Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Simbeye: Sekta binafsi hali ni 'tete'

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bwana Godfrey Simbeye, amesema sekta binafsi sasa hivi zinapitia kwenye wakati mgumu kutokana na kodi ambazo TRA wameziweka, kitu ambacho kinaweka mazingira magumu ya kazi za uzalishaji.

simbeye.jpg

Bwana Simbeye ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba licha ya serikali kuweka jitihada zake za kuimarisha sekta hizo, lakini kumekuwa na changamoto kubwa inakuja kwenye utaratibu usiofaa wa ukasanyaji kodi.

“Serikali kwa juhudi zake imeendelea kutengeneza mazingira mazuri ya biashara, kama kurekebisha njia za usafirishaji ikiwemo reli na viwanja vya ndege, lakini suala la kodi limekuwa ni tatizo, malalamiko mengi ya sekta binafsi yanatoka kwa namna ambavyo TRA wanakusanya kodi, ni kero kubwa, imekuwa kwa mwezi mmoja taasisi binafsi inaweza ikatembelewa na timu ya TRA tatu na zote zikaja na makadirio tofauti, kwa hiyo hilo suala tunatakiwa tuliangalie”, amesema Bwana Simbeye.

Bwana Simbeye ameendelea kwa kusema kwamba changamoto nyingine ambazo sekta binafsi zinapitia kwenye kipindi hiki ambacho uwekezaji unakua, ni pamoja na kukosa mikopo, kutokana na hali ya mabenki ilivyo kwa sasa.

“Uwekezaji mpya unakua Tanzania, hata kwenye kituo cha uwekezaji project mpya zimeongeneka, lakini uwekezaji wa ndani bado haujakuwa sana kwa sababu hali ya kukopesha kwenye sekta binafsi bado haijawa nzuri, bado hatujaona dalili nzuri ya ukopeshaji wa mabenki kwenda sekta binafsi, ingawa serikali imekuwa ikiendelea kutoa dhamana ya serikali, lakini kwa upande wa sekta binafsi bado”, amesema Bwana Simbeye.
 
Bwana Simbeye kama si kuwashwawashwa basi wewe ni mchochezi.
Sasa tusubirie kauli ya Waziri mwenye dhamana na wizara hiyo Akikanusha hayo huo uchochezi..
 
nimefunga maduka mawili, nimerudisha frem kariakoo, nimechoka kufuta vumbi wakati jiji wanataka fedha za usafi, biashra iliyopo hapa dar ni juice ya miwa sijui ukame ukikomaa tutaenda wapi, nguo hawanunui, simu hawanunui, simu ikivunjika kioo kama bado kinaona hata kwa tourch hawatengenezi screen. Sasa hivi angalau wanunuzi wa nje wacongo, wazambia ndio wanaokoa jahazi kwa wafanyabiashara wa mitaji mikubwa
 
Ni vizuri serikali ikaingia moja kwa moja kwenye biashara ili wafanyabiashara wajue moja, kuendelea kuacha mitaji yao au waitoe kwenye mzunguko.. Kwenye mzunguko kuna mmoja anachukua hela anaziweka BOT halafu hazitoi sasa kuna haja gani ya kufananya biashara katika mazingira hayo??

Tunahitaji watu wafanye biashara kihalali katika mazingira yaleyale yaliosababisha wakaamua kwenda kwenye haramu..

TRA angalieni mifumo yenu ya kodi kwa huyu mfanya biashara baadala ya kumkomoa na kuona ni halali kuchukua hela kwake na yeye asipate faida au ikiwezekana afunge kabisa biashara, TRA mbuni vyanzo vipya na namna nzuri yakukusanya kodi na sio kupambana na walewale waliopo ili ifikishe malengo... Kiasi kidogo kidogo cha kodi kikilipwa na kila mtanzania ni muhimu kuliko mtu mmoja akalipa mamilioni halafu wengine weeengi wasilipe..
 
uchumi unakuwaaaaa sana kwakweli

jana nilikuwa nasikiliza efm nimeelewa !~!!!!!!!
walikuwa wanaongelea habari za umasikini Tanzania na kwanini tunaambiwa uchumi unakuwa na umasikini bado unatisha na wala haupungui!!!
kwamba kwa takwimu hizi tunazoambiwa uchumi unakuwa itatugharimu miaka mingine 50 kama sio mia kabisa kupambana na umasikini wa nchi hii
kwamba huo uchumi unaoambiwa unakuwa ni wawekezaji ambao kwa kiasi kikubwa kile wanachozalisha wanaenda nacho kwao hapa wanatuachia makapi tu
kwamba nchi hii inategemea kilimo wakati wakulima karibu wote wanaganga njaa hawana maisha wala kilimo cha uhakika
kwamba asilimia karibu 50 ya watanaznia ni masikini na tunaishi chini ya dola moja na pia kwamba watanzania milion moja ni masikini wa kutisha yaani akiamka asubuhi hajui kama atakukula ama atalala amaatapata wapi chakula hawa ndo wale waliopo kwenye lile kundi linaloitwa "HAWANA HILI WALA LILE"
 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bwana Godfrey Simbeye, amesema sekta binafsi sasa hivi zinapitia kwenye wakati mgumu kutokana na kodi ambazo TRA wameziweka, kitu ambacho kinaweka mazingira magumu ya kazi za uzalishaji.

simbeye.jpg

Bwana Simbeye ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba licha ya serikali kuweka jitihada zake za kuimarisha sekta hizo, lakini kumekuwa na changamoto kubwa inakuja kwenye utaratibu usiofaa wa ukasanyaji kodi.

“Serikali kwa juhudi zake imeendelea kutengeneza mazingira mazuri ya biashara, kama kurekebisha njia za usafirishaji ikiwemo reli na viwanja vya ndege, lakini suala la kodi limekuwa ni tatizo, malalamiko mengi ya sekta binafsi yanatoka kwa namna ambavyo TRA wanakusanya kodi, ni kero kubwa, imekuwa kwa mwezi mmoja taasisi binafsi inaweza ikatembelewa na timu ya TRA tatu na zote zikaja na makadirio tofauti, kwa hiyo hilo suala tunatakiwa tuliangalie”, amesema Bwana Simbeye.

Bwana Simbeye ameendelea kwa kusema kwamba changamoto nyingine ambazo sekta binafsi zinapitia kwenye kipindi hiki ambacho uwekezaji unakua, ni pamoja na kukosa mikopo, kutokana na hali ya mabenki ilivyo kwa sasa.

“Uwekezaji mpya unakua Tanzania, hata kwenye kituo cha uwekezaji project mpya zimeongeneka, lakini uwekezaji wa ndani bado haujakuwa sana kwa sababu hali ya kukopesha kwenye sekta binafsi bado haijawa nzuri, bado hatujaona dalili nzuri ya ukopeshaji wa mabenki kwenda sekta binafsi, ingawa serikali imekuwa ikiendelea kutoa dhamana ya serikali, lakini kwa upande wa sekta binafsi bado”, amesema Bwana Simbeye.
Aisee! hili ni balaa hali ni mbaya sana ile Posta na Kariakoo ninayoijua wakati ule sio ya sasa! na najaribu kujiuliza kama biashara zimekufa na zinazidi kufa TRA kodi watapata wapi?
 
Ni vizuri serikali ikaingia moja kwa moja kwenye biashara ili wafanyabiashara wajue moja, kuendelea kuacha mitaji yao au waitoe kwenye mzunguko.. Kwenye mzunguko kuna mmoja anachukua hela anaziweka BOT halafu hazitoi sasa kuna haja gani ya kufananya biashara katika mazingira hayo??

Tunahitaji watu wafanye biashara kihalali katika mazingira yaleyale yaliosababisha wakaamua kwenda kwenye haramu..

TRA angalieni mifumo yenu ya kodi kwa huyu mfanya biashara baadala ya kumkomoa na kuona ni halali kuchukua hela kwake na yeye asipate faida au ikiwezekana afunge kabisa biashara, TRA mbuni vyanzo vipya na namna nzuri yakukusanya kodi na sio kupambana na walewale waliopo ili ifikishe malengo... Kiasi kidogo kidogo cha kodi kikilipwa na kila mtanzania ni muhimu kuliko mtu mmoja akalipa mamilioni halafu wengine weeengi wasilipe..
Wanatekeleza agizo la kuwafanya malaika wawe mashetani.
 
Mission ya ukusanyaji kodi TRA nadhani inahitaji kutazamwa kisayansi zaidi. Badala ya kuwa supportive kwa wafanyabiashara imekua a major hindrance. Fikiri mfanyabiashara kupoteza masaa kadhaa akisubiri kulipa kodi ofisi ya TRA, hao wafanyakazi wanapiga stori tu, ukiuliza unapewa sababu ambayo ni hiyo hiyo tokea enzi, haibadiriki! "MTANDAO UNASUMBUA!!!"
 
Back
Top Bottom