Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC: Watanzania hawataki mtu atakayeuza madini yao kwa wageni nje

Field Ni kugumu Sana kwa ccm hasa zama hizi ambapo vijana wanaongezeka wazee wanapungua
CCM wametengeneza wenyewe upinzani,kwakudumaza uchumi wa nchi hasa kipato cha mtu mmoja mmoja huwezi kuzuia mafuriko kwa mikono 'also it is a result of one man band show,that has caused alot of uncertainties in this country '
 
Hiyo ndio wanasema ndio tume huru,
Huyo mkurugenzi mpaka hapo anatakiwa ajiuzuru , hana sifa ya kua kwenye nafasi hiyo
 
Kama alikuwa hafai kwa nini walimteua? wote walioteuliwa na tume wanafaa kuwa rais wetu kama hafai basi tume ijiuzuru.
 
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, amesema watanzania wanataka Afya iliyoimarika, barabara nzuri, miradi ya umeme, elimu bora hawataki blah! Blah!

Amesema watanzania hawataki viongozi watakaochukua madini yao na kwenda kuyauza kwa wageni nje, watanzania wanataka viongozi watakaotetea madini yao

Ameyasema hayo alipokuwa anazungumza kumuandikia barua Tundu Lissu ili kutoa maelezo dhidi ya tuhuma za uongo anazotuhumiwa kuzitoa

Amesema Tundu Lissu amekuwa akitangaza matusi, tuhuma na kudanganya wafanyakazi badala ya kutangaza sera

==
YALIYOZUNGUMZWA KWENYE VIDEO YA MKURUGENZI WA UCHAGUZI NEC

Kwa mamlaka ya kisheria Tume iliyonayo, tayari imemuandikia Barua Mh. Tundu Lissu ya kumuita katika Kamati ya Maadili ya Kitaifa ili aje kutoa maelezo na ushahidi wa kile alichokisema katika mkutano wake huko Musoma.

Kwa mara nyengine tena Tume inawasihi Wagombea wa Vyama vyote kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi ili kulinda amani ya nchi yetu, katika kipindi cha kampeni kilichobaki kwa kujali muda wa kampeni, ratiba za kampeni na kuepuka matusi, sababu unatumia muda mwingi kutangaza matusi badala ya kutangaza sera, unatumia muda mwingi kutangaza tuhuma badala ya kutangaza sera, unatumia muda mwingi kuwadanganya Watanzania na wafanyakazi badala ya kutangaza sera.

Watanzania sasa hivi wanataka Afya iliyoimarika, Watanzania sasa hivi wanataka barabara nzuri, Watanzania sasa hivi wanataka miradi ya umeme, Watanzania sasa hivi wanataka elimu bora, Watanzania hawataki bra bra. Watanzania sasa hivi wanataka viongozi ambao watalinda madini yao, sio viongozi watakaokuja kuchukua madini yao na kupeleka kwa wageni nje.
Watanzania hawataki bra bra

Bra bra ndio nini?
 
watawala wameshapanic sana, Magu keshalegea kulegea sana, Bashiru anawatisha tu wanaCCM, PolePole anavurumisha matusi, Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ameingia kupiga kampeni
Bado spana za Serengenti hazijajibiwa kbs Mwaka kila maenye rangi yake tutamjua hadi tar27 ,
 
Wanasheria chukueni taadhari,kuna haja ya Ku-note sehemu flani kwa msaada wa baadae ikibidi. Pia kama kuna mtu mwenye video crip ya huyu bwana kada wa CCM aliye jivika ngozi ya NEC tunaiomba hapa pls.
Kwa sasa madini wanauziwa nani kwani no chakula at hage ufala na yeye madini yanachimbwa na wageni na ndo wanayapeleka nje anadhani wabongo hawajui Halafu mbona kama ni mkampeni wa magu
 
Wanasheria chukueni taadhari,kuna haja ya Ku-note sehemu flani kwa msaada wa baadae ikibidi. Pia kama kuna mtu mwenye video crip ya huyu bwana kada wa CCM aliye jivika ngozi ya NEC tunaiomba hapa pls.
Huyo awe wazi na aainishe ratiba yake ya kampeni na atuambia chama chake ,na amazindua lini,kampeni zake na Kama kina usajili. Napia atuambie ni ameacha jukumu la msingi alilopewa.? Kama mbeleko pia atuambie?
 
Huyu mkurugenzi mkuu wa NEC anaitisha vyombo vya habari na kusema eti watanzania wanataka mtu atakayelinda madini yao, atakayewajengea vituo vya afya, atakayewajengea mabarabara, atakayewaletea umeme. Kwani haya yanaihusu NEC?

Mkurugenzi wa NEC anaposema kuwa watanzania hawataki mtu atakayetorosha madini nje, kwani inaihusu nini NEC?

Kweli nimeamini hawa NEC siyo wa kuwachekea hata kidogo. Hata hii engua ya wagombea wa upinzani inafanywa kimkakati na inaonekana wazi wazi.

Magufuli amevuruga mifumo mingi huru ya maamuzi. Hii nchi inakoelekea siko hata kidogo.

View attachment 1583150
Utadhani Lisu akiingia hatajenga barabara wala vituo vya afya kwamba hivyo ndo vitu vya msingi karne 21 na miaka karibu 60 ya chama Tawala ni aibu kubwa kwa Tume ya uchaguzi
 
What I know for sure is , this october i’m voting for TUNDU LISSUu for so many reasons. but the biggest of all is that i don’t want to see some insecure, paranoid man in the highest office in the country who cares very little about laws and constitution. i also ask you to vote for TUNDU LISSU.
You can count on me too, Ni Yeye!...all votes to Mh. Tundu Antiphas Lissu! The country bumpkin has to go!
 
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, amesema watanzania wanataka Afya iliyoimarika, barabara nzuri, miradi ya umeme, elimu bora hawataki blah! Blah!

Amesema watanzania hawataki viongozi watakaochukua madini yao na kwenda kuyauza kwa wageni nje, watanzania wanataka viongozi watakaotetea madini yao

Ameyasema hayo alipokuwa anazungumza kumuandikia barua Tundu Lissu ili kutoa maelezo dhidi ya tuhuma za uongo anazotuhumiwa kuzitoa

Amesema Tundu Lissu amekuwa akitangaza matusi, tuhuma na kudanganya wafanyakazi badala ya kutangaza sera

==
YALIYOZUNGUMZWA KWENYE VIDEO YA MKURUGENZI WA UCHAGUZI NEC

Kwa mamlaka ya kisheria Tume iliyonayo, tayari imemuandikia Barua Mh. Tundu Lissu ya kumuita katika Kamati ya Maadili ya Kitaifa ili aje kutoa maelezo na ushahidi wa kile alichokisema katika mkutano wake huko Musoma.

Kwa mara nyengine tena Tume inawasihi Wagombea wa Vyama vyote kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi ili kulinda amani ya nchi yetu, katika kipindi cha kampeni kilichobaki kwa kujali muda wa kampeni, ratiba za kampeni na kuepuka matusi, sababu unatumia muda mwingi kutangaza matusi badala ya kutangaza sera, unatumia muda mwingi kutangaza tuhuma badala ya kutangaza sera, unatumia muda mwingi kuwadanganya Watanzania na wafanyakazi badala ya kutangaza sera.

Watanzania sasa hivi wanataka Afya iliyoimarika, Watanzania sasa hivi wanataka barabara nzuri, Watanzania sasa hivi wanataka miradi ya umeme, Watanzania sasa hivi wanataka elimu bora, Watanzania hawataki bra bra. Watanzania sasa hivi wanataka viongozi ambao watalinda madini yao, sio viongozi watakaokuja kuchukua madini yao na kupeleka kwa wageni nje.
Kwani ccm saivi wanauza madini chato, au Ni huko huko kwa wageni nje?!
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom