Mkurugenzi wanyamapori afukuzwa kazi

Safi sana Balozi Kagasheki ingawa uamuzi umekuja umechelewa kusanya ushahidi uwapeleke mahakamani hamna kucheka na wezi wa rasilimali zetu.

Kweli mkuu, ila na aliyeruhusu ndege ya jeshi la nchi nyingine naye tumburuze mahakamani, hapo kweli tutakuwa objective!
 
Hayo mambo yao ya kufukuza bila kuwafilisi na kuwafikisha mahakamani na kutoa ushahidi wenye evidence ni kiini macho cha funika kombe mwanaharamu apite. Government should stand strong about maliasili.
 
Hivi unafikiri huyo Obeid ana nguvu/mamlaka gani? Kuruhusu DEGE LA KIJESHI kuingia nchini na kuondoka bila vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi kujua?!! Kama ni ufisadi wa kutorosha wanyama nje ya nchi, I bet my neck Obeid ametolewa kama mbuzi wa kafara. Haiwezekani KAMWE ndege ya kijeshi kuingia katika anga letu bila CDF kujua au Commander in Chief of the armed forces kujua.
Kama akishtakiwa anaweza kuwataja waliohusika
 
Anaenda kufukuziwa bungeni? Amesimamishwa kazi ama amefukuzwa? Manake kuna tofauti hapo!

Walishasimamishwa muda mrefu, nadhani alikuwa bado hajapata ridhaa ya mkulu kuwafukuza, si unajua hizi ni presidential posts
 
Amefukuzwa tu? Hakuna kosa la jinai hapo?
Hivi unafikiri huyo Obeid ana nguvu/mamlaka gani? Kuruhusu DEGE LA KIJESHI kuingia nchini na kuondoka bila vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi kujua?!! Kama ni ufisadi wa kutorosha wanyama nje ya nchi, I bet my neck Obeid ametolewa kama mbuzi wa kafara. Haiwezekani KAMWE ndege ya kijeshi kuingia katika anga letu bila CDF kujua au Commander in Chief of the armed forces kujua.
isipofunguliwa kesi sijui litakuwa kosa la Mh. Kagasheki au ni Director of Public Prosecution - DPP?

Ila, DPP akiweza basi hawa akina Obeid wanaweza wakawa na opportunity muhimu ya kueleza ukweli juu ya hayo yote.
...na wasipofanya chochote, tunaendelea kuongeza idadi ya usanii wa serikali katika masuala nyeti. Ila hii inaweza kuzaa mapya wakuu, maana ujasiri wa 'kumkunja' twiga na kumpakia kwenye ndege iliyoingia nchini bila kurekodiwa popote haliwezi kupita hivi hivi na wachache kukubali kutolewa kafara.

Nampongeza Balozi Kagasheki kwa kuchukua hatua sahihi kisiasa ingawaje kwa mfumo uliopo hatutegemei kama wezi wetu watatiwa hatiani na vyombo vya sheria.

Hapa tumepata 'mabangusilo' wa kupeleka Mahakamani Kisutu, na kesi itaendelea hadi 2015 kisha tutaambiwa serikali wameshindwa kuthibitisha tuhuma dhidi yao!
 
Hivi unafikiri huyo Obeid ana nguvu/mamlaka gani? Kuruhusu DEGE LA KIJESHI kuingia nchini na kuondoka bila vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi kujua?!! Kama ni ufisadi wa kutorosha wanyama nje ya nchi, I bet my neck Obeid ametolewa kama mbuzi wa kafara. Haiwezekani KAMWE ndege ya kijeshi kuingia katika anga letu bila CDF kujua au Commander in Chief of the armed forces kujua.

SAWA SAWA umenena mkuu. Yeye ni mbuzi wa kafara. Nape "anatupotezea" kwa kuzungumza kuwa CHADEMA wataka kuuza nchi. Nape tujuze kwa hili
 
Mmmh, kufukuzana sawa kama wameharibu, baada ya kufukuzana nani atachukua nafasi yake, kigezo kitakuwa na harufu gani (msomi, mwaninifu, rafiki, ndugu ya fulani, kanda moja, kabila, dini ipi)?
 
Hivi unafikiri huyo Obeid ana nguvu/mamlaka gani? Kuruhusu DEGE LA KIJESHI kuingia nchini na kuondoka bila vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi kujua?!! Kama ni ufisadi wa kutorosha wanyama nje ya nchi, I bet my neck Obeid ametolewa kama mbuzi wa kafara. Haiwezekani KAMWE ndege ya kijeshi kuingia katika anga letu bila CDF kujua au Commander in Chief of the armed forces kujua.

Waziri aeleze waliofukuzwa walipewa amri ya kukamata wanyama na nani. Kama ulivyosema haiwezekani ndege ya kijeshi toka nchi nyingine itue ktk uwanja wetu,ipakie wanyama,iruke bila vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama kuchukua hatua. Hawa ni mabangusilo tu.
 
Mbona Mbangwa na Wella ni majina ya Njomb* hivi? Nani anakanusha. Si nyumbani kwa yule mzee mwenye Bati kichwani?. Can happen only in Tanzania. I Love this country, CV NOT important but ur ancestral land.
 
Kama unaiba mali ya Bil 10, halafu unafukuzwa kazi huku umebakiza miaka 5 na Mafao ya uzeeni mil 50, ni nani ataacha kuiba? Unawaachia mil 50 ya mafao, unasepa Bil 10 - Changa la macho. Kama wako serious wawashtaki na kuwawafunga na si kesi za kuchonga kama zile za EPA za funika kombe mwanaharamu apite au kupisha upepo unaovuma.
 
Twataka alieruhusu ile ndege kutua na kusubiria pale wanyama week nzima!
 
sasa tunasubiri aburuzwe mahakamani kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake

Hawa watu ni kuwafukuza tu na kuwaachia waende zao kwa sababu wakienda mahakamani tunajua mahakama zetu zinavyonuka rushwa watatoa hela kesi itakaa mahakamani kwa miaka 5 alafu jaji atasema hakuna ushahidi wa kutosha kesi itatupwa na kwa hiyo miaka 5 pesa za walipa kodi zitakazotumia kuendesha hizo kesi ni nyingi mnoo...so kuliko kupoteza pesa zetu jamani hao watu wala wasipelekwe mahakamani, washapigwa chini inatosha nina uhakika wana majumba, viwanja mashamba, makampuni binafsi kwa hiyo hawatalala na njaa
 
Back
Top Bottom