Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete tafadhali ona hili...

Pole sana tumelitolea taarifa kwa viongozi husika inatia uchungu sana
Wameahidi kulifuatilia ili lisiwakute na wengine
 
Hivi inaingia akilini hospitali smart kama hiyo ishindwe kumuhudumia mgonjwa kama huyo? Je ni wagonjwa wangapi ambao walikua serious wamepatiwa matibabu na sasa wako uraiani? Hivi watanzania wachache kwa maslahi binafsi kwa nini tuko tayari kusema uongo bila hata haya?
 
Mimi nilikua na mgonjwa pale alikua kalazwa wodini tena kahudumiwa vizuri sana na sasa anaendelea vyema nyumbani hii ni kutokana na huduma nzuri na madaktari walivyojitoa kuokoa uhai wa mgonjwa wetu No research no right to speak! Tumwogope Mungu
 
Habari zenu wakuu,

Nina masikitiko Makubwa sana kwa hiki alilochofanyiwa mgonjwa wangu alielazwa katika ward No 1 chumba cha CCU, Critical Care Unit na Manesi, hususani Manesi walioingia zamu kipindi hiki cha sikukuu ya Christmas.

Mgonjwa yuko pale, anapumulia mashine na chakula analishwa kwa mpira, na anayeruhusiwa kumlisha/kuwalisha ni Manesi tu, cha ajabu unaleta uji, mtori au chochote kile kwa mgonjwa, cha kushangaza ukirudi asubuhi unakuta chupa ipo vile vile, mgonjwa hajalishwa na mgonjwa anatumia madawa makali.

Sasa na njaa hiyo inakuwaje na hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kukaa na mgonjwa ndani mle. Kila ukiingia kumwangalia mgonjwa wako unakuta Manesi wana chat tu na simu zao, hata ukimuita anaweza kuchukua hata nusu saa, mpaka amalize ku chat ndo anyanyuke.

Jengo lile lina WiFi ya Bure ya TTCL basi imekuwa kosa, muda wote wao ni ku chat tu. Mkurugenzi mpendwa, kama imewezekana mmezungusha jengo zima CCTV camera inashindikana vipi kuweka CCTV camera kwenye Ward hizi ili kuweza kuona unyanyasaji huu wanaofanyiwa wazazi wetu wagonjwa pale?

Tunatumia garama Kubwa sana kulipia huduma pale, watu tumechangishana mpaka tumeuza viwanjwa vyetu kwa ajili ya kulipia matibabu pale, lakini kwa kweli huduma inayotolewa na Manesi hawa utafikiri wanalazimishwa, au hawalipwi mshahara?

Ukweli inauma sana, gharama pale ni kubwa sana na hata ikatokea bahati mbaya mgonjwa akafariki akiwa anadaiwa matibabu, ni mpaka deni ndugu walipe ndio mambo Mengine yaendelee. Inauma sana kwa mnachotufanyia.

Kwa upande wa madaktari sina tatizo nao kabisa, Ukweli madaktari wa pale ni wazuri sana na wanajitahidi sana kwa kweli, tatizo lipo kwa hawa manesi tu, ambao muda mwingi wao ni ku chat tuuu WiFi ya Bure.

Nakuomba sana Mkurugenzi husika angalia hili, sisi wenye wazazi wetu pale tunaumia sana na tunalipa pesa nyingi sana pale. Tunaomba wagonjwa wetu wapewe stahili yao pale, kama wale Manesi pale hawana wito watoke pale wapo wengi huku uraiani wenye wito hawana kazi. wapewe hiyo nafasi.

Mwisho nakuomba uweke CCTV camera ndani ya hizi ward kuweza kuwabaini. Mheshimiwa Jakaya Kikwete alianzisha Taasisi ile kwa malengo mazuri sana na imesaidia watu wengi kwa kweli kwanini nyinyi watu wachache msio na wito mtuharibie?

Mtoke mpishe wengine msituharibie Taasisi yetu nzuri na msiharibu jina la Mheshimiwa Rais Mstaafu.

Naomba Mkurugenzi husika fuatilia hili...

Hivi muda wa kuandika yote haya umeutoa wapi kama sio majungu! Nakupa kazi tuletee majina ya hao manesi maana najua wanavaa vitambulisho
 
Baadhi ya manesi binafsi huwa siwaelewi..........utafikiri huwa wanalazimishwa kusomea hiyo fani.
Kwa Tanzania hii siku hizi kazi si wito tena, mtu anaamua kuliko kukaa nyumbani ni bora achukue kozi fulani, halafu kazi anapata kwa memo "mpokee kama tulivyoongea" unategemea huyo ataithamini hiyo kazi, kilichobaki ni kutuulia wagonjwa wetu
 
Nasoma hii taarifa huku roho inaniuma saaana
Pole saana Mkuu najua maumivu ya kuwa na mgonjwa hlf asipate huduma ya kisawasawa
Ukizingatia mgonjwa yupo ICU na gharama ya pale isikie tu kwa mwenzio
Mkuu hii mesej yako naicopy&kupaste nakuiforward kwa wahusika wakuu kabxaaa
Hili swala lazma tulikemee kwa ujumla
Utakuwa umefanya la maana sana, Mungu akubariki
 
Habari zenu wakuu,

Nina masikitiko Makubwa sana kwa hiki alilochofanyiwa mgonjwa wangu alielazwa katika ward No 1 chumba cha CCU, Critical Care Unit na Manesi, hususani Manesi walioingia zamu kipindi hiki cha sikukuu ya Christmas.

