Mkurugenzi wa wilaya ya Malinyi amsimamisha kazi Mtendaji wa Kata

kisatu

Senior Member
Jan 16, 2015
150
95
*MKURUGENZI WA WILAYA YA MALINYI AMSIMAMISHA KAZI MTENDAJI WA KATA*

Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Malinyi ndugu Marcelin Ndimbwa amemweka ndani na kumsimamisha kazi Mtendaji wa Kata ya Itete bwana Rajabu Mgurule kwa kuupuza sheria halali za halmashauri na kupuuza agizo halali la mkuu wa mkoa wa Morogoro ndg Steven Kebwe dhidi ya wafugaji wanaoingiza mifugo yao kwenye Mashamba ya Wakulima pamoja na tuhuma za kujihusisha na rushwa...

Ikumbukwe mkurugenzi akiwa anazindua vikundi 25 vya wakulima siku3 zilizopita aliwaahidi wananchi hakuna mifugo itakayovamia Mashamba hayo, hivyo kwa maamuzi hayo wananchi wamempongeza mkurugenzi wao kwa kuonesha kukomesha vitendo sugu vya wafugaji hasa kwa kumchukulia hatua za kisheria mfugaji bwana Hamad ambaye aliingiza ng'ombe zake kwenye Mashamba ya mradi wa umwagiliaji takribani wiki mbili sasa na kuamuliwa kulipa kwa sheria ndogo inavyoanisha shilingi elfu 50 kwa kila ng'ombe na 20,000 kwa ajili vijana wataowaswaga ng'ombe jumla 70,000.

Mtendaji wa kata ya Itete bwana Rajabu Mgurule alimtoza elfu 20 kinyume na taratibu ambayo ilitakiwa kutoza elfu70, hivyo kupelekea mkurugenzi kutoa amri ya kumsimamisha kazi na kukamatwa kwa Mtendaji huyu pamoja na mfugaji ili sheria ichukue mkondo wake.

Pia wananchi wamemlalamikia hakimu wa mahakama ya Wilaya ndugu MFURU ambaye amekuwa hapo kwa zaidi miaka 20 kwamba anafanya kazi kwa mazoea na kumuomba mkurugenzi wao mh Ndimbwa kumtoa ndani ya wilaya yao maana amekuwa akitenda kazi kwa mazoea hususan kwa kesi za wakulima na wafugaji, hakuna kesi hata moja ambayo wakulima wamewahi kushinda dhidi ya wafugaji, mkurugenzi amewaahidi kulifanyia kazi mara moja kwa kulipatia ufumbuzi suala hilo kwa sababu Malinyi imepata hadhi ya wilaya hivyo watahitaji Hakimu mwenye hadhi ya wilaya yaani Hakimu mkazi.

( Source : Majira la 04/08/2016

WP_20160804_004.jpg

WP_20160804_005.jpg
 
Asante Mkurugenzi wa MALINYI bwana MARCELIN NDIMBWA kwa kazi nzuri,MOROGORO ni moja ya maeneo ambayo migogoro ya wafugaji na wakulima imekua inaleta madhara mara kwa mara...tuungane sote pamoja kuunga mkono juhudi kama hizi ili tutengeneze Tanzania mpya yenye amani na utulivu....
 
Kazi ime anza rasmi
Watendaji walikua wananyanyasa wananchi. Na pia walikua wanaporaga mashamba yavijiji kuwapa wenye pesa kipindi kile ndio wilaya ya ulanga viongozi wakubwa walikua mbali sn sasa serikali ipo karibu
 
Back
Top Bottom