Mkurugenzi TPA: Mkataba wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ungeifilisi Tanzania

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Bandari ya Bagamoyo ingefilisi, kuuza nchi

Sunday May 19 2019
pic+kokoko.jpg

Kwa ufupi
Pamoja na kusamehewa kodi na ushuru mbalimbali kama zile za lazima kisheria, kulipwa fidia ya hasara ya kibiashara watakayopata kwa mujibu wa mahesabu yao, mwekezaji pia aliweka sharti la kuachiwa ajipangie bei ya kuwatoza watakaosafirisha mizigo kupitia bandari hiyo,.

By Peter Saramba na Jonathan Mussa, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Mwanza. Wakati Watanzania wa kawaida, wabunge na Spika Job Ndugai wakiendelea kujiuliza kwanini Serikali imesitisha majadiliano kuhusu uwekezaji kwenye mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, imebainika kuwa Serikali ingefilisika iwapo ingekubali masharti ya mwekezaji.

Pamoja na kusamehewa kodi na ushuru mbalimbali kama zile za lazima kisheria, kulipwa fidia ya hasara ya kibiashara watakayopata kwa mujibu wa mahesabu yao, mwekezaji pia aliweka sharti la kuachiwa ajipangie bei ya kuwatoza watakaosafirisha mizigo kupitia bandari hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deusdedith Kakoko akizungumza leo Jumapili Mei 19,2019 na Mwananchi katika mahojiano maalumu Jijini Mwanza, amesema licha ya Serikali kukubali kusamehe ushuru wa stempu, ukaguzi wa forodha (customs inspection) ile ya ukaguzi wa meli ambayo ni tozo ya Kimataifa na kufungua kituo (one stop center) cha kuhudumia biashara katika bandari ya Bagamoyo, mwekezaji aliibua masharti mengine mapya 14 yasiyotekelezeka.

Kakoko ametaja masharti mapya yaliyoibuliwa na mwekezaji kuwa ni ya kusamehemewa kodi ya mapato, kodi ya taasisi, kodi ya ongezeko la thamani ya mali, kodi ya mapato kwa watu binafsi, ushuru wa Seriali za mitaa na kodi ya majengo.

“Mwekezaji pia alitoa mashari ya kusamehewa tozo ya ardhi, kodi ya fidia kwa wafanyakazi, kodi ya uendelezaji wa ujuzi, kodi ya forodha na kodi ya ongezeko la thamani, VAT.

“Walitaka wasamehewe kodi, ushuru na tozo zote za vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini; hii ingesababisha wageni, hata wasiohitajika wala kuwa na kazi ya kufanya kujazana nchini,” amesema Kakoko.

Amesema mwekezaji aliweka masharti hayo kwa kisingizio kwamba hakuna shehena ya kutosha na kuhoji inakuwaje mwenye fedha awekeze kwenye biashara isiyolipa.

“Hakuna shehena ya kutosha wakati wewe (mwekezaji) unataka kuwekeza kwenye reli na bandari. (Ni lazima) Unakuja kwa sababu biashara ipo” amesema Kakoko.

Amesema masharti hayo yangekubaliwa, ni dhahiri Taifa lingeambulia sifuri huku mwekezaji akichukua asilimia 100 ya kila kinachopatikana licha ya ukweli kwamba pande zote zimewekeza.

Mkurugenzi Mkuu huyo ametaja ardhi, rasilimali watu na nguvu kazi pamoja na mazingira bora ya uwekezaji uliopi nchini kuwa ni sehemu ya uwekezaji wa Serikali huku mwekezaji akitakiwa kuleta mtaji.

“Wakilegeza masharti na kukubali tugawane sawa sawa hakuna tatizo; waje na fedha zao. Lakini wahakikishe nasi tunapata. Haiwezekani sisi tupate sifuri lakini wao wapate asilimia 100,” amesema
 
Ingefilisika kweli kwa kuwa inapenda mteremko ikidhani kuwa mikopo ya wachina haina sharti la kudata demokrasia ndani ya nchi, kwamba wachina ni watu wema hawaingilii mmbo yako ya ndaninya nchi kama walivyo mabeberu. Sasa hamna pa kukimbilia lazima mwapigie mabeberu magoti.
 
Ndio kusema unamkubali Rais Magufuli kiaina?
Ndugu Chamoto,BAK hajasema kuwa anamkubali Magufuli bali anajaribu kutupasha kuhusiana na mustakabali wa taifa kwa sababu ni wajibu wake kama Raia na hii inadhihirisha kuwa hata kama wewe ni mpinzani tukija kwenye swala kubwa kama hili inatubidi tu kusimama kidete maana tungefilisiwa Watz tungekosa hata pa kunyea.
Mchina hajali mlikuwa marafiki kwa mda gani yeye maslahi mbele
 
Magu amezuia mkataba wa hovyo, BAK kaleta mada inayoelezea kitu kizuri kilichofanywa na awamu hii sasa huoni kuwa anakubali (japo kwa shingo upande) mazuri anayoyafanya Magu?
 
Umebahatika kusoma ripoti ya CAG Assad na kuona madudu na maovu ya huyo nduli na dikteta wa Ikulu? Ni Rais yupi aliwahi kuchota trillions hazina bila ya idhini ya Bunge? Ni yupi kati ya waliomtangulia aliwahi kugomea CAG asikague matumizi makubwa yaliyofanywa na yeye? Ni yupi kati ya waliomtangulia alipandikiza chuki za kutisha miongoni mwa Watanzania hadi kutishia amani na mshikamano wa Watanzania uliodumu miaka mingi sasa?

Huoni kuwa awamu ya tano umetuokoa na uwekezaji huu wa hovyo ambao wengi tuliupinga vikali miaka iliyopita?
 
