Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Shidolya Kizimbani kwa Mauaji ya Mlinzi Wake

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
MKURUGENZI wa kampuni ya Utalii ya Shidolya ya jijini Arusha, Lazarus Mafie maarufu kwa jina la Shidolya(60)Mkazi wa Kimandolu, wilayani Arumeru, mkoani hapa amefikishwa Mahakamani akituhumiwa kutenda kosa la mauaji ya kukusudia kwa mfanyakazi wake.

Mafie na wenzake wawili wanadaiwa kumuua, Furanael Mbise ambaye alikuwa mlinzi nyumbani kwa Shidolya kwa kumkata na kitu chenye ncha kali na kisha kudanganya kuwa marehemu ameuawa na majambazi.

Akisoma shtaka hilo, mbele ya hakimu Gwanta Mwankuga wa mahakama ya wilaya ya Arumeru na mwendesha mashtaka wa serikali, Naomi Mollel aliiambia mahakama hiyo kwamba mshtakiwa huyo na wenzake wawili walitenda kosa hilo, Oktoba 18 mwaka huu 2020 nyumbani kwa mtuhumiwa.

Mwendesha mashtaka huyo aliwataja washtakiwa wengine kuwa ni Mfanyabiashara, Joseph Mafie(45) Mkazi wa Usa River na Joachim Mwanakatwe au Baraka(26) ambaye ni mtunza bustani wa kampuni ya Shidolya na Mkazi wa Kimandolu wilayani Arumeru.

Watuhumiwa hao kwa pamoja hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na shauri hilo namba 22/2020 kuwa la mauaji na hivyo mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Watuhumiwa hao mara baada ya kusomewa shitaka, walipelekwa mahabusu katika gereza kuu la Arusha lililopo kisongo wilaya ya Arumeru kutokana na shauri hilo kutokuwa na dhamana hadi kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo Desemba 2/2020.

Mwili wa Marehemu Mbise uliokuwa umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospital ya mkoa Mount Meru, umezikwa nyumbani kwake huku mtuhumiwa Shidolya akisimamia mazishi hayo ikiwemo kununua jeneza kabla ya kukamatwa na polisi akituhumiwa kuhusika na kifo cha marehemu ambaye alikuwa ndugu yake na alimwajiri kwa shughuli za ulinzi nyumbani kwake.

Katika hatua nyingine kumkuwepo jitihada zanazofanywa na ndugu wasl watuhumiwa ikiwemo mke wa mkurugenzi huyo kuhakikisha wanawanasua na masahibu hao ili kurejea uraiani kinyume cha sheria.
 
Mfanyabiashara Maarufu na mkurugenzi wa kampuni ya Utalii ya Shidolya ya jijini Arusha ,Lazarus Mafie maarufu kwa jina la Shidolya(60)Mkazi wa Kimandolu ,wilayani Arumeru,mkoani hapa,amefikishwa Mahakamàni akituhumiwa kutenda kosa la kumuua kwa kukusudia mlinzi wake.

Mafie na wenzake wawili wanadaiwa kumuua, Furanael Mbise ambaye alikuwa mlinzi nyumbani kwa Shidolya baada ya kuhisi kwamba mlinzi hiyo anamahusiano ya kimapenzi na mke wake aitwaje Jeni Mafie ambapo marehemu aliuawa kwa kumkata na kitu chenye ncha kali na kisha Shidolya alidanganya kuwa marehemu ameuawa na majambazi.

Akisoma shtaka hilo,Mbele ya hakimu Gwanta Mwankuga wa mahakama ya wilaya ya Arumeru,mwendesha mashtaka wa serikali,Naomi Mollel aliiambia mahakama hiyo kwamba mshtakiwa huyo na wenzake wawili walitenda kosa hilo,Oktoba 18 mwaka huu nyumbani kwa mtuhumiwa.

Mwendesha mashtaka huyo aliwataja washtakiwa wengine kuwa ni Mfanyabiashara, Joseph Mafie(45) Mkazi wa Usa River na Joachim Mwanakatwe au Baraka(26) ambaye ni mtunza bustani wa kampuni ya Shidolya na Mkazi wa Kimandolu wilayani Arumeru.

Watuhumiwa hao kwa pamoja hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na shauri hilo namba 22/2020 kuwa la mauaji na hivyo mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Watuhumiwa hao mara baada ya kusomewa shitaka ,walipelekwa mahabusu katika gereza kuu la Arusha lililopo kisongo wilaya ya Arumeru kutokana na shauri hilo kutokuwa na dhamana hadi kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo Desemba 2/2020 .

Mwili wa Marehemu Mbise uliokuwa umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospital ya mkoa Mount Meru ,umezikwa nyumbani kwake huku mtuhumiwa Shidolya akisimamia mazishi hayo ikiwemo kununua jeneza kabla ya kukamatwa na polisi akituhumiwa kuhusika na kifo cha marehemu ambaye alikuwa ndugu yake na alimwajiri kwa shughuli za ulinzi nyumbani kwake.

Katika hatua nyingine kumkuwepo jitihada zinazofanywa na ndugu wa watuhumiwa ikiwemo mke wake Jenni Mafie ili mkurugenzi huyo kuhakikisha wanamnasua na masahibu hao ili kurejea uraiani kinyume cha sheria.


IMG_20201124_115730_578.jpg
 
Apo uyo mtunza Bustani ndo Snitch kaona mlinzi anafaidi akaamua kutoboa siri
Sasa sijui na yeye alitaka baada ya kuona mwenzie kapewa? 😂😂😂

Lakini jambo moja ni wazi. Siamini kama mlinzi ndio alikua na guts za kuanza kumtongoza mke wa tajiri yake ambaye pia ni ndugu yake. Uwezekano mkubwa kama kweli jamaa alikua anamkula basi aliyeanza kumshawishi mwenzake ni huyo mwanamke
 
Back
Top Bottom