Mkurugenzi wa FBI apinga madai ya Trump kuhusu Obama

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945





Mkurugenzi wa shirika la kijasusi la FBI James Comey amekana madai ya rais Donald Trump kwamba aliyekuwa rais wa taifa hilo Barrack Obama alidukua simu yake kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

Bwana Comey amesema kuwa amelitaka shirika la haki nchini humo kukataa madai hayo kwamba Obama aliagiza uchunguzi wa simu za Donald Trump wakati wa kampeni za uchaguzi uliokwisha.

Alikana madai hayo akisema kuwa yanayoonyesha FBI ilivunja sheria.

Hatua hiyo iliripotiwa na gazeti la the New York Times na kuthibitishwa na NBC.

Rais Trump akizungumza kupitia simu.Anasema kuwa Obama alikuwa akidukua simu zake

Idara ya haki haikutoa taarifa ya mara moja kuhusu ombi la bwana Comey.

Vyombo vya habari nchini Marekani viliwanukuu maafisa vikisema kuwa bwana Comey anaamini hakukuwa na ushahidi kuthibitisha madai ya Trump.

Rais huyo wa Marekani kupitia chama cha Republican ambaye anakabiliwa na uchunguzi mkali kuhusu uingiliaji wa Urusi ili kuunga mkono uchaguzi wake hajatoa ushahidi wowote kuunga mkono madai yake kwamba simu zake katika ofisi ya Trump Tower zilidukuliwa.
 
huyu bwege aache kumsakama Obama kwa matatizo yake binafsi. Kila Obama akitaka kuji-distance na siasa huyu bwege anamvuta. Anataka kutengeneza diversion za makashfa yake kwa sasa. Tangu uhuru wa US hakujawahi kuwa na rais asiyeishiwa vituko yeye na wasaidizi wake pale White House. It is clear ni mdoli wa Kremlin.
 
huyu bwege aache kumsakama Obama kwa matatizo yake binafsi. Kila Obama akitaka kuji-distance na siasa huyu bwege anamvuta. Anataka kutengeneza diversion za makashfa yake kwa sasa. Tangu uhuru wa US hakujawahi kuwa na rais asiyeishiwa vituko yeye na wasaidizi wake pale White House. It is clear ni mdoli wa Kremlin.

mdukuzi lazima ashughulikiwe
 
tatizo ni kwamba tangu aingie ofisini, kila baya/gumu linalomfika yeye anamsukumizia Mjaluo Obama hadi sasa watu tumeanza kukereka. Apige kazi aache kulialia

kazi inapigwa kama kawa na mdukuzi atashughulikiwa kama kawa
 
Vita Kati ya elite na middle class, agenda ni cheap labour na ukwasi kwa elite group, elimu ajira ulinzi miundo mbonu na mengineyo kwa middle class ( unaweza kujazilia)
 
Back
Top Bottom