Mkurugenzi wa Barabara Ajiua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi wa Barabara Ajiua

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Morani75, Nov 18, 2007.

 1. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2007
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wandugu wenzangu wa Jambo, naomba kuwasalimia.....

  Nimeona hii habari kwenye gazeti la Nipashe la jana na nimeona niweze kuwashirikisha... Kwa wale tuliofanya kazi kwenye sekta ya Miundombinu kama mimi kwa kweli nimeshtushwa sana na tukio hili na limeacha maswali mengi sana katika kichwa changu ukizingatia matatizo tuliyonayo hivi sasa katika sekta hiyo.

  Mungu ailaze roho ya ndugu yetu pema peponi, Amina

  Article ni hiyo hap chini:

  Mkurugenzi Miundombinu ajimaliza kwa risasi
  2007-11-18 10:48:23
  Na Anna Nkinda wa Jeshi la Polisi


  Mkurugenzi wa Kampuni ya Trunk Roads Tanzania, Bw. Leopord Mjungi (53) amejiua kwa kujipiga risasi kifuani.?Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Kamishna Msaidizi wa Polisi Ramadhani Mssika alisema kuwa, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki, saa tisa alasiri katika kijiji cha Magata Katuranga wilani Muleba Mkoani humo.

  Kamanda Mssika alisema, Bw. Mjungi ambaye alikuwa mfanyakazi wa Wizara ya Miundombinu, alikuwa kijijini kwao kuanzia ?Novemba 11 akitokea jijini Dar es Salaam, alijipiga risasi kwa bastola aina ya Browning Cal. No. 9mm Serial No. 245NW70768.

  ``Alikwenda nyumbani kwa bibi yake aitwaye Regina Kwebunaya (100) kwa ajili ya kumsalimia na baada ya kuwaaga ndugu zake ili aanze safari yake ya kurudi jijini ?Dar es Salaam, ndipo alipoingia chumbani kwake na kujipiga risasi,`` alisema Kamanda Mssika.?

  Kwa mujibu wa Kamanda huyo, baada ya polisi kufika eneo la tukio na kufanya uchunguzi, walikuta tiketi ya ndege iliyokuwa inaonyesha kuwa angesafiri siku hiyo ya tukio kwenda Dar es Salaam kupitia Mwanza.

  Bw. Mssika alisema kuwa, Jeshi la Polisi Mkoani humo linaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha tukio hilo.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. D

  Dotori JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2007
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  It will be good to know what led to his death? It is sad though
   
 3. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2007
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  HUYU NAHISI NI FISADI ALISHIRIKIANA MA MAGUFULI NA KWA SASA ANAONA UNGA UTAMWAGIKA MUDA WOWOTE SO KAAMUA KUKWEPA SO (SPECULATION). Mungu aiweke roho yake mahali pema.
   
 4. O

  Ogah JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Duuhhh

  Tumepoteza "MASHINE" muhimu sana pale Wizarani. Amini usiamini aliyemfanya Magufuli ang'ae pale Wizarani ni huyu Mujungi aliyetutoka. Tumepoteza mtu makini sana pale miundombinu.

  Pole kwa familia na pole kwa Taifa la Tanzania, Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi. Amina
   
 5. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #5
  Nov 18, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  sasa amejiua kwa sababu ipi? au ameuliwa na kutengenezwa mazingira haya?
   
 6. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #6
  Nov 18, 2007
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,278
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  ccm hiyoooooo........!!!!!!
   
 7. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #7
  Nov 18, 2007
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,278
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  guys natania tuu li chama letu tawala....as hii ni miaka yao ya shetani kila baya lazima liende kwao...
  in the other hand its so sad kumpoteza binadamu mwenzetuu Mungu ailaze roho yake pema peponii
  Amen
   
 8. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #8
  Nov 18, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Huenda kajiua kwa sababu za kawaida kabisa, huenda ni migogoro ya kifamilia tu. Ukute jamaa alikuwa na matatizo na familia yake (wazazi), maana taarifa zinasema kuwa alijiua baada ya kutoka kuwatembelea wazazi wake kule kijijini. Nadhani tungesubiri majibu ya uchunguzi kabla ya kuendelea na 'conspiracy theories'
   
 9. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #9
  Nov 18, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Well,
  Alikosa upendo na mapenzi ya karibu- toka kwa marafiki wa karibu na watu wa familia yake! Asingefikia hatua hiyo
   
 10. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #10
  Nov 19, 2007
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Chanzo: Majira
  Novemba 18, 2007
   
 11. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2007
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Hii kali, inaelekea jamaa alikuwa na mpango wa kujiua kawapunguzia gharama za kumsafirisha ndugu zake
   
 12. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #12
  Nov 19, 2007
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Hapana, hebu soma hii:

  Huyu nyanya yake inaelekea kazeeka na aliona anakaribia hatma ya maisha yake (100yrs!) sasa yawezekana kabisa alimwambia "Mwanangu sasa mimi nakaribia kukipa,,, tafadhali pokea mikoba yangu... na ukikataa nitakugeuza .... ". Jamaa kusikia hivi akaona bora nife kuliko fedheha :)

  Am just kidding!
   
Loading...