Mkurugenzi Tanesco abadilisha uamuzi wa kujiuzulu

Status
Not open for further replies.

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,009
Posted Date::11/23/2007
Mkurugenzi Tanesco abadilisha uamuzi wa kujiuzulu
* Aandika barua kwa bodi kubatilisha
* Kuzungumza na waandishi wa habari Jumatatu

Na Tausi Mbowe
Mwananchi

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Dk Idris Rashidi aliyewasilisha barua ya kujiuzulu kwa bodi ya shirika hilo juzi amebadilisha uamuzi wake.

Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana na kudhibitishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Balozi Fulgence Kazaura zilisema kuwa, Dk. Rashidi aliwasilisha barua ya kubatilisha uamuzi wake huo jana.

" Ni kweli nimepokea barua ya Dk Rashidi kubatilisha uamuzi wake wa awali leo asubuhi na kusema kuwa ameamua kufuta uamuzi wake alioufanya awali, " alisema Kazaura.

alisema Alhamisi, Mkurugenzi huyo aliwasilisha barua ya kuomba kujiuzulu wadhifa huo, lakini kabla bodi hiyo kukutana na kutoa uamuzi, aliandika barua kubatitilisha uamuzi wake..

Hata hivyo, Balozi Kazaura alisema katika barua zote, Dk Rashidi hakutoa sababu za msingi za kujiuzulu kwake, na kutaja baadhi ya maneno yaliyopo katika barua hizo.

" Naomba kujiuzulu, sijapata shinikizo kutoka kwa mtu yoyote, nashukuru kwa kufanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja na Tanesco, nashukuru nimejifunza mengi, '' alimnuku Dk Rashidi

Hata hivyo, Balozi Kazaura, alisema Mkurugenzi huyo ametumia busara kubwa kwa kukaa na kufikiri maamuzi yake na uamuzi na kubatilisha.

" Dk Rashidi ni mtu wa busara, kwani ameweza kukaa na kutafakari kisha kuamua kwa kutumia busara ili kuendeleza kutuitumikia kampuni yetu, " alisisitiza.

Kufutia hali hiyo, Balozi Kazaura, alisema bodi hiyo itakutana na kujadili uamuzi huo lakini hakusema ni lini.

Dk Rashidi alikataa kuzungumzia suala hilo na kuahidi kuzungumza na waandishi Jumatatu ya ijayo kwa lengo la kutoa ufafanuzi.

Awali kiwingu kilitanda kuhusu taarifa za kujiuzulu kwa Mkurugenzi huyo, kutokana na taarifa zake za kuchanganya, awali alikataa kabla ya kukiri kupeleka barua ya kujiuzulu kwa bodi hiyo na kudai kuwa anachosubiri ni mchakato wa uamuzi wake kukubaliwa.

Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi juzi usiku aliambia Mwananchi kwamba amepata taarifa za Dk Rashidi kuandika barua ya kujiuzulu, lakini ilikuwa haijafika mezani kwake.

Juzi Mwananchi ilipowasiliana Dk Rashidi majira ya saa 2:30 usiku, alikiri kuandika barua ya kujiuzulu wadhifa wake na kwamba suala hilo sasa lipo katika mchakato wa utekelezaji.

Taarifa za awali zilidai Dk Rashidi alijiuzulu kwa kuandika barua baada ya mvutano uliodaiwa kuibuka katika kikao cha bodi hiyo juzi, kufuatia upinzani mkali kuhusu mkakati wa shirika hilo kupandisha bei ya umeme na gharama za kuunganisha nishati hiyo.

Inadaiwa kuwa, msimamo wa Mkurugenzi huyo katika kikao hicho, ulikuwa kupandisha gharama za umeme, lakini wajumbe wengine wa kikao hicho kilichoongozwa na Balozi Kazaura kilimpinga kikisema kuwa msimamo wake hautekelezeki.

Taarifa hizo pia zinesema kuwa, Mkurugenzi huyo pia alifikia uamuzi huo, baada ya kikao hicho kumpinga katika msimamo wake wa kukikatia umeme Kiwanda cha Saruji Tanga, baada ya kubainika kwamba kinautumia kinyemela bila kulipa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Bodi ya Tanesco ilimpinga kwa kusema kuwa, msimamo huo sio sahihi kwani utatibua mkakati wa serikali wa kudhibiti bei ya bidhaa hiyo.

Taarifa zaidi zinasema kwamba huenda utekelezaji wa hatua ya Dk Rashidi umekwama baada ya Rais Kikwete kumzuia kufanya hivyo.

Dk Rashidi aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco mwishoni mwa mwaka jana kuziba pengo la uongozi wa Net Group Solutions kutoka Afrika Kusini uliohitimisha mkataba wake wa miaka minne Desemba 31 mwaka jana.

Dk Rashidi ambaye amewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) aliteuliwa kushika wadhifa huo kutokana uzoefu wake wa masuala ya uchumi hivyo umuhimu wa kuwa na mtu mwenye uwezo wa kusimamia masuala ya kifedha hivyo kupunguza gharama za uendeshaji wa shirika.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Rashidi alikuwa Ofisa Mwendeshaji Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Rabobank Holland inayosimamia shughuli za benki ya National Microfinance (NMB) tangu Oktoba mwaka juzi.

Vilevile, aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC kati ya mwaka 1992 hadi Juni mwaka 1993 na Mkurugenzi wa Benki ya Akiba Commercial (ACB) tangu mwaka 1999 hadi Machi 2000.
 
Huyu anatapatapa tu wangemwacha tu aishie. Wanapomkubalia abaki ndio anaona shirika linampapatikia kwa sana, na si ajabu akajigeuza Demi-god, na kazi zitakuwa haziendi. Mtu mwenye kiburi cha kutishia kujiuzulu kila anapotofautiana na wenzake, hafai. Kazi za umma zinafanywa kwa ushirikiano, si kuwatishia wenzako kujiuzulu pale wanapokuwa hawakubaliani na mawazo yako. Kama ni kujiuzulu, ondoka kweli usibabaishe watu. Na kazi huwa hailazimishwi mtu, kwa hiyo hakuna ambaye amemkatalia kujiuzulu, ni yeye tu alikuwa ana-"test the waters", sasa ameshaona kina chake. Huyu anapaswa aondoke. Ukitaka kujua hakuwa na nia ya kujiuzulu, ona amewahi ku-withdraw barua haraka haraka kabla haijajadiliwa na bodi. Kama angekuwa sincere, angesubiri jibu la Bodi kama ingemwomba abaki. Ni kama mtu unagombana na mkeo, halafu anaanza kukuchimba mkwara "nipe talaka yangu", ukimpa kweli anarudi kukuangukia miguuni. Ndicho alichofanya huyu Dr Rashid, sioni sifa yoyote wala msimamo wowote alioonesha kwa jambo hili alilolifanya "kitoto" kabisa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom