Mkurugenzi wa urasimishaji wa rasilimali na biashara - Mkurabita

Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
4,432
1,387
Kwa niaba ya Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi moja (01) kama ilivyoainishwa hapa chini.

1. MKURUGENZI WA URASIMISHAJI WA RASILIMALI NA BIASHARA – (NAFASI
1)

1.1 MAJUKUMU YA KAZI

  1. Kuandaa na kufanya Mapitio ya Miongozo ya urasimishaji wa rasilimali na biashara kwa ajili ya kutekeleza shughuli za urasimishaji Tanzania.
  2. Kuandaa na kufanya mapitio ya vigezo vinavyotumika kuchagua maeneo ya utekelezaji wa urasimishaji wa rasilimali na biashara kila mwaka kwa Tanzania.
  3. Kusimamia utekelezaji wa urasimishaji wa biashara kwa Mfumo wa kuanzisha Kituo Kimoja cha Urasimishaji na Uendelezaji wa Biashara katika Malmalaka za Serikali za Mitaa za Tanzania.
  4. Kusimamia utekelezaji wa urasimishaji rasilimali ardhi Mijini na Vijijini Tanzania.
  5. Kubuni, Kuandaa na Kutekeleza Programu za kuwajengea uwezo wananchi waliorasimisha rasilimali ardhi na biashara zao ili kuzitumia katika kupata mitaji kutoka Taasisi za fedha kwa ajili ya shughuli za kiuchumi
  6. Kuandaa na kutekeleza Mpango na Bajeti ya kila mwaka kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za urasimishaji wa rasilimali na biashara Tanzania.
  7. Kubainisha na kutoa ushauri wa utatuzi wa changamoto ambazo zinabainika wakati wa utekelezaji wa urasimishaji wa rasilimali ardhi na biashara Tanzania;
  8. Kushirikiana na Mtaalam wa Utafiti, Ufuatiliaji na Tathmini kufanya Utafiti, Ufuatiliaji na Tathimini ya utekelezaji wa shughuli za urasimishaji wa rasilimali na biashara Tanzania.
  9. Aidha, Mkurugenzi wa Urasimishaji, anao wajibu wa kufanya tafsiri ya matokeo ya utafiti, fuatiliaji na tathmini na kuandaa mpango kazi wa utekelzaji wa mapendekezo yanayotolewa;
  10. Kushirikiana na Mtaalamu wa Mawasiliano kwa Umma katika kuhamasisha na kujenga hamasa kwa wamiliki wa rasilimali na biashara ili waweze kurasimisha na kuzitumia rasilimali ardhi na biashara zao kwa shughuli za kiuchumi;
  11. Kusimamia na kuratibu uaandaji wa taarifa ya utekelezaji wa urasimishaji wa rasilimali na biashara katika vipindi vya robo mwaka, nusu mwaka na mwaka Tanzania;
  12. Kubuni na kusimamia utekelezaji wa mambo mbalimbali yanayolenga kuboresha mchango wa ajenda ya urasimishaji katika kukuza uchumi wa nchi na kupunguza umaskini wa kipato kwa mtu mmoja mmoja;
  13. Kubuni na kusimamia utekelezaji wa mambo mbalimbali yanayolenga kuchochea uendelevu wa matokeo ya urasimishaji wa rasilimali na biashara nchini.
  14. Kazi zingine ambazo atapangiwa na Mratibu wa Mpango;
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
  • Awe na Elimu ya kiwango cha shahada ya Uzamili katika moja ya maeneo yafuatayo:- Uchumi, Uongozi wa Biashara, Ujasiriamali na Usimamizi wa Ardhi.
  • Awe na Uzoefu usiopungua miaka mitano (5) katika kubuni, kuandaa na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ajili ya kukuza uchumi na kuondoa umaskini kwa wananchi wanyonge wa Tanzania.
  • Awe na uzalendo na uadilifu usio na mashaka na awe tayari kutekeleza majukumu yake bila usimamizi na mwenye kujituma mwenyewe na awe na uwezo wa kuongoza na kusimamia wengine.
  • Awe na uwezo wa kuwasiliana katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza
  • Awe na ujuzi wa komputa kutumia “Microsoft Word, Microsoft Excel na Power point”
  • Awe na umri usiozidi miaka 55.
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za Mishahara za MKURABITA.

1.4 AINA YA AJIRA
Mkataba ambao unaweza kurejewa kutegemea na utendaji wa kazi utakaoneshwa wakati wa utekelezaji.

1.5 KITUO CHA KAZI
Kituo cha kazi ni Dodoma ingawaje utekelezaji wa urasimishaji wa Rasilimali na Biashara unafanyika katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za Tanzania Bara na Zanzibar.

MASHARTI YA JUMLA.
  1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 55
  2. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
  3. Waombaji ambao ni Watumishi wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao.
  4. Waombaji waambatishe kupitia mfumo wa maombi ya kazi, maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu zinazopatikana pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  5. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, nakala za vyeti vya kidato cha nne na sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
    • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates
    • Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
    • Computer Certificate
    • Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
    • Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
  6. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  7. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTE NA/AU NECTA).
  8. Waombaji wa nafasi za Ajira waliostaafishwa/kuachishwa kazi katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  9. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  10. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 08 Septemba, 2020
  11. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
  12. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; Recruitment Portal
  13. (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom