VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Kwenye ukurasa wa 12 wa gazeti la leo la Mwananchi kuna tangazo la mkutano wa Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni unaofanyika leo pale Magomeni. Tangazo limetolewa na Ndugu Aron T. Kagurumjuli kama Mkurugenzi wa Manispaa.
Katika tangazo hilo,Madiwani wanakaribishwa kuhudhuria mkutano huo KWA GHARAMA ZAO WENYEWE. Ingawa gharama zenyewe hazikuainishwa,nauliza utaratibu huu umeanza lini? Au kwakuwa Madiwani wengi ni wa UKAWA hapo Kinondoni?
Madiwani ambao hawana mshahara,wanapata wapi pesa za kujigharimia kuhudhuria mkutano huo? Waandaaji wanawajibika kwa lipi? Huu ni utesaji na udhalilishaji wa wazi wa Madiwani. Ni sawa na mpango wa kuwasafirisha Wakurugenzi kwa daladala hadi Dodoma!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam