Mkurugenzi wa baraza la mitihani ajiuzulu haraka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi wa baraza la mitihani ajiuzulu haraka

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mkombozi, Oct 7, 2008.

 1. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2008
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ndugu zangu

  Nimekua nikifuatilia kwa karibu utendaji wa baraza la mtihani la Taifa la Tanzania yaani NECTA. Utendaji wake unasikitisha sana ukiongozwa na Dr Ndalichako. Nimekua nikisikia mara vyeti vimefojiwa, kwa mfano wale wa BOT, Baraza lenyewe lilikiri wazi watu wanafoji vyeti, hii ni udhaifu mkubwa kwa baraza

  Utaifu mwingine uliojitokeza jana ni swala la kuvuja mitihani hasa wa Basic Mathematics, hiki ni kitendo cha aibu na kashfa kubwa sana. Kwa nji za wenzetu ni haraka sana kwa mkurugenzi wa baraza kujiuzulu tena haraka sana. Hapa Tanzania ni mpaka ashinikizwe. Mimi nadhani ni muda muafaka kwa mkurugenzi wa NECTA kujiuzulu na pia baraza nzima kubadilishwa.

  Je sisi tutakua na uhakika gain kua mitihani mingine haijavuja?Kama hesabu imevuja basi hamna shaka kua mengine nayo yamevuja. Hii inakuja kutuletea viongozi wa Kirichmond, wazee wa Vijicent n.k

  Kwa mtazamo wangu baraza la mitihani la taifa libadilishwe lote, utendaji wake unashuka
   
 2. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hivi akishajiuzulu hiyo mitihani haitavuja tena?Kwani kabla yake yeye mitihani ilikuwa haivuji?
  Think of a more critical and solution oriented agenda!Siku hizi TZ kujiuzulu imekuiwa fasheni ama?Suala hapa ni kwamba wale wahusika wakuu katika kuvujisha mitihani wachukuliwe hatua madhubuti za kisheria na siyo kujiuzulu tuu!
   
 3. M

  Masatu JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hii dhana ya kuwajibika umepoteza maana kabisa Bongo....
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ivi garama za kurudia izo paper jamani zinatoka wapi?
  Mi nijuavyo papaer zinakuwaga mpaka 3 ikivuja ya kwanza wananyuka ya pili then na ya 3 kama ya 2 imevuja.
  Poleni wadogo zangu najua itakuwa imewakwanza.
  Wajitaidi kuwa makini hao necta as wakijiuzulu haisaidii toka enzi zile hayo mambo yapo.
   
 5. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,278
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  dats why i love ma country tz...de mista prezidaaa is very busy nw with his bday party nadhan alitaka aitangaze iwe public holiday!

  nyie mnaodiriki ku ask gharama za kurudia mitihani zatoka wapi,u mus b kiddin!our nchi is not dat poor if u maskini sema ni weye mwenyewe u maskini sio tanzania!

  hilo la watu kuwajibika huko necta u kip on dreaming cz it wont happen actually watakao wajibishwa kama kawaida ni wanafunzi!utasikia shule flani zimefungiwa zimefutwa etc wakati pepa imevuja nchi nzima!oops sorry kwa kuwapa bichwa necta kuw aimevuja moja tu,pepa zimevuja nikimaanisha hata za next week mie mwenyewe huku ughaibuni ninazo form 4 wawasiliane nami tu vyema!
   
 6. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2008
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu kevo umeongea point sana,mie ni katika wale waliovunja rekodi ya kuiba mitihani mpaka mitihani yote ikafutwa.Nilifikiri kipindi kile lingetafutwa suluhisho la kudumu,kumbe wapi bwana na mbaya zaidi na teknolojia nayo imekua.

  Nafikiri kwa sasa tubadilishe mbinu,sisi wenyewe tuwe wakali.Wote wanaohusika na kuvuja kwa mitihani hii tunawawajibisha kwa kuwapa adhabu kali ambayo itakuwa ni fundisho kwa wengine.hii iwe inaendelea mpaka tatizo linaisha.

  lakini kwa kuwa nafasi zenye tunapeana kwa kujuana,hivyo tunaoneana haya tuandike maumivu.siku hizi hadi vyuoni kuvuja mitihani ni suala la kawaida,sasa wewe unategemea tutakuwa na wasomi wa aina gani na viongozi wanaotokana na wasomi hawa watakuwaje.
   
 7. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mitihani (maswali na majibu) form 4 mwaka huu Tanzania inapatikana kwa SMS!!!!!!!!!!!!!!!
   
 8. N

  NGAUTI Member

  #8
  Oct 28, 2008
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  Kashfa ya mwaka Baraza la Mitihani

  2008-10-27 13:57:26
  Na Waandishi Wetu


  Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), limesambaza vyeti bandia vya matokeo ya kidato cha nne mwaka jana, (result slip) katika shule mbalimbali za sekondari nchini.

  Wanafunzi walioathirika na hatua hiyo, ni wale waliohitimu kidato cha nne mwaka jana, na baadhi yao wameanza kupata misukosuko, ikiwemo kufikishwa mahakamani kwa madai ya kughushi.

