Msambichaka Mkinga
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 1,649
- 2,911
Watanzania wote wenye mapenzi mema, ambao ni karibia wote, ndio walinzi wa Rais wetu, lakini mlinzi mkuu ni Mungu.Habarini wana JF,
Nijielekeze kwenye maada, moja kwa moja. Kuna taarifa imetoka kuhusu safari ya mheshimiwa rais, hapo kesho ambapo atakwenda Uganda.
Swala la usalama wa taarifa za ikulu, ni muhimu sana, hususani katika kipindi hichi ambapo rais wetu ni mpya, na kuna maadui wengi tu wa ndani na nje ya nchi ambao, pengine hawakutaka awe rais.
Kutoa taarifa ya safari yake kwa umma, kabla ya yeye kufika Uganda, inaweza toa fursa kwa wenye nia mbaya, kutekeleza nia ovu.
Simuombei mabaya mheshimiwa rais, ila natoa tahadhari tu. Angeweza mtuma mjumbe maalumu kama alivyotumwa Dkt Amina Mohammed leo, kwa niaba ya rais uhuru Kenyatta.
Japo anaweza kuwakilishwa lakini kuna umuhimu wa pekee, anapoenda Rais mwenyewe kuliwakilisha Taifa lake. Zaidi atume wawakilishi huko kwenye kufungua masoko, stand, madaraja, n.k. lakini kwenye majadiliano yenye maslahi makubwa kwa nchi yake, aende akazungumze na viongozi wenzake wa kitaifa.