Mgonjwa yuko pale, anapumulia mashine na chakula analishwa kwa mpira, na anayeruhusiwa kumlisha/kuwalisha ni Manesi tu, cha ajabu unaleta uji, mtori au chochote kile kwa mgonjwa, cha kushangaza ukirudi asubuhi unakuta chupa ipo vile vile, mgonjwa hajalishwa na mgonjwa anatumia madawa makali.

Sasa na njaa hiyo inakuwaje na hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kukaa na mgonjwa ndani mle. Kila ukiingia kumwangalia mgonjwa wako unakuta Manesi wana chat tu na simu zao, hata ukimuita anaweza kuchukua hata nusu saa, mpaka amalize ku chat ndo anyanyuke.

Jengo lile lina WiFi ya Bure ya TTCL basi imekuwa kosa, muda wote wao ni ku chat tu. Mkurugenzi mpendwa, kama imewezekana mmezungusha jengo zima CCTV camera inashindikana vipi kuweka CCTV camera kwenye Ward hizi ili kuweza kuona unyanyasaji huu wanaofanyiwa wazazi wetu wagonjwa pale?

Tunatumia garama Kubwa sana kulipia huduma pale, watu tumechangishana mpaka tumeuza viwanjwa vyetu kwa ajili ya kulipia matibabu pale, lakini kwa kweli huduma inayotolewa na Manesi hawa utafikiri wanalazimishwa, au hawalipwi mshahara?

Ukweli inauma sana, gharama pale ni kubwa sana na hata ikatokea bahati mbaya mgonjwa akafariki akiwa anadaiwa matibabu, ni mpaka deni ndugu walipe ndio mambo Mengine yaendelee. Inauma sana kwa mnachotufanyia.

Kwa upande wa madaktari sina tatizo nao kabisa, Ukweli madaktari wa pale ni wazuri sana na wanajitahidi sana kwa kweli, tatizo lipo kwa hawa manesi tu, ambao muda mwingi wao ni ku chat tuuu WiFi ya Bure.

Nakuomba sana Mkurugenzi husika angalia hili, sisi wenye wazazi wetu pale tunaumia sana na tunalipa pesa nyingi sana pale. Tunaomba wagonjwa wetu wapewe stahili yao pale, kama wale Manesi pale hawana wito watoke pale wapo wengi huku uraiani wenye wito hawana kazi. wapewe hiyo nafasi.

Mwisho nakuomba uweke CCTV camera ndani ya hizi ward kuweza kuwabaini. Mheshimiwa Jakaya Kikwete alianzisha Taasisi ile kwa malengo mazuri sana na imesaidia watu wengi kwa kweli kwanini nyinyi watu wachache msio na wito mtuharibie?

Mtoke mpishe wengine msituharibie Taasisi yetu nzuri na msiharibu jina la Mheshimiwa Rais Mstaafu.

Naomba Mkurugenzi husika fuatilia hili...

Hii hospital unayoisema ni moja ya kituo the best katika East and Central Africa, juzi tu wabunge wa EA walikua wanafurahia kuwa na taasisi kama hii within the region na kwamba sasa wataokoa fedha nyingi za kupeleka wagonjwa nje ya nchi, wenzetu wanaona na kuthamini huduma nzuri wewe hauoni hili ni moja ya ajabu la dunia.
 
Watu mnao mkejeli mleta mada mnanishangaza! Malalamiko ya uzembe Hospitalini ni mengi sana. Halafu yeye amekua specific kipindi cha Christmass ndiyo ame observe shida hiyo.

Sasa unapotaka picha na majina then what!? na kama mgonjwa wako alihudumiwa vizuri siyo mbaya ukatoa hushuhuda wako ila siyo vizuri kumkejeli ambae hajabahatika kupata experience hiyo. Muhimbili wanajitahidi ila changamoto zipo tena nyingi.
 
Duh, pole sana! Mm shemeji yangu alilazwa pale siku 5 bila kupatiwa hata kidonge mpaka alipofariki. Ilitubidi ss wenyewe tumpelekee tu dawa zake alizokuwa anatumia ili aendelee nazo. Mtu anatatizo la kupumua hata oxygen hakuwekewa. Alifariki usiku, wagonjwa jirani walisema alibanwa sana na pumzi walipiga sana kengele kumwita nesi hakuna aliyetokea mpaka aka collapse. Tuliishia kulipa 700,000/= ya kitanda utafikiri alikuwa kwenye 5 star hotel. Halafu not a wodi hizi za wengi kulipa hizi za watu watatu kwenye chumba peke yenu wote mko hoi wa kumsaidia mwenzie hakuna mnakufa huko chumbani wanawakuta mmekauka. Inauma sana!

Mkuu onyesha na risiti ya malipo ya hizo 700,000 ulizolipa ili kuipa nguvu hoja yako JF sio kijiwe cha uongo!
 
Back
Top Bottom