Mkurugenzi wa Barrick Gold adai Makinikia yaliyozuiwa Bandarini Dar yana thamani ya $280 Milioni

Kamati ya Prof Mruma ilisema kuwa kwenye zile Kontena 277 kuna dhahabu ya USD 521.3mil, Copper ya Usd 10.6mil, Silver ya Usd 1.08mil, Iridium ya Usd 105mil, Iron ya 1.2mil, Ytterbium ya Usd 7.5mil, Beryllium ya 3.8mil, Tantalum ya Usd 1.3mil, Rhodium ya Usd 0.689mil, Lithium ya Usd 0.649mil, na Sulphur ya Usd 0.844mil.

Jumla kuu ya thamani ya madini yote kwenye zile kontena 277 walipata Usd 652.663 million.

Asante sana Mkuu,

Sasa hivi yatauzwa kwa bei gani?
Tofauti na iliyotajwa mwanzo ni kiasi gani?
 
Jamani Tungeacha kumjadili huyo Mshamba, alinikela sana alivyoenda Afrika kusini kumshauri yule Mjinga akamate ndege yetu kule Canada kwa sababu ambazo ni za kutunga.
Alishawishi ndege ikamatwe Afrika kusini kwa kushirikiana na TL
Duh!
Maoni yako yanaonyesha una hasira sana na huyu jamaa!

Naomba umsamehe kwa sababu kusamehe ni ibada!
 
Hapa sioni jipya ila kwakuwa huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu basi kampeni ndiyo hizo zimeshaanza kwa namna ya kuwapamba watu fulani na wengine kuwachafua.

Mikataba mibovu toka mwanzo ni nani walioingia ni akina Mh Zitto, Mh Lissu na watu wao? Au ni ccm na serikali yake kupitia kwa wagonga meza wao?? Tutakutana kwenye majukwaa wakati wa kampeni ukifika na siyo humu jamvini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu;
Utaonaje jipya kama hujui kuukuu?

Waache wanajua kuukuu waone jipya!
 
Mkuu;
Utaonaje jipya kama hujui kuukuu?

Waache wanajua kuukuu waone jipya!
Siku hizi umekua na mtindio wa ubongo sana. Kishika uchumba kiliahaidiwa na Barick wenyewe. Mchanga tuliizuia na sasa inasafirishwa sasa kinachofurahisha ni nini? Mchanga usingekuwepo kisheria tungesema tunayauza sisi ila bado ni yao furaha ni nini sasa.

Shida kubwa ambayo utawala huu unakosea ni pale mtu akitoa maoni yake wao wanachukulia kama ni sheria na kumchukulia kama adui...upumbavu mtupu.

Muulize Lugora kwanini alisema jeshi la shetani alikua anamaanisha nini wkati anampamba mh Rais
 
Dollar milioni 280?
Si tuliambiwa thamani yake ni dollar bilioni 108? Iliko kokotolewa gari aina ya Noah kwa kila mtanzania?
Kweli kushangaa ruksa ila usisahau kuchanganya na yakwako ukiyaacha ya mbayuwayu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo ni jumla ya pesa tokea mwanzo wa makinikia kusafirishwa nje ya nchi na sio thamani ya makontena yaliyoshikiliwa bandarini.
 
Kuna jamaa mmoja aliwaita kina Mruma rubbish, wana muambia huu sio mchanga kama mchanga wetu wa Baharini, nyuso zenu mnazificha wapi mkisikia taarifa kama hizi? sasa hivi hao Wamekimbilia nje kupigania human rights,from politicians to human rights,hayo ni madhara ya kushindwa kukubali ukweli.
Ukweli una tabia ya kutopenda kupuuzwa!
 
Siku hizi umekua na mtindio wa ubongo sana. Kishika uchumba kiliahaidiwa na Barick wenyewe. Mchanga tuliizuia na sasa inasafirishwa sasa kinachofurahisha ni nini? Mchanga usingekuwepo kisheria tungesema tunayauza sisi ila bado ni yao furaha ni nini sasa.

Shida kubwa ambayo utawala huu unakosea ni pale mtu akitoa maoni yake wao wanachukulia kama ni sheria na kumchukulia kama adui...upumbavu mtupu.

Muulize Lugora kwanini alisema jeshi la shetani alikua anamaanisha nini wkati anampamba mh Rais
Kusema siku hizi nimekuwa na mtindio wa ubongo inaonesha unanifuatilia kwa karibu! Ninakushukuru kwa kunifuatilia na kupoteza muda wako ukilinganisha historia yangu katika ujengaji hoja! Endelea kunifuatilia kwa sababu unaonekana ni mmoja wa mashabiki wangu hapa Jamiiforums!

Nadhani Barrick Gold waliamka tu na kusema watatoa kishika uchumba bila shinikizo kutoka serikalini!

Nadhani hata mchanga waliozuia hakuna lililofanyika na serikali imeamua ACACIA iendelee kama ilivyokuwa mwanzo (default mode)!

Yaani ACACIA imerudi kama ilivyokuwa kabla ya mwezi Agosti 2016!
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom