Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari (TPA): Bandari ya Bagamoyo ingefilisi na kuuza nchi

Shigganza

Senior Member
May 24, 2018
160
412
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA), Deusdedith Kakoko ameeleza kwamba mradi wa ujenzi wa Bandari Bagamoyo haukuwa na tija kwa taifa na ungeenda kuifilisi na kuiuza Nchi kutokana na vipengele vya kinyonyaji ambavyo wawekezaji walitaka viwekwe kwenye mkataba na Serikali ilipopendeza kuwepo kwa win win situation wanaonekana kutokuwa tayri

Baadhi ya masharti hayo ya kinyonyaji ni pamoja na:

## Kupewa uhuru wa kujipangia bei za kutoza watakao safirisha mizigo kupitia bandari hiyo.

##Kusamehewa kodi na Ushuru mbalimbali ikiwemo zilizopo kisheria

## Kulipwa fidia ya hasara ya kibiashara katika hesabu watakazofanya wenyewe.

ahsante kwa taarifa hiyo mkurugenzi wangu,ila ina maana awamu ya nne ya utawala wetu they did NOT apply their MIND?kuhusiana na mradi huu?mmmmm mtawalipa lini wale waliokua wafanyakazi wa bandari mafao yao au ndio tunasubiri wafe wote??
 
Mimi nakumbuka awamu ya nne watu walipinga sana hii bandari. Leo serikali imeamua kuachana nayo. Watu wanalalamika tena. Hivi watanzania kwa nini ni wepesi sana kusahau? Kwa sababu hizo basi naungana na watendaji wetu tuachane na hii project. Tutafute wafadhili ambao hawatakua na masharti kama ya hawa wachina. Wachina ni hatari sana kuliko wakoloni wa kizungu. Mchina anakunyonya kwa kalamu tu. Jamani yaani waown bandari kwa miaka 99.Means kizazi chetu chote tutakuwa tushakuwa mavumbi. Who knows labda wangeongeza karne nyingine tena.
 
Nje ya mada.
 
Sio miaka 99, ni 30-40yrs. Lakini ndio maana pia tumeajiri wasomi ili watusaidia kwenye mazungumzo iwe win win na isiwe win lose. Je wataalamu wetu walishawahi kuresearch na kuja majibu juu ya faida ya hii bandari na umuhimu wake ili hata siku za usoni tukipata hela tujenge wenyewe au tutafute mwekezaji mwenye terms zinazoweza kuwa na faida pande zote.

Binafsi kwangu plan yakujenga bandari hii sio mbaya labda kama shida ipo kwa muwekezaji, Je hatuwezi tukatumia hela zetu wenyewe au kutafuta muwekezaji mwenye terms nzuri tukatekeleza wazo hili?.

Je huyu Mkurugenzi wa Bandari alishalipinga hili wazo awamu ya nne, Je huyu mkurugenzi huwa pia anapinga miradi yoyote awamu hii isio na tija au pia anasubiri awamu ya sita. Bado napata shida kuamini haya mambo chini ya utawala wa CCM, awamu ya nne hakuna kiongozi wa umma wala Mbunge wa CCM aliyepinga uwepo wa bandari ya Bagamoyo,leo Spika anatuambia ingeanza Bandari then ikaja SGR wakati michakato ya SGR inaanza yeye alikuwepo na wala hakunyanyua mdomo, awamu ya nne hakuna Mbunge wala diwani wa CCM aliyepinga mikataba ya Gas lakini leo watu wale wale wanatuambia Gas sio yetu.. Ni ngumu sana kuwaamini viongozi wanaotokana na CCM.
 
Mkurugezi hakuwa katika nafasi hii, alikuw a Tanroad kipindi hicho,tena mkoani hivyo sauti yake isingesikika.
 
Spika usimuhasabie.
Pale hakuna kitu.
 
Maana siku zote wapnzani wanapiga kelele kuwa mikataba iwekwe wazi, lakizi wabunge wa ccm wamekuwa wakiwazodoa
 
Yaani Machinery nzima ya serikali inakuja kutupiga propaganda baada ya kufuta mradi wenye manufaa makubwa ya kiuchumi kwa nchi.
Hakuna muwekezaji atakuja kuwekeza katika nchi yako halafu asirudishe mtaji wake na kupata faida. Hiyo bandari siyo mkopo na wala siyo msaada, Ni foreign direct investment!
Sasa unashindwaje kumpa mtu incentive za kuinvest matrillion yote hayo ya shilingi kwa miaka hata kama ni 50 kisha baada ya hapo uwe huru na bandari yako?
Halafu nani kasema kwa kipindi chote ambacho Mchina angeendesha bandari tusingefanikiwa?- Vipi kuhusu ajira?, Vipi kuhusu Income Tax?, Vipi kuhusu viwanda ambavyo vingeambatana na mradi!.
Tunajenga SGR bila Source ya Mzigo mkubwa wa maana, tutaishia kusafirisha mbuzi na ngozi!

Lazima tuwe wavumilivu, miaka 50 kwa nchi ni midogo sana!
 
Kabisa nilitarajia apa Watanzania wote hasa wanasiasa wa Upinzani kuungana na Serikali kutetea maslahi ya Nchi
Maana siku zote wapnzani wanapiga kelele kuwa mikataba iwekwe wazi, lakizi wabunge wa ccm wamekuwa wakiwazodoa
 
Mkurugezi hakuwa katika nafasi hii, alikuw a Tanroad kipindi hicho,tena mkoani hivyo sauti yake isingesikika.

Mkuu nimetolea mfano tu wa jinsi mambo yanavyoenda, vipi huyo mkurugenzi aliyepita alishalipinga hili hadharani kama mtaalamu wa Bandari na masuala yake (sina uhakika na hili), Je tunawatu wenye weredi kwenye masuala ya port operations (weredi + exposure) ambao wapo kwenye mazungumzo au tumepeka wanasiasa na watu waiojua uhalisia wa port operations ila mazungumzo yawe ya kitaalamu zaidi? Je huwa tuna utamaduni wa kukodisha consultation firm zenye wabobezi kwenye masuala haya ili zitusaidia kuzungumza kwenye majadiliano kama haya? Kuwepo kwenye kamati za majadiliano kunahitaji watu wenye weredi na exposure ya hali ya juu kwenye port operations, economics, business administrations, taxes expart hasa kwenye port operations, Engineers based in port operations and management, wanasheria nguli kwenye masuala ya sheria za bandari na uwekezaji.. WASIWASI WANGU HUWA TUNAPELEKA WANASIASA KWENYE MASUALA MUHIMU AMBAYO MWISHO WA SIKU HUISHIA KWENYE MASLAHI YA KISIASA NA SI MASLAHI YA NCHI.

Awamu ya tatu chini ya BWM hakuna mwanaCCM aliyesimama hadharani kupinga suala la ubinafsishaji wa mashirika ya umma ila wote walimuunga mkono BWM.. Leo hii tena watu walewale wanakuja kukwambia makosa makubwa sana yalifanyika kwenye sera ya ubinafsishaji kiasi cha kuanza kujutia na kuwaumiza watanzania, WHO PAYS THIS.?
 
Ataitwa bungeni na ndugai shauri yake, hapa mimi ndiyo huwa nakubaliana na magufuli hili nalo nakubaliana naye
 
Back
Top Bottom