni ufisadi wa kutorosha wanyama nje ya nchi, I bet my neck Obeid ametolewa kama mbuzi wa kafara. Haiwezekani KAMWE ndege ya kijeshi kuingia katika anga letu bila CDF kujua au Commander in Chief of the armed forces kujua.

Wewe hamnazo kweli,,yaani obeid unamuona hausiki.Sasa kama angeo na hilo si sawa kwanini aliruhusu wanyama hao waondoke.Hayo ya anga na kadhalika..chenge alisha nunua radar au na hiyo mnasema haifanyi kazi,haya basi hawamu ijayo tutawapa fungu mkanunue Uchina
 
ina maana ni hao wa tatu tu ndio waliokuwa wanavuna hao twiga?? maige na timu yake vipi hakuna ushaidi? Au kagasheki anaogopa asionekane mtu wa visasi??
 
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Obeid Mbangwa, amefukuzwa kazi. Wengine ni Frank Mlemi na Simon Wella. Kosa lao ni la kujihusisha na ufisadi usafirishaji wanyamapori nje ya nchi. Kufukuzwa kwao kumetengazwa asubuhi hii na Waziri Kagasheki, Dodoma

Naye bajeti yake inasomwa nini? Maana kabla ya bajeti kusomwa wizarani sikia vituko vya mawaziri tumeona tanesco, kuvunjwa nyumba nk
 
Jamani, juyo jamaa ana uwezo wa kuruhusu Ndege za kupakia twiga zitue KIA?
Huyo jamaa sio Mbuzi wa kafara kama bwana Mhando?
Nani ana uwezo wa kuruhusu ndege za nchi nyingine kutua nchini, na kuondoka na Twiga?
Bwana Kagasheki, unasema kweli???

Kagasheki anaweza kuwa feki mwingine ktk wizara hii.

Twiga ndani ya ndege, ndge ilipita KIA, Kwenye usalama wa taifa na polisi woooote! Hawa waliambiwa nini mpaka wakaruhusu twiga apandishwe?

Nani aliwapa amri kama ilivyo kazi yao ili twiga wapite? Huyo ndo tunamtaka.
 
Enzi ya Mwalimu Nyerere, jambo la kwanza maofisa hawa wangetaifishiwa mali zao walizozipata kwa kuifisidi nchi. Kisha wangeenda lupango na adhabu ya ziada ya viboko 24. Lakini siku hizi wanaogopwa kwasababu ni wenzetu!
 
Hatimaye wauzaji wa wanyama wetu wafukuzwa kazi.

Waziri Nyalandu amewafukuza kazi wauzaji wa twiga na wanyama wengine.

Akizungumza na waandishi habari leo.

SOURCE: Star tv.
 
mmmh, watz mtaelewa lini sinema????

Washakupiga chenga?

Wamefukuza vidagaa au mapapa?
 
Na yule Boss aliyeng'atuka? Kumbuka hata mke wa Kaisari kwa kosa tu la kutuhumiwa... Wakurya tunasema: Amang'ana gasarikire!
 
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Obeid Mbangwa, amefukuzwa kazi. Wengine ni Frank Mlemi na Simon Wella. Kosa lao ni la kujihusisha na ufisadi usafirishaji wanyamapori nje ya nchi. Kufukuzwa kwao kumetengazwa asubuhi hii na Waziri Kagasheki, Dodoma

Hahaha! Hii kweli ni ze komedi yaani hawa watu wanaweza kusafirisha wanyama wote wale bila ya polisi au wizara kujua. Yaani hakuna mtu aliuliza kwa nini lile lidege la kijeshi la Qatar limetua KIA na walipoona wanyama wamefika KIA still hawakufanya lolote. Mi siwezi kuamini hata siku moja ya kuwa hawa watu ndo wahusika wakuu kwenye hii dili. Hii kitu ilikuwa authorized kutoka juu tu!

 
Hatimaye wauzaji wa wanyama wetu wafukuzwa kazi.

Waziri Nyalandu amewafukuza kazi wauzaji wa twiga na wanyama wengine.

Akizungumza na waandishi habari leo.

SOURCE: Star tv.

Mkuu Ninyalandu au KAGASHEKI? na kuwafukuza watu bila kurudisha WANYAMA wetu nisawa na bule,rudisha wanyama wetu firisi wausika.
 
Back
Top Bottom