Mkurugenzi wa NIDA, Dk Arnold Kihaule ametua mkoani Morogoro akiwa na vitambulisho vya taifa 24,010

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dk Arnold Kihaule ametua mkoani Morogoro akiwa na vitambulisho vya taifa 24,010.

Alitua Morogoro ili kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kufika mkoani humo na kukaa siku tatu, ili aweze kutatua tatizo la upatikanaji wa vitambulisho hivyo kwa wananchi. Rais Magufuli alimpa agizo hilo kwa njia ya simu juzi, baada ya wananchi kutoa malalamiko yao juu ya ugumu wa kupata vitambulisho hivyo. Alizungumza nao eneo la Msamvu mjini Morogoro, akiwa njiani kuelekea Dodoma.

Walimueleza Rais kuwa wanashindwa kusajili namba zao za simu, kwa kuwa hawana vitambulisho na kwamba huduma hiyo haipatikani kwa urahisi.

"Nimefika baada ya kupokea maelekezo ya Rais nije Morogoro ili kutatua changamoto mbalimbali za wananchi kuhusu suala la utambuzi na usajili wa kupata vitambulisho vya taifa na nimekuja na vitambulisho 24,010," alisema Dk Kihaule.

Alisema vitambulisho vingine 78,081, vililetwa mkoani Morogoro Novemba 16, mwaka huu na sasa vinafanyiwa utaratibu wa kufikishwa katika kata, vijiji na vitongoji ili viwafikie walengwa. Kwamba vitambulisho vingine 17,400 tayari vimesambazwa kwenye wilaya zote za mkoa huo hadi ofisi za kata, vijiji, mitaa na vitongoji. Aliwataka wananchi kwenda kuangalia namba zao na kuchukua vitambulisho hivyo.

73a5932f263f8bd471dbad00d6c3f7ea.jpeg
 
Nadhani hakuelewa malekezo ya Rais, aliagizwa kutatua changamoto za upatikanaji wa Vitambulisho nchi nzima ikiwemo kufungua ofisi kila wilaya akishindwa aanza kuliwalipa gharama za malazi wananchi wanaotoka wilayani kuja mikoani kufuatilia vitambulisho, sasa kwenda na vitambulisho 24 elfu ndy kutekeleza maagaizo ya Rais?
 
Bado hajamaliza kazi, maana mwamba alisema kwamba yawezekana hili ni tatizo la Tanzania nzima. Hivyo aangalie namna ya kulimaliza ili wananchi masikini wasiteseke kama nilivyo sasa
 
Bado hajamaliza kazi, maana mwamba alisema kwamba yawezekana hili ni tatizo la Tanzania nzima. Hivyo aangalie namna ya kulimaliza ili wananchi masikini wasiteseke kama nilivyo sasa
Mimi nilijiandisha mwaka 2018 December, Hadi Leo sijapata kitambulisho Cha Taifa na ninaishi mjini.sebuse aliyeko matombo morogoro? Kwa kifupi NIDA ni jipu
 
Back
Top Bottom