Mkurugenzi wa LAPF anashirikiana na ufisadi wa LAPF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi wa LAPF anashirikiana na ufisadi wa LAPF

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 8, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,626
  Likes Received: 5,788
  Trophy Points: 280
  Mwandishi Wetu
  TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), mkoani Dodoma imewakamata wajumbe watatu waliotathimini zabuni ya kutafuta mtaalamu wa kuweka viyoyozi kwenye jengo la kisasa mali ya Mfuko wa Pensheni ya Wafanyakazi wa Serikali za mitaa (LAPF), linalojengwa Dar es Salaam.
  Jengo hilo linajengwa nyuma ya jengo la Millennium Tower Kijitonyama na linatarajiwa kugharimu mabilioni ya shilingi.
  Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Dodoma Eunice Mmari alisema wajumbe hao walifikishwa kortini mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi.

  Mmari alisema wajumbe hao walifikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka matatu likiwamo la kutumia vibaya mamlaka waliyopewa ya kumtathimini mkandarasi bora.
  Aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Jamal Mruma ambaye ni mfanyakazi wa LAPF, Vedastus Nyagilo na Prosper Manuka ambao ni wajumbe wanaojitegemea. Wajumbe hao wako nje kwa dhamana.
  Alidai washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama na kutumia mamlaka yao vibaya katika kumteua mkandarasi anayefaa kuweka viyoyozi katika jengo hilo.

  Kutokana na kutumia mamlaka hayo vibaya, wajumbe hao walimteua mkandarasi asiyekuwa na uwezo.
  Alisema washtakiwa hao walikana mashtaka yote na kesi yao itatajwa tena mwishoni mwa mwezi huu.
  Kwa upande mwingine katika mazingira ya kutatanisha Mkurugenzi Mkuu wa LAPF, Eliud Sanga alipoulizwa kuhusu suala hilo, alisema hakuna watu waliokamatwa kuhusiana na tuhuma za rushwa kwenye ujenzi wa jengo lake
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,626
  Likes Received: 5,788
  Trophy Points: 280
  Zile ttaasisi za fedha zote kikwete kaweka majambazi wake ili akiitaji kula akuna atakaengaka nenda tib mwizi yule petero nyoni ,,njoo huku lapf,,,tapeli wa mjini huyu eliudi watu wamemtundika jina la eliudi kikwete anapoaribu anahamishiwa mlo mwingine shame jakaya shame eliudi
   
 3. l

  luckypepeta Member

  #3
  Jan 23, 2016
  Joined: Dec 26, 2015
  Messages: 25
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 5
  Mhe Waziri Mkuu hili liko kwenye mamlaka yako
   
Loading...