Mkurugenzi wa wilaya mahakamani kubatilisha matokeo ya uchaguzi- Ushindi Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi wa wilaya mahakamani kubatilisha matokeo ya uchaguzi- Ushindi Chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Feb 19, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani chato mkoani kagera kimemburuza kortini mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya chato Hamida Kwikwega kwa madai ya kubatilisha ushindi wa mwenyekiti wa kijiji cha Nyakakarango Zamda Kusoya (Chadema) aliyekuwa amechaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika Januari 15 mwaka huu.

  Zamda S. Kusoya alishinda kwa kura 178 dhidi ya mpinzani wake John Athanas (CCM) aliyepata kura 155 na ushindi huo kutangazwa na kaimu mtendaji wa kijiji Peter George.


  Baada ya kutangazwa ushindi huo inadaiwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo alitumia nafasi yake vibaya kupinga na kutotambua matokeo ya mwenyekiti huyo kwa madai uchaguzi haukuzingatia taratibu na kanuni ikiwemo kutoapishwa kwa msimamizi Peter George wa uchaguzi huo. Kutokana na hali hiyo Chama Cha Demokrasia na maendeleo kilimtaka Mkurugenzi huyo kuyatambua matokeo hayo na kwamba iwapo kuna kanuni ambazo hazikuzingatiwa hana budi kuweka pingamizi mahakamani na si yeye kubatilisha matokeo hayo.


  Katibu wa Chadema wilayani Chato Mange Sayi amesema Chama chake kimelazimika kumburuza mahakamani mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa kuwa ameshindwa kuzingatia kanuni za uchaguzi kama zinavyomuelekeza. "Sisi kama Chadema tumelazimika kumfikisha mahakamani Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato kwa kuwa amekuwa akishindwa kusimamia taratibu na kanuni za chaguzi kutokana na maslahi ya chama tawala".alisema Sayi


  Aidha katibu huyo amesema kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusomwa machi 14 mwaka huu katika mahakama ya wilaya hiyo.
  Mbali na Mkurugenzi huyo kaimu mtendaji wa kijiji cha Nyakakarango Peter George ataunganishwa kwenye mashitaka hayo kutokana na kusimamia uchaguzi kisha kutangaza matokeo hayo na baadaye kushinikizwa na Mkurugenzi wa halmashauri kutomtambua mshindi halali.
   
 2. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Magamba wanadhani wataendelea kutawala milele, kwa nini hawakubali kwamba watanzania wamewachoka?
   
 3. m

  mchambakwao Member

  #3
  Feb 19, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ya Chato ni moja ya matukio yanayofanywa na halmashauri zetu.
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  lewis makame yupo wapi?

  najisikia apertite ya kesi.
   
 5. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Uchaguzi wenyewe kumbe wa udiwani. Chadema wana njaa ya hatari sana.
   
 6. k

  kajunju JF-Expert Member

  #6
  Feb 19, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  Huyu mkurugenzi kama ana akili kama za dadake aliyewai kuwa mkuu wa wilaya ya kasulu<naye ni kwikwega> basi yote ni mab...gus
   
 7. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #7
  Feb 19, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Shameful comment!
  Nini basi maana ya uchaguzi? Kuna haja gani ya kupoteza fedha za kuandaa uchaguzi na raslimali nyingine? Wewe ni muumini kweli wa Demokrasia au unatanguliza na kujali tu maslahi yako tu?
   
 8. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #8
  Feb 19, 2012
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Aina ya hawa wakurugenzi ndo watasimamia mchakato wa kuandika katiba mpya? Kumbe bado sheria iliyopitishwa majuzi na Bunge haitafanya la maana! Yaani huyo amepindisha matokea live bado kuna kesi?
   
 9. Nyamburi

  Nyamburi JF-Expert Member

  #9
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Magamba'z thinking capacity!kwa hiyo uchaguzi wa udiwani uamriwe na mkurugenzi atakavyo?
   
 10. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #10
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Mkuu nakwaminia kwa taarifa zilizo makini, hawa maghamba wanadhani Tanzania ya jana ni sawa na leo, wacha apambane na mkono wa sheria sasa!!!!
   
 11. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #11
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Acha zako hizo kwanini wabadili matokeo kama uchaguzi wenyewe wa madiwani????? Wenye njaa ni Maghamba wana kila kitu lakini hawajashiba hata udiwani kwao ni nongwa!!!!!!

   
 12. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #12
  Feb 19, 2012
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hovyo!
   
 13. rweyy

  rweyy Senior Member

  #13
  Feb 19, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  kumbe na wewe hamunazo kama huyo mkurugenzi
   
 14. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #14
  Feb 19, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  mnaumia sana cdm wanavyoshika kasi vijijini! Hadi 2014 robo tatu ya wenyeviti wa vijiji watakuwa chadema. Mtaipata fresh.
   
 15. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #15
  Feb 19, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Faiza Foxy at work from @IKULU, Kurugenzi ya mawasiliano.
   
 16. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #16
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Wewe ni Madaso yasiyothaminika katika jamii.
   
 17. Kayoka

  Kayoka JF-Expert Member

  #17
  Feb 19, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,427
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  ukiwa kwenye s*ku zako maneno yako hata hayana mshiko..!!
   
 18. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #18
  Feb 19, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  hivi wewe ndiyo yule changudoa anayejiuza jirani na maeneo ya waheshimiwa! sikujua mapema aisee
   
 19. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #19
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Naona njaa kali inawapeleka magamba kuzimu.Rest in fire.
   
 20. h

  hans79 JF-Expert Member

  #20
  Feb 19, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  tatizo la kutojitielewa,rudi shule ya awali
   
Loading...