Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa mashtaka nchini Tanzania (DPP): Yeyote mwenye lengo la kuvuruga amani ya nchi atashughulika bila kujali dini, jinsia wala cheo chake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Mkurugenzi wa mashtaka nchini Tanzania (DPP) Biswalo Mganga amesema yeyote mwenye lengo la kuvuruga amani ya nchi atashughulika bila kujali dini, jinsia wala cheo chake.

Biswalo ameeleza hayo leo Ijumaa Oktoba 23, 2020 wakati akizindua ofisi ya Taifa ya mashtaka wilaya ya Mufindi iliyopo mjini Mafinga, akisisitiza kuwa jukumu la amani ya nchi ni la kila Mtanzania.

Amesema lengo kuu la kufungua ofisi hiyo ni pamoja na kuondoa malalamiko ya uvunjifu wa amani.

“Ni vizuri kulinda amani tuliyonayo kwa sababu machafuko yakitokea tutaenda wapi? Nchi nyingi zinataka tuharibikiwe kwa sababu wao wameshaharibikiwa, hivyo ni vizuri taratibu na sheria za nchi tulizojiwekea tuzifuate ili tuweze kupata haki, amani na usalama na nchi iweze kupata maendeleo,” amesema Biswalo.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamuhuri William amewataka wananchi kuitumia ofisi hiyo kupata haki na kulinda amani ya wilaya ya Mufindi na mji wa Mafinga.

“Ofisi hii itawasaidia wananchi kuwa na utawala bora na kesi kuendeshwa kwa haki na kuondoa malalamiko kwa wananchi katika ukiukwaji wa haki kwa wananchi na uvunjifu wa amani, ”amesema Jamuhuri

Mwananchi
 
Mbona tume ya ccm inaharibu AMANI na Uchakataji wa Kura na haikeemei?
 
Unaonaje ukianza na wakurugenzi wa usimamizi wa uchaguzi wana hatarisha amani ya nchi yetu,unazani wanavyo fanya ni sawa hawataki kuwaapisha wapinzani ,nini matokeo yake
 
Ni mtu anayeanza kulewa nafasi yake. DPP na vitisho kama hivyo haviendani kabisa! Kanaweza kuwa ni ka mtu ambako bado hakaamini kama hiyo nafasi ni yake.
 
Ni mtu anayeanza kulewa nafasi yake. DPP na vitisho kama hivyo haviendani kabisa! Kanaweza kuwa ni ka mtu ambako bado hakaamini kama hiyo nafasi ni yake.
Tunahitaji katiba mpya ili kuwepo na vipengele vya kuwadhibiti watu kama hao.
 
Back
Top Bottom