Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma naye ni jipu. Mhe. Rais mmulike anakwamisha maendeleo ya Nzuguni

relis

JF-Expert Member
May 24, 2015
3,187
4,762
Hili suala la urasimishaji katika eneo la Nzuguni Dodoma ni Jipu lililoshindikana.

Takriban mwaka wa pili sasa na nusu zoezi la kurasimisha makazi limekuwa likienda kwa kivivu, Ujanjaujanja na kila aina ya dhulma kwa watu waliokuwa na maeneo katikati eneo hilo, kuna watumishi wa manispaa hasa Dada mmoja anayefahamika kwa jina la Oliva ni wa kumulikwa wahusika wamfuatilie kaleta vilio na malalamiko makubwa kwa Serikali kwa maslahi yake binafsi.

Eneo la Nzuguni A lilipimwa lakini makosa ni mengi hasa ya viwanja kuingiliana watu wamelalamika mpaka kwa Mkuu wa Wilaya, manispaa inaahidi kufanya marekebisho lakini hakuna kinachofanyika, watu wamejichokea wameamua kuendelea na ujenzi wakisubiria Huyo atakayekuja kuvunja haliyakuwa manispaa ndio tatizo.

Kiujumla Uongoji wa jiji hapo Manispaa umefeli katika kumaliza tatizo la urasimishaji wa makazi na viwanja Nzuguni A. Tunaendelea kumuomba Mhe. Rais aingilie kati juu ya viongozi hawa wanaopokea mishahara ya kodi zetu huku wakushindwa kuwajibika katika majukumu yao.
 
usiiamini ccm na watu wake ndugu yangu, hawaaminiki...wadokozi wamejaa humo
 
Back
Top Bottom