  Akizungumza na Nipashe nyumbani kwake Magomeni, mmoja wa wazazi wa wanafunzi hao, Rehema Mlata, alisema mtoto wake, Alexander Gundula (22), hivi sasa yupo mahabusu mjini Mbeya, kwa kosa lililofanywa na NECTA, kusambaza vyeti hivyo.

  Alexander alikuwa miongoni mwa askari wanafunzi katika Chuo cha Magereza Kiwira, mkoani Mbeya.

  Mlata, alisema Alexander alisoma na kuhitimu katika Shule ya Sekondari Azania, mkoani Dar es Salaam kati ya mwaka 2004 hadi 2007.

  Uongozi wa Azania, kupitia waraka wake wa Oktoba 3, mwaka huu kwa Mkuu wa Mafunzo, Chuo cha Magereza Kiwira, umethibitisha mwanafunzi huyo kusoma katika shule hiyo.

  Mlata alisema Alexander alichukua result slip shuleni hapo Februari mwaka huu, kwa ajili ya kujiunga na Magereza, na kwamba alifanikiwa kuanza mafunzo chuoni hapo.

  Alisema Septemba mwaka huu, Alexander alikamatwa mjini Mbeya na kufikishwa mahakamani, akidaiwa kughushi result slip yenye namba S0101/0032, aliyopewa na uongozi wa Azania.

  Ilidaiwa kuwa hatua hiyo ilifikiwa baada ya Magereza kuthibitishiwa na NECTA, kuwa cheti hicho kilikuwa na kasoro zilizokifanya kisifanane na vingine vilivyotolewa mwaka jana, hivyo kuamua kwamba kilikuwa cha kughushi.

  Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Magereza, ilimwandikia barua Alexander, yenye namba HQC.58/X1/287, ikielezea kuachishwa mafunzo kutokana na kosa la kughushi cheti hicho, na hivyo kukosa sifa ya kuajiriwa.

  Kufuatia uhakiki wa ajira uliofanywa na kamati ya uhakiki kutoka Makao Makuu ya Magereza kuanzia tarehe 31 Agosti mwaka 2008 hadi Septemba mwaka huu, imedhihirika kuwa cheti cha kufuzu masomo ni cha kughushi hivyo moja kwa moja unapoteza sifa za kuajiriwa kama askari Magereza, ilieleza sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Kaimu Kamishna Mkuu wa Magereza, E.M. Nkuku.

  Mlata alisema alikwenda kuonana na uongozi wa Magereza jijini Dar es Salaam, na kujibiwa kwamba uthibitisho kwamba cheti hicho kilikuwa cha kughushi, ulitolewa na NECTA.

  Mzazi huyo alifanikiwa kupata nyaraka kadhaa zinazothibitisha kuwa result slip hiyo, ilitolewa katika Shule ya Sekondari Azania.

  Kwa upande wake, uongozi wa Azania uliandika barua tofauti, ikiwemo namba AZ/BMT/19, kwenda NECTA, ikieleza kuwa Alexander ni mwanafunzi halali wa shule hiyo na result slip husika ilikuwa halali na ilitolewa shuleni hapo.

  Lakini Magereza waliendelea na msimamo wao kwamba wamethibitishiwa na Baraza la Mitihani kuwa result slip hiyo ni feki, alisema.

  Mlata alionyesha barua ya Baraza kwenda Magereza inayotaka Alexander achukuliwe hatua za kisheria, ili iwe fundisho kwa wengine wenye kawaida ya kughushi.

  Hata hivyo, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Azania, Benard Ngoze, alilithibitishia gazeti hili kuwa Alexander alikuwa mwanafunzi halali wa shule hiyo, na kwamba result slip iliyotolewa shuleni hapo ilitoka NECTA na si ya kughushi.

  Alisema vyeti hivyo vilipelekwa shuleni hapo na NECTA mwaka jana, na kwamba vijana wengi wanaokutwa navyo hivi sasa wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.

  ``Zile result slip walileta wenywe Baraza kwa dispatch na tukazipokea, wanafunzi walikuwa wakija kila mtu kwa wakati wake, wanalipia Sh. 5,000 na kuchukua, sasa wanaziruka wakati zimetoka kwao?`` alihoji.

  Alisema alishaandika barua mara kadhaa kwa uongozi wa Baraza la Mitihani na Magereza kuthibitisha kuwa result slip ya Alexander ilipatikana kihalali shuleni hapo, lakini inashangaza kuona bado wahusika wanaendelea kumtia msukosuko kijana huyo.

  Baada ya kugundua kuwa ni kweli hizo result slip zimetoka kwao, Baraza walichukua nyingine 17 zilizobaki hapa shuleni na walisema wanaenda kuwashughulikia watu wa idara ya uchapaji, kwamba walihusika na udanganyifu huo, alisema.

  Alisema inawezekana watu wa idara hiyo katika Baraza, waliuza result slips halisi na kisha kuchapisha za kughushi na kusambaza katika shule mbalimbali nchini.

