Mkurugenzi TPDC abadili gia angani, asema hakuna uhaba wa mafuta nchini

..amesema tpdc hawana uwezo wa kuhifadhi mafuta.

..wanataka kujenga uwezo huo kufikia miezi 3 mpaka 6.
 
Mkurugenzi wa shirika la maendeleo ya petroli Tanzania amesema Tanzania haina uhaba wa mafuta nchi ikiwa ni tofauti na kauli iliyonukuliwa na gazeti la Nipashe wakati akiongea na wanahabari. Mapema January Makamba alikanusha Tanzania kuwa na uhaba wa mafuta na kumtaka mkurugenzi huyo kwenda kujieleza ofisini.

Pia, soma=> Makamba: Hakuna uhaba wa mafuta nchini, amtaka mkurugenzi TPDC akajieleze kabla hawajachukua hatua

=> TPDC: Mafuta yaliyopo yatosha siku 15

Mataragio alisisitiza kuwa Tanzania ina akiba ya kutosha ya mafuta.

"Ningependa kutoa ufafanuzi kuhusu habari ambayo imeandikwa leo na gazeti la Nipashe, ambayo inasema kwamba nchi hii ina mafuta ya kutosha kwa siku kumi na tano(15). Hiyo siyo kweli kabisa, nchi yetu ina mafuta mengi ya kutosha."

"Kitu ambacho nimeongea jana niliongelea uwezo wa nchi katika kuhifadhi mafuta, na nikasema kwamba mipango ya nchi kupitia TPDC tuongeze uwezo wetu wa kuhifadhi mafuta kwenda miezi mitatu(3) mpaka miezi sita(6)."

"Kwa hiyo nipende kuchukua nafasi hii kuwahabarisha wananchi wote kwamba hakuna haja ya taharuki, mafuta tunayo ya kutosha, na tuna uwezo wa kuwahudumia bila shida, kwa hiyo haina haja ya kupanic kwamba mafuta hayatoshi au kuna upungufu wa mafuta."


Sasa kama uwezo wetu wa kuhifadhi mafuta ni siku 15 tu, kwa vyovyote vile mafuta yaliyopo yanatosha si kwa zaidi ya siku 15, sasa mbona amesema kitu kilekile tena?
 
Basi alinukuliwa vibaya; hii inchi inaendeshwa kwa uongo na unafiki kwa asilimia 80. Ndo maana haiendelei
Kama anasema nchi inataka iongeze uwezo wa kuhifadhi mafuta kutoka siku 15 za sasa hadi siku 90 (miezi mitatu), kwahiyo mafuta yaliyopo nchini sasa hivi yanauwezo wa kututosha siku ngapi kulingana na uwezo wetu wa sasa?
 
Back
Top Bottom