Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 875
- 960
*MD KAYOMBO ASHIRIKI MISA YA MKESHA WA CHRISTMASS PAROKIA YA BUHINGO*
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg. John Lipesi Kayombo jana alishiriki misa takatifu ya mkesha ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo katika kanisa la Roman Catholic Parokia ya Buhingo kigango cha Misasi na kutoa michango mbalimbali.
Akiwa katika Parokia hiyo iliyopo katika kijiji alichozaliwa cha Misasi katika Wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza Mkurugenzi Kayombo alichangia michango mbalimbali kwa ajili ya muendelezo wa ujenzi wa nyumba za mapadri na kanisa hilo.
Akitoa michango hiyo ambayo ni kiasi cha Shillingi Millioni moja (1,000,000/=) kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hizo za Mapadri na mifuko hamsini (50) ya Saruji yenye thamani ya Shilling laki saba na elfu hamsini (750,000/=) kwa ajili ya muendelezo wa ujenzi wa Kanisa hilo, Mkurugenzi Kayombo alisema anamshukuru Mungu kwa kumwezesha kuiona Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo na kuahidi kuendelea kutoa kidogo anachopata.
"Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuiona tena sikukuu ya kuzaliwa Yesu Kristo kwani wengi walitamani kufika siku hii, lakini amewachukua kwa hilo namshukuru sana", alisema Mkurugenzi Kayombo na kuendelea ;-
"Kwa hilo sina cha kumlipa zaidi ya kutoa ninachokipata kwa ajili ya kumtukuza, Ameen", alisema Mkurugenzi Kayombo.
Wakati huo huo akipokea michango hiyo kiongozi wa kanisa hilo Padri John Kasembo ambaye ni Paroko msaidizi alimshukuru sana Mkurugenzi Kayombo kwa moyo wake wa kuchangia kwa ajili ya mungu na kuwaasa vijana wengine wafate mfano huo.
"Kwa niaba ya wanajumuiya napenda kutoa shukurani za dhati kwa kitendo ulichokifanya, kwa hakika ni kitendo cha kumpendeza mungu na atakuzidishia zaidi na zaidi", alisema Padri Kasembo.
Pia Padri Kasembo aliwaasa vijana kufuatisha kitendo alichokifanya Mkurugenzi Kayombo cha kuchangia kwa ajili ya kumtukuza Mungu na kuacha starehe za dunia.
```Imetolewa na;
Kitengo cha Mahusiano,
Ofisi ya Mkurugenzi,
Misasi, Wilaya ya Missungwi.
Mwanza```