  Walipokuja hapa tuliwaambia watu wa Baraza kuwa wanastahili kushtakiwa kwa kutengeneza vyeti bandia hata sisi tumeanza kuogopa, kama taasisi nyeti kama hii inafanya vitu vya ajabu kama hivi nani tutakayewaamini, alihoji Mwalimu Ngoze.

  Baraza hilo limekiri kutokea kosa hilo katika barua yake ya Oktoba 13, mwaka huu, ikiwa na kumbukumbu namba MTS.2/14/Vol.L.IV/65, ya kumwomba radhi Alexander kwa kosa lililofanyika.

  Uchunguzi katika kumbukumbu za Baraza la Mitihani Tanzania umeonyesha kuwa result slip ya Alexander Gundula ni sahihi.

  Tayari tumemwandikia Kamishna Mkuu wa Magereza kumjulisha kuhusu uhalali wa result slip hiyo ambayo pia imerudishwa kwake tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza, ilisema barua hiyo iliyosainiwa na Kaputa kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk Joyce Ndalichako.

  Ingawa Baraza hilo halikukiri moja kwa moja katika barua yake kuwa result slip hizo zilitolewa na Baraza hilo, maofisa wake waliokwenda shule ya Azania, walikiri kuwa zilitolewa na taasisi hiyo yenye jukumu la kuandaa mitihani nchini.

  Msemaji wa Magereza, Omari Mtiga, alisema uhakiki wa vyeti vya askari wanafunzi, ni mchakato wa kawaida unaofanywa na jeshi hilo.

  Mtiga aliyeahidi kulifutilia suala hilo kwa undani, alisema utaalamu wa kubaini ikiwa vyeti vilivyowasilishwa na wanafunzi ni sahihi ama vimeghushiwa, unafanywa na NECTA.

  Wakituambia kwamba cheti fulani kimeghushiwa, sisi tunaamini hivyo na hatua inayofuata ni kumfikisha mhusika katika vyombo vya sheria, alisema.

  Hata hivyo, Mtiga alionyesha kushangazwa na tukio hilo alilolifananisha na mchezo wa kuigiza, na kusema taarifa zaidi itatolewa leo.

  ``Njoo Jumatatu, mimi nitakuwa nimesafiri, lakini taarifa zaidi utazipata kwa huyu Kaziulaya, ni mmoja wa wasaidizi wangu,`` alisema.

  Kwa upande wake, Dk. Ndalichako hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo, kwa madai kuwa halijui.

  ``Kuna maamuzi yanayofikiwa na wasaidizi wangu, naomba tuwasiliane kesho, nitakuwa nimelifuatilia na kukupa jibu, nipigie simu kabla hujaja ofisini kwangu,`` alisema.

  Hata hivyo, Nipashe ilipowasiliana naye kwa mujibu wa ahadi yake, Dk. Ndalichako alidai yupo kwenye mkutano, na baadaye alipopigiwa mara kadhaa, simu yake ya mkononi ilikuwa inaita bila kupokewa.
  Taarifa nyingine zilizopatikana hivi punde, zilidai kuwa, Magereza imeagiza Alexander kuripoti chuoni hapo na kuendelea na mafunzo, baada ya barua ya NECTA kuthibitisha kuwa result slip aliyonayo imetolewa na Baraza hilo.

  Imeandaliwa na Mashaka Mgeta na Joseph Mwendapole

  SOURCE: Nipashe

  BARAZA LA MITIHANI KUMEOZA JAMANI.KWA STAILI HII,WATAFUNGWA WANAFUNZI HALALI NA WEZI WA VYETI WATAPETA.WAZIRI WA ELIMU YUKO WAPI?INASIKITISHA
   
 9. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,187
  Likes Received: 681
  Trophy Points: 280
  NECTA wakati wa kusafisha jumba lenu umefika. Swala la vyeti bandia na mitihani kuvuja yametuchosha. Mfumo mzima wa mitihani na utoaji vyeti inabidi kusukwa upya ili kutatutua/kupunguza haya matatizo yaliyojikita mizizi kwa sasa. Tupunguze au kuacha kabisa kufanya kazi kwa mazoea ili kondoa kasoro za kiutendaji zinazotukabili.
   
 10. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2008
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  This is very very serious,kama kweli kijana alex kafukuzwa chuo na kuswekwa ndani basi mara moja akusanye ushahidi wote awapeleke mahakamani.yaani ukisikia bingo ndo hii yeye akadai pesa yoyote anayotaka na asikubali kurudi tena chuoni magereza,yaani yeye iwe mbele kwa mbele kuwapeleka kwa pilato ili liwe funzo kwa watu wengine!ingekuwa mimi sa hizi naogelea kwenye mapesa maana necta na magereza(unawa sue pamoja) lazima wangeomba mediation.
   
 11. Zilla The G

  Zilla The G JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2017
  Joined: Dec 26, 2014
  Messages: 469
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 60
  kazi ipo!!


  Tunafukua makaburi!!!
   
Loading...