Mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu naye aanza kukatwa mshahara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu naye aanza kukatwa mshahara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CR wa PROB, Nov 1, 2011.

 1. CR wa PROB

  CR wa PROB Senior Member

  #1
  Nov 1, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sioni kama hili la leo lililofanywa na akina Mrema ni suluhu ya hilo tatizo au vipi, Kwa kifupi Mkurugenzi wa Halmashuri ya Wilaya ya Kishapu ametia hasara serikali yetu sh billioni tatu ila adhabu aliyopewa ni kupewa hati chafu na kukatwa mshahara kwa 15%, je wewe kama mzalendo wa Kitanzania unaona kama hii adhabu ni ya haki?? Jamani hiuvi ina maana hii nchi haina adhabu nyingine kali zaidi ya hiyo??? au hivi ndio tunatimilizi miaka 50 ya uhuru wa kushindana kuchamba?


  Source ITV Habari ya saa mbili leo.
   
 2. l

  laun Senior Member

  #2
  Nov 1, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Taarifa ya habari ya ITV leo kulikuwa na taarifa ya ubadhirifu wa bil 3 za miradi katika halmashauri ya Kishapu.
  Adhabu iliyoamriwa na kamati ya bunge ni kukatwa asilimia 15 ya mshahara wa DED,DT na DIA.
  Hii ni akili au matope,ni sawa na kumuhukumu mwizi wa ng'ombe kulipa kuku.
  Nina uhakika kuwa hiyo 15 ya mishahara ya hao jamaa wote haifiki hata 1 mil, itafidia vipi bil 3.
  Hali kama hii inapelekea watumishi kutokuwa na hofu na nidhamu juu ya usimamizi wa mali za umma.
   
 3. Mmasi

  Mmasi Senior Member

  #3
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kijana mi ndo kwanza nakushanga huyu ameanzaga zamani wanamleaga tu mi nimekuwa nasikiliza taarifa zake kwenye vyombo vya habari cku nyingi.cni walewaleeeeee.!
   
 4. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hukumu haitolewi kwa utashi wa mtu kafanya nini, angalia sheria za fedha zinasemaje? Hoja ya msingi ilikuwa ni kuwafukuza kazi na kuwafungulia mashitka kwa kuitia hasara serikali ya kiwango fulani huko ndiko hayo unayoyataka yatatokea.
   
 5. CR wa PROB

  CR wa PROB Senior Member

  #5
  Nov 1, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sasa wewe unashauri nini kifanyike?? na kama taarifa zake ulizipata toka mda mrefu sana kwa ninim hukumweka huju jamvini ili wadau watoe maoni yao labda adhabu ingebadilika??
   
 6. montroll

  montroll JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 288
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Mwacheni mrema jamani, amepigana sana na sasa amekata tamaa, ameamua kupiga siasa tu.
  He has joined them latently.
  Siku hizi anazuga tu.
  Tumsamehe na tumkumbuke. ni kati ya waasisi wa vuguvugu la kudai haki.

  Mapambano yakudai haki yaendelee mpaka kieleweke, Naamini mrema angekuwa na nguvu angepambana pia.

  Sometimes age does not favor one's guts, we need people with guts now.

  Just passing huh!
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Nov 1, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Ukiona mtu analipishwa hivyo ujue yeye siyo mwizi, bali kawajibika tu kwa nafasi yake na Mwizi Mkubwa ni kigogo tena kutoka kwa Mkulu kama siyo Mkulu mwenyewe
   
 8. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  mie kadi yangu ya ccm nilishatupa zamani gani. unaenda kwa mwenyekiti wa kitongoji kusuluhisha tatizo anakuomba rushwa, khaa. hawana aibu, wanangu nitawaamishia hata somalia kusema kweli
   
 9. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Haiingii akili uwizi mkubwa kama huo, mtu anakatwa 15% ya mshahara wake then baada ya wiki mtu huyohuyo atajipa dhihara ili apate per diem ya kuzirudisha pesa zake alizokatwa.
   
 10. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 180
  dah! Hawa jamaa ccm ni kavu kuliko maelezo. Nalog off
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,862
  Trophy Points: 280
  sanduku la kura ndio suluhisho la yote
   
 12. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Ningerkuwa Kishapu ningeitisha maandamano kumpinga hadi ashtakiwe. Hivi kuna sheria yeyote ya kumfikisha mahakamani kwa wananchi wa kawaida? Haiwezekani wananchi wanateseka kwa kukosa huduma bora hospitalini, dispensary nyingi za kishapu choka mbaya hadi uende kolandoto au shy town! shule za kata ndo usiseme kabisa, barabara ni hatari tupu kumbe jamaa anafakamia pesa ya miradi.

  Huyu ni wakukataa tu, mnaitisha maandamano ya kumkataa, huku kesi ikipelekwa mahakamani, atajificha wapi. I am from Kishapu.
   
 13. m

  mwanza JF-Expert Member

  #13
  Nov 2, 2011
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 508
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 60
  Labda Mrema karne ya 19, leo hii hakuna mtumishi mwenye nafasi nzuri halmashauri anayetegemea mshahara wengi wao wanaishi kwa rushwa hata ukisema hakuna mishahara kazini watakuja na hawatalalamika
   
 14. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #14
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tatizo la sehemu kama kishapu wananchi wanadharaulika maana wanaonekana hawana elimu ya kutosha na umasikini mkubwa kiasi cha kuwaona viongozi na matajiri kama miungu wao. Kitendo cha kuchagua mwarabu tajiri kama mbunge wao kinadhibitisha haya. Siku zote ukiona wananchi wanawalamba miguu matajiri tena wa kiarabu na wahindi ujue hamnazo.

  Kishapu ni jimbo la shinyanga wanaweza kukataa haya kwa kuchagua mbunge makini atakaye Pambana na huu uhuni wa watendaji wa halmashauri. Wabunge matajiri wanashirikiana na watendaji kama hawa kupitisha deals zao tu halafu wananchi mnasubiri chumvi na vilemba wakati wa uchaguzi. Waambie ndugu zako na wazazi wenu kuwa ndo tatizo! Ikibidi mkuu wanyime misaada watabadilika.
   
 15. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #15
  Nov 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,410
  Likes Received: 1,968
  Trophy Points: 280
  kwa kiasi kikuba uliyoongea si sawa kishapu yanaweza kutokea mabadiliko makubwa sana kwa taarifa nilizonazo huyo bwana alishinda kwa sababu mgombea wa cdm alikuwa ni muajiriwa alifanya kampeni mwezi mmoja akarudi kazini na alipata kura za nyingi mimi naamini kwa hali upepo ulivyo watu wenye maisha magumu wanaelewa hivi sasa kuliko wenye raha mfano halisi ni igunga.
   
 16. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #16
  Nov 2, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ​bado sio solution
   
Loading...