mangikule
JF-Expert Member
- Jun 11, 2012
- 6,052
- 5,425
Mbona haya ni maneno ya kampeni ya mgombea mmoja? Is this idiot impartial for real? Kumbe kumuondoa chizi lazima tupigane!!Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, amesema watanzania wanataka Afya iliyoimarika, barabara nzuri, miradi ya umeme, elimu bora hawataki blah! Blah!
Amesema watanzania hawataki viongozi watakaochukua madini yao na kwenda kuyauza kwa wageni nje, watanzania wanataka viongozi watakaotetea madini yao
Ameyasema hayo alipokuwa anazungumza kumuandikia barua Tundu Lissu ili kutoa maelezo dhidi ya tuhuma za uongo anazotuhumiwa kuzitoa
Amesema Tundu Lissu amekuwa akitangaza matusi, tuhuma na kudanganya wafanyakazi badala ya kutangaza sera
==
YALIYOZUNGUMZWA KWENYE VIDEO YA MKURUGENZI WA UCHAGUZI NEC
Kwa mamlaka ya kisheria Tume iliyonayo, tayari imemuandikia Barua Mh. Tundu Lissu ya kumuita katika Kamati ya Maadili ya Kitaifa ili aje kutoa maelezo na ushahidi wa kile alichokisema katika mkutano wake huko Musoma.
Kwa mara nyengine tena Tume inawasihi Wagombea wa Vyama vyote kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi ili kulinda amani ya nchi yetu, katika kipindi cha kampeni kilichobaki kwa kujali muda wa kampeni, ratiba za kampeni na kuepuka matusi, sababu unatumia muda mwingi kutangaza matusi badala ya kutangaza sera, unatumia muda mwingi kutangaza tuhuma badala ya kutangaza sera, unatumia muda mwingi kuwadanganya Watanzania na wafanyakazi badala ya kutangaza sera.
Watanzania sasa hivi wanataka Afya iliyoimarika, Watanzania sasa hivi wanataka barabara nzuri, Watanzania sasa hivi wanataka miradi ya umeme, Watanzania sasa hivi wanataka elimu bora, Watanzania hawataki bra bra. Watanzania sasa hivi wanataka viongozi ambao watalinda madini yao, sio viongozi watakaokuja kuchukua madini yao na kupeleka kwa wageni nje.