wa hapahapa
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 7,454
- 4,376
hatari sana
Ndio utulie sasa watendaji wengine waendelee kufanya yao kwa picha ya boss!Ya Kairuki ni sawa kabisa ninamuunga mkono.
Hao wafanyakazi wakikubali kazi ouna vipengele vinawakanya hayo, awanyooshe tu.
Tena na kufungwa jela wafungwe.
Ndio utulie sasa watendaji wengine waendelee kufanya yao kwa picha ya boss!
Hata hujaelewa,umekurupuka kujibu suala ambalo hulielewiEeeeeeeh
Eti watendaji wengine... mimi ni mtendaji wa wapi? Ha ha haaaaa
Huu mchele utakuwa ni Mali ya lumu.baAmefanya uchunguzi gani hadi kufikia hayo maamuzi!?
Navyojua hata nchi zilizoendelea watu wakirusha video clips wapelelezinndio itaka kukutana nao kujua kilichojiri... sasa huyu hata aliyetekodi hajasikia kutoka kwake na ni wapi anadai alinunua huo mchele anakimbilia kuongea hayo yote.
Kwa upande fulani maneno hayo bila yeye kutupa ukweli wa kutuambia kwanini anasema hakuna mchele wa plastic basi kazi ipo.
Afanye hayo kwanza kutueleza zaidi, sio wananchi wote tupo kusikiliza tu mtu kasema tunashangilia **** tunayotaka kusikia pia.
Hivi wafanyakazi wengi wa serikali kwa nini hawajui kuangalia nje ya box na kutuletea habari kamili...huwezi tu kusema hakuna huku huna hata cha kutueleza kwanini unasema hakuna.
Halafu unatisha wananchi, sasa yakitokea makubwa hamuyajui mnafikiri kuna atakayekuja kujitokeza kuyaongea au kuyaonyesha?
Hapo hao Polisi, Wizara, TFDA wote wajiongeze... eti fulani kasema hakuna... hata kama ni hivyo imekuwaje hamjawa na subira kuongea na hao watuhumiwa na kama kweli ndio mtuambie.
Raisi wetu anapiga kazi, tabu wengine kuongea tu basi. Rais wetu unahitaji vichwa vipya kukusaidia kuongoza nchi wavivu na wasio na maarifa wamejaa tele serikalini kwako.
Ndio kisingizio upate uhalali wa kusema uongo, sio lazima polisi kuna TFDA, TBS, Mbunge wako, Mwenyekiti wa chama ukipendacho mbona hujulishi?Ukimshtaki polisi wanatoa siri zako so hawa polisi sio wa kuwaamini kabisa
Hata hujaelewa,umekurupuka kujibu suala ambalo hulielewi
Huu mchele utakuwa ni Mali ya lumu.ba
Mbn jamaa anawaka sana!
Ova
Kanunue mchele wa mpunga mpya, huu ndiyo msimu wake, upike halafu ukandamize uufanye matonge ya duara uone kama hautadunda. Tena mchele mpya ndiyo unadunda sana.
Hivi matumbo yenu yana mashine za kuyeyusha plastic ziwe mavi? Hamfikirii hata kiduchu?
Kamanda kamata hawa wajinga wote weka ndani, labda ndiyo watatia akili.
Nani alikudanganya kuwa capsules za kwenye dawa ni plastics?Unazifahamu dawa aina ya 'capsule'? Mtu anapokunywa hizo dawa, huwa anakunya mavi yenye capsule?
Au mtu akimeza dawa hizi zinaitwa rangimbili, mbona anakunya mavi ya kawaida. Hilo ganda (cover) huwa linayeyukia wapi humo mwilini?
Au mtu anaposhonwa nyuzi ambazo sio za kutoa (mfano baada ya kutahiri au upasuaji), hizo nyuzi huwa zinayeyukia wapi mwilini?
Yaani wewe akili zako zinakutaarifu kuwa mtu anayekula 'mchele wa plastic' ni lazima angekunya plastic pia?!! Punguani wa kichwa.
-Kaveli-
Mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya jinai (DCI), Robert Boaz, ametoa onyo kali kwa watumiaji wa mitandao ya jamii kwa lengo la upotoshaji na kuliagiza Jeshi la polisi kuanza mara moja kuwashughuliakia na kuwachukulia hatua za kisheria watu wenye tabia hiyo.
Hayo yamezungumzwa na mkurugenzi huyo mara baada ya mitandao ya kijamii kusambaza video yenye habari inayonyesha uwepo wa mchele wa plastiki nchini.
Boaz amekanusha uwepo wa mchele huo wa plastiki na kumsaka kwa udi na uvumba mtu aliyerekodi video hiyo ili asaidie kutoa taarifa zaidi.
Na amewaomba wananchi kutumia vizuri mitandao ya kijamii na kujiepusha kusambaza taarifa zisizokuwa na ukweli, kwani ni hatari na husababisha madhara makubwa katika jamii.
”Kabla ya kusambaza taarifa kwanza uwe na uhakika wa vyanzo vyako, wahsuika wanaweza kuingia kwenye matatizo yasiyokuwa ya msingi”. amesema Boaz.
Aidha waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia na wazee na watoto , Ummy Mwalimu ametaarifiwa na Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA), kuwa hakuna mchele wa aina hiyo nchini.
Waziri Ummy amewasisitizia watanzania kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii, na kuepuka upotoshaji.
Hii ni Taarifa ya TFDA
Ndio nakwambia hujaelewa!Halafu akili yako sijui haifanyi kazi vizuri,mimi nakujua mpaka nikuzungumzie wewe?Nafahamu unafanya shughuli gani mpaka nikuseme wewe?Muwe mnajiongeza!!!!PeriodEeeeeeh
Unaniandikia mimi na mimi nimeamua kukuuliza... ningekuwa sijaelewa unavyodai ungenijibu au kusema hauniongelei mimi FULL STOP
Kuelewa nini?
Acha tu...hawa watu si ndo wanasemaga raia walisaidie jeshi la polisi
kufichua waalifu na uhalifu kwa ujumla sasa hii imekaaje
wewe unaongelea kudunda...Sawa yawezekana video clip haina ukweli,tunachoomba ikanushwe na kutufafanulia kile tunachokiona kinadunda ni nini?