Usiniwekee maneno yako mdomoni mwangu.Eti namkubali huyo fisadi kwa shingo upande? 😳😳😳Vipi wewe!? Usilazimishe kisichokuwepo wala ambacho hakitakuja kutokea eti mimi nimkubali huyo nduli wa Ikulu.

Magu amezuia mkataba wa hovyo, BAK kaleta mada inayoelezea kitu kizuri kilichofanywa na awamu hii sasa huoni kuwa anakubali (japo kwa shingo upande) mazuri anayoyafanya Magu?
 
Umebahatika kusoma ripoti ya CAG Assad na kuona madudu na maovu ya huyo nduli na dikteta wa Ikulu?
Nimeisoma na kama umeipitia vizuri utaona kuwa madudu unayoyasema yalijumuisha awamu zilizopita.
Ni Rais yupi aliwahi kuchota trillions hazina bila ya idhini ya Bunge? Ni yupi kati ya waliomtangulia aliwahi kugomea CAG asikague matumizi makubwa yaliyofanywa na yeye?
Umesahau EPA, MEREMETA, escrow na hata ITPL
Ni yupi kati ya waliomtangulia alipandikiza chuki za kutisha miongoni mwambie Watanzania hadi kutishia amani na mshikamano wa Watanzania uliodumu miaka mingi sasa?
Tuliona serikali ya Mkapa ilivyowafanya waislam mwembechai na kule zanzibar, tulilaani sana hapa wakati mke wa Dr. Slaa alivyopigwa kichwani mpaka akachirizika damu bila kusahau Mwangosi alivyotolewa utumbo, ni chuki zipi zinazopandikizwa awamu hii?
 
Hapo watakuwa wamenyimwa rushwa ndio maana wameyaona haya yote, na wachina hawawezi kutoa rushwa mara mbili.
 
Bandari ya Bagamoyo ingefilisi, kuuza nchi
Sunday May 19 2019
pic+kokoko.jpg

Kwa ufupi
Pamoja na kusamehewa kodi na ushuru mbalimbali kama zile za lazima kisheria, kulipwa fidia ya hasara ya kibiashara watakayopata kwa mujibu wa mahesabu yao, mwekezaji pia aliweka sharti la kuachiwa ajipangie bei ya kuwatoza watakaosafirisha mizigo kupitia bandari hiyo,.

By Peter Saramba na Jonathan Mussa, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Mwanza. Wakati Watanzania wa kawaida, wabunge na Spika Job Ndugai wakiendelea kujiuliza kwanini Serikali imesitisha majadiliano kuhusu uwekezaji kwenye mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, imebainika kuwa Serikali ingefilisika iwapo ingekubali masharti ya mwekezaji.

Pamoja na kusamehewa kodi na ushuru mbalimbali kama zile za lazima kisheria, kulipwa fidia ya hasara ya kibiashara watakayopata kwa mujibu wa mahesabu yao, mwekezaji pia aliweka sharti la kuachiwa ajipangie bei ya kuwatoza watakaosafirisha mizigo kupitia bandari hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deusdedith Kakoko akizungumza leo Jumapili Mei 19,2019 na Mwananchi katika mahojiano maalumu Jijini Mwanza, amesema licha ya Serikali kukubali kusamehe ushuru wa stempu, ukaguzi wa forodha (customs inspection) ile ya ukaguzi wa meli ambayo ni tozo ya Kimataifa na kufungua kituo (one stop center) cha kuhudumia biashara katika bandari ya Bagamoyo, mwekezaji aliibua masharti mengine mapya 14 yasiyotekelezeka.

Kakoko ametaja masharti mapya yaliyoibuliwa na mwekezaji kuwa ni ya kusamehemewa kodi ya mapato, kodi ya taasisi, kodi ya ongezeko la thamani ya mali, kodi ya mapato kwa watu binafsi, ushuru wa Seriali za mitaa na kodi ya majengo.

“Mwekezaji pia alitoa mashari ya kusamehewa tozo ya ardhi, kodi ya fidia kwa wafanyakazi, kodi ya uendelezaji wa ujuzi, kodi ya forodha na kodi ya ongezeko la thamani, VAT.
“Walitaka wasamehewe kodi, ushuru na tozo zote za vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini; hii ingesababisha wageni, hata wasiohitajika wala kuwa na kazi ya kufanya kujazana nchini,” amesema Kakoko.

Amesema mwekezaji aliweka masharti hayo kwa kisingizio kwamba hakuna shehena ya kutosha na kuhoji inakuwaje mwenye fedha awekeze kwenye biashara isiyolipa.

“Hakuna shehena ya kutosha wakati wewe (mwekezaji) unataka kuwekeza kwenye reli na bandari. (Ni lazima) Unakuja kwa sababu biashara ipo” amesema Kakoko
Amesema masharti hayo yangekubaliwa, ni dhahiri Taifa lingeambulia sifuri huku mwekezaji akichukua asilimia 100 ya kila kinachopatikana licha ya ukweli kwamba pande zote zimewekeza.

Mkurugenzi Mkuu huyo ametaja ardhi, rasilimali watu na nguvu kazi pamoja na mazingira bora ya uwekezaji uliopi nchini kuwa ni sehemu ya uwekezaji wa Serikali huku mwekezaji akitakiwa kuleta mtaji.

“Wakilegeza masharti na kukubali tugawane sawa sawa hakuna tatizo; waje na fedha zao. Lakini wahakikishe nasi tunapata. Haiwezekani sisi tupate sifuri lakini wao wapate asilimia 100,” amesema
Hongera serikali ya Magufuli kwa kuliona hilo
 
Back
Top Bottom