Mkurugenzi wa Halmshauri ya wilaya ya Butiama anamhujumu mwenyekiti wa kijiji cha Sirorisimba

Jul 23, 2018
46
66
HUJUMA ZA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA BUTIAMA DHIDI YA JITIHADA ZA VIONGOZI NA WANANCHI WA KIJIJI CHA SIRORISIMBA.

(Soma kwa umakini).

Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya BUTIAMA amelalamikiwa na viongozi wa kijiji cha SiroriSimba kilichopo kata ya Sirorisimba pamoja na wananchi kwa hujuma anazoifanyia serikali ya kijiji hicho hususani mwenyekiti wa serikali ya kijiji anaetokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Mkurugenzi amehujumu juhudi zote zilizofanywa na mwenyekiti wa kijiji hicho cha Sirorisimba ndg. IBRAHIM MEREMO kwasababu ambazo mwenyekiti anasema "hazifahamiki".

MIRADI ILIYOTEKELEZWA KIJIJINI HAPO KUPITIA MWENYEKITI WA KIJIJI.

1. Ujenzi wa shule ya msingi Sirorisimba
2. Madarasa matatu mapya ya shule hiyo ya msingi
3. Ofisi ya kisasa ya serikali ya kijiji
4. Jiko la kupikia chakula cha wanafunzi
5. Jengo la stoo ya kutunzia chakula/nafaka
6. Serikali hiyo ya kijiji pia chini ya mwenyekiti wake ndg. Meremo wameandaa ujenzi wa sekondari ya kijiji hicho (ambao umeshimamishwa na mkurugenzi)
NB; Mambo yote haya yamefanyika bila wananchi kuchangishwa hata hats senti tano.
Maendeleo yote hayo yamesimamiwa na mwenyekiti wa kijiji kwa ushirkiano wa karibu na shirika la PSI Tanzania.

HUJUMA ALIZOFANYA MKURUGENZI MPAKA SASA.

1. Mkurugenzi ameingilia zoezi na kulazimisha kijiji kiendelee kutoa nguvu kwenye ujenzi wa sekondari ya kata km 8 kutoka kijijini na la sivyo kisimame kujenga sekondari iliyoko kijijini na kwamba kuendelea kujenga sekondari ama kufanya maendeleo ya ujenzi wa kijiji na kuendeleza ujenzi wa maboma shule ya msingi sirorisimba ni #UHAINI

2. Mkurugenzi ametumia vibaya ofisi ya umma kumteuwa mtu nje ya sheria na kumwandikia barua kuja kijijini kuwa ndiye atakuwa mwenyekiti wa kijiji kwa lazima. Yaani kwamba, mwenyekiti wa kijiji anateuliwa na mkurugenzi kinyume na utaratibu ilihali mwenyekiti aliyepo hajakataliwa na wananchi.

3. Pamoja na miradi yote mizuri ya mfano inayofanywa na halmashauri ya kijiji cha sirorisimba ofisi ya mkurugenzi imeshindwa kuheshimu maamuzi ya wananchi na kuendeleza mipango yao inayounga sera ya elimu ya kila kijiji kuwa na shule badala yake amewatisha wanakijiji kuwa kuendelea na shughuli kijijini badala ya Kata ni uhaini na kusababisha kusimamisha shughuli kijijini bila sababu.

5. Mkurugenzi ameamua kuunda tuhuma zisizo na uthibitisho na kumwandikia mwenyekiti wa kijiji, kwa mfano, mkurugenzi amesema kuwa mwenyekiti hajasoma mapato na matumizi kwa miaka mitatu mfululizo jambo ambalo linapingana na muhtasari wa kijiji unaoonesha agenda hiyo kuwepo kwa mwaka na inatekelezwa kama sheria inavyoagiza.

6. Mkurugenzi ameunda tuhuma zisizo na uthibitisho kuwa mwenyekiti amekula sh.4,000,000/= jambo ambalo linasikitisha kijiji kwani kiasi kikubwa hicho cha fedha hakijawahi kutumika popote kwa kazi isiyokuwa na baraka za wananchi na hakuna bank statement inayoonesha jambo hilo kwenye akaunti ya kijiji.

Muhimu sana kijiji kinafanya kazi zote hizo bila kuchangisha wananchi na kuwahimiza wadau kwa hiari jambo ambalo ni la mfano na linalohitaji pongezi.

