Mkurugenzi wa jiji Mwanza apiga danadana posho ya walimu kwa ajili ya sensa ya kesho

Kisanduku

JF-Expert Member
Jul 9, 2009
284
482
Malipo ya posho ya walimu ya kuanza kazi kwa ajili ya sensa yameingia dosari jijini Mwanza kuhusu njia ya kuwalipa walimu hao kwa sensa inayofanyika kesho nchini.

Walimu wanaohusika na zoezi hilo walijulishwa kwamba wakusanyike kwenye vituo vya Kata ambako watalipwa fedha hizo. Mapema leo asubuhi walimu wakakusanyika vituoni.

Lakini wakiwa vituoni wakapewa taarifa kwamba itakuwa ni vigumu kuzungukia vituo vyote na hivyo waondoke vituoni na wote wakutane Mwanza Secondary School ambayo kwa kifupi huitwa Mwanza Seco na ndiko malipo yatakapofanyika na si tena vituoni hapo.

Walipofika Mwanza Seco walimu wamesubiri wakijua watalipwa lakini dakika kama 20 zilizopita wakaambiwa kwamba hawatalipwa tena hapo Mwanza Seco kwa sababu Mkurugenzi wa Jiji amekosa escort. Hivyo, walimu wakaambiwa wafunge safari tena kutoka Mwanza Seco hadi Halmashauri ya Jiji.

Kutokana na usumbufu huu kumezuka fujo na aina fulani ya mgomo hadi kuleta hisia kwamba kuna njama ziko juu ya hii danadana ukichukulia kwamba kuna mwalimu anayeweza kuwa ametembea umbali kadhaa kutoka kituo cha nyumbani kwenda kituo cha Kata, ksha umbali toka kituo cha kata hadi Mwanza Seco, na sasa atatakiwa kutoka Mwanza Seco hadi Jiji ambako ni umbali wa kilomita tatu.

Kutokana na mtafaruku huu hadi dakika hii hakuna imani ni nini kinaendelea na hivyo wapo waliokata tamaa. Nusu wameamua kufunga safari ya tatu kuondoka hapo Mwanza Seco kwenda Jiji na nusu wameamua kubaki kwa sababu kwamba kama ni tatizo la escort basi hilo si lao wao kama walimu haliwahusu kwa sababu wamevumilia safari ya kutoka vituo vya kata na hakuna sababu ya kusumbuliwa kuondoka Mwanza Seco kwenda pengine tena.

Waandishi mliomo humu JF, habari ndiyo hiyo!
 
Mkuu, sijui umeipataje hii. Ni kweli unayosema lakini hata waliofunga safari kutoka Mwanza Seco hadi Jiji wamekuta huko Jiji hakuna chochote.

Hivyo, kimsingi inaeonekana kama kuna njama walimu wasilipwe posho hii.
 
Hapo mkiambiwa ccm ni janga la hili taifa la amani na utulivu mnabisha, hadi vibarua wanadhulumiwa!
 
Mkuu, sijui umeipataje hii. Ni kweli unayosema lakini hata waliofunga safari kutoka Mwanza Seco hadi Jiji wamekuta huko Jiji hakuna chochote.

Hivyo, kimsingi inaeonekana kama kuna njama walimu wasilipwe posho hii.

Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!!!!
 
Waache kuifanya hiyo kazi basi!! Watu wanataka kupika data za watu hapo, hivyo hiyo hela italiwa na wachache walafi!!
 
Hakuna sensa, ni vituko tu. Wengine vifaa hakuna kabisa. Tshirt na kofia hakuna kitu km hicho.. Bado wanaogomea sensa. Hapa Mlandizi Kibaha DC kamuweka rumande mwalimu juzi kisa alichelewa kwenda kutambua eneo la kuhesabia na kesi ni jtatu.
 
Hizo habari za kuwahamisha kutoka kumoja kwenda kwingine anawapa nani? mwajiri wao au watu tu wa mitaani?
 
Nimegundua wanaoihujumu sensa sio tuu wanaokataa kuhuseabiwa bali pia watu kama hawa
maandalizi ya sensa yameanza toka 2006 mpaka leo bado mnaleta longolongo za ela
Imagine kuna maeneo vifaa ndo wamepewa leo si hujuma izi
 
Hatimaye kelele zetu zimesaidia. Nimetaarifiwa kwamba wameanza kulipwa kule Jiji dakika hii!!
 
Hizo habari za kuwahamisha kutoka kumoja kwenda kwingine anawapa nani? mujiri wao au watu tu wamitaani?

Kuhamishwa kumetoea au hakukutokea. Ndiyo hoja unayotakiwa kukubaliana nayo au kuipinga!
 
some times uvumilivu kidogo sio dhambi.

Ni kweli. Ndiyo maana Mchungaji Rwakatare alishindwa kuvumilia ya JF akadhani akiishitaki bungeni itasaidia, akidhani tutapunguza kufukunyua mbinu za uovu.

Unadhani nini kilikwamisha yote haya hadi kazi hii kuanza saa hizi za jioni, saa ambazo huwa ni za kufunga ofisi yoyote katika weekdays.
 
Kumbe huko mwanza walimu pekee ndio wanahusika na sensa! Maeneo mengine ya nchi yetu wahusika ni mchanganyiko maalumu.Wahitimu wa drs la VII, kidato cha IV, VI, vyuo vikuu nk nk
 
may be just a few logistic complications.
 
Kuhamishwa kumetoea au hakukutokea. Ndiyo hoja unayotakiwa kukubaliana nayo au kuipinga!

Usiwe punguani, anaweza kuja mtu akawaambia hapa hazitolewi pesa, jee ana mamlaka hiyo? pengine mmoja katika hao wataopokea fedha kaona hapa itakuwa foleni kubwa ngoja niwapunguze akaanza kuvumisha kuwa fedha zitatolewa kwingine. Fikiri.

Tunataka kujuwa hao waliohamishwa waliambiwa na nani ili tumkabe huyo, aliamriwa na nani?
 
Kumbe huko mwanza walimu pekee ndio wanahusika na sensa! Maeneo mengine ya nchi yetu wahusika ni mchanganyiko maalumu.Wahitimu wa drs la VII, kidato cha IV, VI, vyuo vikuu nk nk

Wahitimu wa darasa la VII nao wamechukuliwa kuwa makarani wa sensa???!!! Terminology za ki sensa wanazielewa??? Wanaweza kuwa na utaalam wa kujenga rapport nzuri na mhojiwa??
 
Back
Top Bottom