Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini wa TAKUKURU anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha aandika barua kwa DPP kukiri makosa

Kwa kweli wana bodi kuna kitu sikijui naomba anaefahamu anijulishe nini maana ya kutakatisha fedha? Ni kwa namna gani unaweza kusema Fulani ametakatisha fedha?
 
Kwa kweli wana bodi kuna kitu sikijui naomba anaefahamu anijulishe nini maana ya kutakatisha fedha? Ni kwa namna gani unaweza kusema Fulani ametakatisha fedha?
Kutakatisha fedha au kwa lugha ya Malkia ni Money Loundering ni kitendo cha kutumia kwenye uwekezaji au biashara fedha iliyopatikana kwa njia haramu.

Makosa ya kutakatisha fedha yamo kwenye Sheria ya Anti Money Laundering Act ya mwaka 2007. Hii ni Sheria iliyohuishwa Tanzania kutoka nchi za Magharibi hususan USA ambazo zilitaka kudhibiti ugaidi ambao chanzo cha fedha zake ilikuwa ni mihadarati, silaha za magendo, mafuta au biashara ya binadamu.

Tatizo la Sheria hii ilifanywa kama copy and paste bila kuangalia athari. Kwa Tanzania makosa mengi yanayotangulia utalatishaji (predicate offence) yana dhamana wakati le kosa la kutakatisha halina dhamana. Sasa wakati mtu ni mtuhumiwa tu na bado haijathibishwa kama amepata fedha kiharamu, ananyimwa dhamana.

Kwa kifupi Kutakatisha fedha imekuwa ni kichaka cha Jiwe kuwatesa wale asiowapenda kama kina Eric Kabendera.
 
Back
Top Bottom