Mambo yote haya yameibukiwa kwenye ziara ya Katibu wa CHADEMA mkoa wa Mara alipokuwa kwenye ziara ya kichama.
Katibu wa mkoa amemthibitishia mwenyekiti kuwa kisheria na kimaadili yuko salama aendelee kuchapa kazi ya wananchi na aendelee kutekeleza miradi yote iliyopo kwenye mipango ya kijiji na kwamba mkoa unajipanga kumpelekea msaada zaidi hivyo asizuiliwe na mtu yeyote na anayejaribu kuzuia maendeleo ya kijiji cha sirorisimba huyo hafai kukaa kwenye ofisi za umma.

KWANINI MKURUGENZI ANAMHUJUMU MWENYEKITI WA KIJIJI HUYU?

Sababu kubwa iliooneka kwa mkurugenzi ni hofu ya kuona mwenyekiti anaungwa mkono sana na wanakijiji na wasiokuwa wanakijiji, ndio maana hujuma za kumsimamisha zinaratibiwa ofisini kwa mkurugenzi.
Lakini pia mwenyekiti amekataa kutoa eneo la ofisi ya kijiji kuwa "dairy". Mwenyekiti amekataa kushiriki ufisadi wa kujificha kwenye ujenzi wa sekondari ya kata inayotumika kula nguvu ya wananchi na ushahidi wake uko wazi kuwa kuna viongozi wamekula fedha za tofali, mawe, michanga, saruji, nondo, hivyo kupelekea ujenzi wa shule hiyo ya kata kukwama.

Mwenyekiti meremo amekataa muungano huo wa kula fedha za wananchi anajenga kijiji chake mkurugenzi hujuma za kumkwamisha badala ya kumpa moyo.

Utendaji wa mwenyekiti wa kijiji hicho unaungwa mkono na wajumbe wote wa serikali ya kijiji pamoja na wananchi bila kujali utofauti wa vyama vyao. Lakini jambo la kushangaza, mkurugenzi huyu akaona jambo hilo halina maana wala halipaswi kuungwa mkono.

Ukiisoma barua hiyo iliyoandikwa na kusainiwa na aliyejitambulisha kama Kaimu Mkurugenzi ndg. Kedmon M. Chipanyanga ina baadhi ya hoja ambazo kimsingi hazina mashiko katika mazingira ya sheria na kijamii.

Mfano, katika kipengele cha tano (v) barua inaeleza kuwa "kukataa kupokea wito wa Baraza la Ardhi". Katika dai hili, siyo kweli kwamba mwenyekiti alikataa kuitikia wito bali hakuipata barua yenyewe. Na hata hivyo, ofisi ya kijiji ipo kwa ajili shughuli za kila siku ambazo kimsingi zinaendeshwa na mtendaji wa kijiji (VEO) na siyo mwenyekiti wa kijiji wala siyo yeye anaepaswa kukaa ofisini na kupokea barua za serikali.

Pia, barua inamtaja ndg. Ibrahim Chacha Nchama kama mdai wa eneo lililopo ndani ya kijiji hicho kwa madai kuwa miaka 80' alikuwa anafanya kazi kwenye dairy hiyo na alikuwa halipiwi hivyo, akaamua kulikatalia eneo kama sehemu ya kujilipa.

Mkurugenzi na Afisa Mtendaji wameungana kuwa kinyume kabisa na mwenyekiti huyu kwa sababu ya kusimama na kuupigania ukweli na maslahi ya wananchi wa Sirorisimba.

Watumishi wa kariba hii ya mkurugenzi huyu ambao wanaenda kinyume na maendeleo ya wananchi sidhani kama wastahili kuendelea kuwepo katika ofisi za umma. Natamani kuona serikali ikilifuatilia suala hili na kulichukulia hatua stahiki.

Nimeambatanisha picha za miradi iliyotekelezwa na barua ya mkurugenzi.View attachment 850445
IMG-20180829-WA0028.jpg
View attachment 850447
IMG-20180829-WA0038.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeambatanisha picha za miradi iliyotekelezwa na barua ya mkurugenzi.View attachment 850445View attachment 850446View attachment 850447View attachment 850448

Sent using Jamii Forums mobile app
Hoja za kimahakama zinajibiwa mahakamani, za ofisi majibu yanapatikana ofcn, za kjj zinajibiwa kwenye mkutano wa kijiji: humu JF siyo mahali pake...fuata taratibu.

Chadema hata wakituhumiwa kuiba pesa, wanasema siasa...sasa nyie n watu wa namna gani? Jibu hoja, jibu tuhuma. Acheni kujificha, kutafuta huruma ya kisiasa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom