Mkurugenzi Takule wa BRT: non peformer, alifikaje hapo?

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,882
13,171
Mradi wa BRT jijini umesua sua kwa muda mrefu sana.
Hata hivyo kuanza kwake mradi umekumbana na matatizo mengi sana na sasa imeanzza kudhihirika kuwa uongozi wa BRT ni dhifu sana kimipango kiasi ya kwmba hata viongozi wa juu wameanza kugutuka.

Kimsingi si watu wengi wanafahamu kuwa licha ya kuanza mradi huu, hakuna mipango madhubuti ya mradi iliandaliwa, kiasi kwamba hata stesheni nyingi za mabasi ziko sehemu ambazo ni makazi ya watu ambao hawakuarifiwa au kufidiwa mapema.
Ukiacha eneo la Gerezani lilokuwa na kesi, sehemu nyingine kama Fire NHC, wenye eneo wala hawakushirikishwa juu ya mradi huu.

Mradi ulienda mbali zaidi na kutoa tenda kwa kampuni za kichina, wakati ambapo hata dite yenyewe haijapatikana!!

Mtu lazima atajiuliza, kulikoni huyu Ndugu Takule na uongozi wake unaofanya mipango kwa kubahatisha?
Na alifikaje hapo alipo?

Magufuli jana kasema angekuwa chini yake (Wizara ya Ujenzi) , angempiga chini.

Hata Rais JK kashtukia mpango wa kujenga kituo "cha muda" eneo la Chuo Kikuu kwa fedha za umma kiasi Tshs Bilioni 2.

Mtu wa kawaida atajiuliza hii BRT ni mradi wa Serilkali au wa mtu binafsi?
Na ni dhahiri kuwa Nd Takule na uongozi wake ni non performers , na walifikaje kuwa hapo in the first place?
 
Huyu aliibukiaga kwenye mradi wa USRP tangu miaka ya mwisho ya 1990 ambako baada ya kuboronga ndo kashikishwa huo mradi. Hana mawazo mapya kwani alishachoka.
 
Lazima wampige madongo Lekule kwani wameshindwa kula fedha za huu mradi hivyo nyongo inawachanganya; mbona hawakusema lolote kule kwenye mradi wa Bagamoyo -Msata ambako mabilioni ya shilingi za walipa kodi ziliibwa mchana kweupe na wezi waliohusika wanatesa barabarani?
 
Lazima wampige madongo Lekule kwani wameshindwa kula fedha za huu mradi hivyo nyongo inawachanganya; mbona hawakusema lolote kule kwenye mradi wa Bagamoyo -Msata ambako mabilioni ya shilingi za walipa kodi ziliibwa mchana kweupe na wezi waliohusika wanatesa barabarani?
Kwa hiyo una maana huyo jamaa karuhusiwa kufanya apendavyo?
 
Back
Top Bottom