Mkurugenzi wa Jiji la Dar: Biashara za Mabanda katikati ya mji hazijazuiwa kama wengine walivyo tafasiri

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Dar es Salaam,

Kufuatia tangazo lililotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam siku ya Ijumaa tarehe 07/05/2021 kuhusu kuondoa vibanda vya wafanyabiashara wadogowadogo (wamachinga) waliopo kandokando ya barabara.

Ufafanuzi wa tangazo hilo lililotangazwa kwa njia ya gari ni kama ifuatavyo kwamba vibanda vinavyotakiwa kuondoshwa ni vile vilivyojengwa kwenye barabara za watembea kwa miguu na juu ya mifereji ya maji ya mvua katika eneo la katikati ya Jiji.

Maelekezo yaliyotolewa kwa wafanyabiashara ndogondogo ni kutumia meza zenye maumbo yanayohamishika. Aidha Halmashauri ya Jiji haijazuia biashara ndogondogo kuendelea kufanyika katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam.

Kwa sasa vibanda vya kudumu vilivyojengwa kwenye maeneo hayo ya katikati ya Jiji vimekuwa kero kutokana na baadhi ya vibanda hivyo kujengwa mbele ya maduka ya wafanyabiashara wakubwa na hivyo kuzuia wateja kuingia dukani aidha vibanda hivyo pia vimekuwa vikizuia njia za watembea kwa miguu hasa kwenye mabasi ya mwendokasi hivyo kuhatarisha usalama wao, pia vimekuwa vikizuia shughuli za usafi kutofanyika.

Hivyo Mkurugenzi anasisitiza kwamba biashara katikati ya mji hazijazuiwa kama wengine walivyo tafasiri, muda umetolewa hadi mwishoni mwa mwezi Mei kwa wafanyabiashara waliojenga vibanda vya kudumu kuviondosha na kutumia maumbo yaliyoelekezwa.

Imetolewa na;

Tabu F. Shaibu

Mkuu wa kitengo cha Habari,Uhusiano na Mawasiliano

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
 
Ndiyo hizo tulizozielewa waziondoe, watoe hivyo vibanda, vya njia za pikipiki, baiskeli, na waenda kwa miguu.
Ndiyo hizo zipo pembezoni mwa barabara.

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Nakumbuka Marehemu aliwaambia wamachinga washike bidhaa zao mikononi, hili la kuwwambia wabakishe meza ,Bado Hali itakuwa ni ngumu,wale wauza vyombo pale mtaa wa sikukuu.

Utakuta meza moja Ina vyombo ukipakia kwenye fuso inajaa na vingine vinabaki.
 
Nakumbuka Marehemu aliwaambia wamachinga washike bidhaa zao mikononi, hili la kuwwambia wabakishe meza ,Bado Hali itakuwa ni ngumu,wale wauza vyombo pale mtaa wa sikukuu
Utakuta meza moja Ina vyombo ukipakia kwenye fuso inajaa na vingine vinabaki.
Marehemu hajawahi kemea hawa wamachinga na hakuna halimashauri ilikuwa na nguvu mbele ya machinga.
 
Nakumbuka Marehemu aliwaambia wamachinga washike bidhaa zao mikononi, hili la kuwwambia wabakishe meza ,Bado Hali itakuwa ni ngumu,wale wauza vyombo pale mtaa wa sikukuu
Utakuta meza moja Ina vyombo ukipakia kwenye fuso inajaa na vingine vinabaki.
Hawa walioko barabarani sio machinga, huwezi kusema wewe machinga wakati mzigo uliomwaga hapo chini kwenye meza ni zaidi milion 10, Mipango miji warejee kanuni za mipango miji, tangazo la afisa habari halina suluhu yoyote, Bora wangenyamaza tu sababu hakuna linalobadilika.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Adha tunayoipata mitaa ya katikati ya mji hata pembezoni ni kubwa kiasi kwamba hata wageni wanatushangaa, serikali ijielekeze vizuri inataka kodi au inataka kujionesha inajali wafanyabiashara wadogo? Maana wenye maduka makubwa ndio wenye hizo biashara za barabarani na zinawasaidia sana kukwepa kodi.

Watendaji was serikali hamtumii akili ya kawaida kuona mtu banda analojenga ni la zaidi ya milioni 20 na bidhaa iliyomo ndani anayouza ni zaidi ya milioni 25 bado unamwita huyu mtu mmachinga kisa magufuli aliwapa vitambulish?!

Tujitahidi kufuatilia namna nzuri ya kuwafanya wauze bidhaa zao bila kuathiri haki na uhuru was watu wengine.
 
Hawa walioko barabarani sio machinga, huwezi kusema wewe machinga wakati mzigo uliomwaga hapo chini kwenye meza ni zaidi milion 10, Mipango miji warejee kanuni za mipango miji, tangazo la afisa habari halina suluhu yoyote, Bora wangenyamaza tu sababu hakuna linalobadilika.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Bahati mbaya umekutana na jamaa yako mkawa mnasalimiana mbele ya biashara yao matusi
 
Watu waache kupotosha umma hiyo hali ni ngumu kwa kweli.sio hapo tu mpaka mbagala rangi tatu hali sio nzuri kabisa ukishashuka kwenye daradara.wamachinga wamekaa kila sehemu

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
mbagala mwisho wa matatizo.mwendokas unajengwa huku watu wamo humo.mamlaka kimya akiumia mtu
 
Back
Top Bottom