Mkurugenzi Wa Halmashauri ya Mbozi kuhojiwa kwa upotevu Wa fedha tshs 200 Milioni

usikumnene

Member
Apr 23, 2017
81
108
Kipindi cha kusoma magazeti asubuhi nilimsikia mtangazaji akisoma kichwa cha habari cha gazeti moja kuwa Mkurugenzi wa Mbozi kuhojiwa kwa upotevu Wa sh 200m, mwenye taarifa kamili atujuze tafadhali.

=======

DED Mbozi aenda kuhojiwa ubadhirifu wa mil. 200/-

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Kazimbaya Makwega, ametii agizo la Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara ya kutaka kwenda wilayani Lushoto kujibu tuhuma za ubadhirifu wa Sh. milioni 200.

Serikali ilipokea fedha Sh. bilioni 1.8 kutoka kwa mwekezaji mpya kampuni ya New Kimamba Fibres, iliyonunua shamba hilo la mnazi kwa fedha hizo na kati ya hizo halmashauri ilipata Sh. milioni 600 kwa ajili ya ushuru wa huduma.

Upatikanaji wa fedha hizo uliifanya halmashauri hiyo kuanza michakato ya kutangaza zabuni kumpata mkandarasi atakayepima viwanja hivyo vyenye ukubwa wa hekta 1,637 na kupatikana kampuni hiyo ya Geoplan East Afrika Limited ya jijini Dar es Salaam ambayo ilipewa tenda ya Sh. milioni 300 kupima viwanja hivyo.

Hata hivyo, upatikanaji wa kampuni hiyo ulizua utata baada ya kudaiwa leseni yake ilikwisha muda na jinsi fedha zilivyotoka kabla ya kuanza kazi tayari kampuni hiyo ilipewa Sh. milioni 200 kinyume na taratibu za manunuzi.

Wakati suala hilo linafanyika wilayani humo, huku baadhi ya wakuu wa idara akiwamo ofisa ardhi wakisaini fedha za zaidi ya siku 30 bila kwenda kwenye tukio, wametakiwa kurejesha fedha hizo, huku Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbozi akitakiwa kurudishwa Lushoto kujibu tuhuma hizo.

Ubadhirifu wa matumizi hayo ya fedha uliibuka baada ya Waziri Waitara kufanya ziara wilayani humo katika kikao chake na watumishi na kubaini kuwapo kwa matumizi hayo yasiyofuata taratibu za manunuzi na kutoa maagizo ya kusimamishwa watumishi watatu, huku akimtaka Mkurugenzi Makwega, kufika kuhojiwa.

Mkurugenzi Makwega ametii agizo kwa kufika wilayani Lushoto akiendelea kuhojiwa na maofisa toka Tamisemi, huku wenzake watatu wakisimamishwa kazi kufuatia matumizi hayo ya fedha Sh. milioni 200 kati ya 300.

Akizungumza na gazeti hili jana ofisini kwake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lushoto, Lucas Shendolwa, alikiri kuwapo na matumizi ya fedha hizo akidai kuwa serikali baada ya kupokea fedha Sh. 2,808,240,000 kutoka kwa mwekezaji mpya wa shamba la mnazi na kusema kuwa Sh. milioni 600 walipewa kwa ajili ya ushuru wa huduma.

Alisema baada ya magizo ya Waziri Mkuu, madiwani wanatakiwa kurudisha fedha walizolipana posho walipoketi vikao ambazo ni Sh. 9,075,000 na kwamba mkurugenzi na timu yake wanatakiwa kurejesha Sh. milioni 200, na baadaye hatua zitachukuliwa.

Watumishi waliosimamishwa kufuatia tuhuma hizo ni Mhasibu wa Halmashauri ya Lushoto, Lenatus Mkasiwa, Meneja wa Mradi, Rehema Shimliwa, Ofisa Manunuzi, Deogratus Lwamtawe na aliyekuwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, aliyehamishiwa Wilaya ya Mbozi, Kazimbaya Makwega yupo Lushoto akihojiwa.

Halmashauri ya wilaya hiyo jana imekaa kikao kujadili na kupata ukweli kuwa viwanja hivyo vimepimwa huku ikielezwa kuwa kampuni iliyopewa zabuni hiyo iliweka mawe ya mipaka kwenye maeneo ya vichaka kisha kuondoka.

Baadhi ya watumishi katika Halmashauri ya Lushoto walifurahishwa na kitendo cha mkurugenzi huyo kuitwa kujibu tuhuma hizo wakidai ni msumbufu, huku akikiuka maadili ya kazi kwa kutumia vibaya madaraka yake kwa kuwahamisha hamisha vituo vya kazi hasa wanawake.

Chanzo: Nipashe


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom