Mkurugenzi wa TPA aliyesimamishwa kazi, Kakoko ashikiliwa kwa mahojiano na TAKUKURU

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
1617083263886.png


Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo amethibitisha taasisi hiyo kumshikilia kwa mahojiano Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Deusdedit Kakoko aliyesimamishwa kazi na Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan.

Hivi Karibuni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alimsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini TPA Mhandisi Deusdedit Kakoko, kupisha uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha bandarini.

Rais Samia alifanya uamuzi huo Jumapili, Machi 28, 2021 baada ya kupokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Takukuru Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

“Ripoti nimeona, nimeipitia na nimebaini ubadhirifu mkubwa uliofanywa pale bandari, hili suala mnatakiwa kushirikiana, nakuomba Takukuru jishughulishe pale, alipita Waziri Mkuu alilishughulikia.

“Waziri Mkuu aliunda kamati na wakafanya uchunguzi kidogo ambao yaliyotoka, hatua chache zilichukuliwa lakini imani yangu ni kwamba kama kuna ubadhirifu pale waliosimamishwa ni hawa wa chini huku, ninaomba mara moja nitoe agizo la kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa Bandari halafu hatua zaidi ziendelee,” alisema Rais Samia.
 
Niwashauri TAKUKURU wang'ate maana hilo jamaa lina mpunga wa kutosha wakipewa hela wachukue pia wamfilisi.
 
Untouchables now wanaisoma namba kweli hii ndio nchi iliyokua inahubiriwa uzalendo na mtakatifu mwendazake, nadhani bado yule mzee kiwete wa TANROADS yule atakua na hela kuliko Cyril Ramaphosa wa SA, believe me, kwakua alikua anakwapua anampelekea mfalme sasa kwakua yeye sio mjinga anachukua chake mapema kabla hajampelekea mzee mzigo,

Mwaka huu taifa litainuka na uchafu wooote utaanza kuonekana, kumbe walikua wanatoa mapovu sijui uzalendo sijui mababeru sijui madume kumbe ilikua gia ya kujificha wasihojiwe loh Tanzania nchi yangu.
 
Untouchables now wanaisoma namba kweli hii ndio nchi iliyokua inahubiriwa uzalendo na mtakatifu mwendazake, nadhani bado yule mzee kiwete wa tanroads yule atakua na hela kuliko Cyril Ramaphosa wa SA, believe me , kwakua alikua anakwapua anampelekea mfalme sasa kwakua yeye sio mjinga anachukua chake mapema kabla hajampelekea mzee mzigo, mwaka huu taifa litainuka na uchafu wooote utaanza kuonekana , kumbe walikua wanatoa mapovu sijui uzalendo sijui mababeru sijui madume kumbe ilikua gia ya kujificha wasihojiwe loh Tanzania nchi yangu
Iruhusu akili yako iwe inatafakari bila kutafakari unakuwa huna tofauti na mende zaidi ya maumbo tu
 
Back
Top Bottom