Mkurugenzi Standard Chatered aleweshwa penzi la mwanafunzi
::Aibiwa vitu vya milioni saba hotelini
::Mwanafunzi apandishwa kizimbani
na primtiva pancras
MWANAFUNZI wa Sekondari ya Green Acres, iliyopo Magomeni, Dar es Salaam, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akituhumiwa kumwibia Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered, Mothusi Dingalo, anayesadikika kuwa mpenzi wake.
Dingalo ni Mkurugenzi wa Benki hiyo nchini Botswana. Anadaiwa kuibiwa fedha hizo katika Hoteli ya Palm Beach, Dar es Salaam.Inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo alimpa dawa za kulevya Dingalo, ili aweze kufanikisha wizi wake.Awali ilidaiwa kuwa Dingalo, alifikia katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski Dar es Salaam na baada ya kuishi hapo kwa siku chache alihamishiwa Palm Beach, ili kupisha ugeni wa Rais wa Marekani, George Bush.
Ilidaiwa kuwa Dingalo akiwa katika mapumziko katika hoteli hiyo, alitokea msichana na kujitambulisha kwake kuwa ni mwalimu, hivyo alimwomba wapumzike pamoja.
Dingalo alikubali ombi hilo na inadaiwa kuwa walilala pamoja na msichana huyo kwa siku moja.
Ilidaiwa kuwa Dingalo, alishtuka asubuhi na kukuta akiwa ameibiwa mali zake, na ndani ya chumba hicho kulionekana kichupa kidogo kinachodhaniwa kilikuwa kimetumika kuhifadhi dawa za kulevya.
Hata hivyo, ilidaiwa kuwa baada ya mshitakiwa kushtuka alikuta ameibiwa vitu mbalimbali vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya Sh milioni 7.
Akisoma mashitaka yanayomkabili mwanafunzi huyo, Inspekta wa Polisi, Nossoro Sisiwaya, alidai kuwa Februari 18, mwaka huu, katika maeneo ya hoteli ya Palm Beach, mshitakiwa alitenda kosa.
Sisiwaya alidai, mshitakiwa aliiba simu mbili, tiketi ya ndege ya kusafiria kutoka Dar es Salaam, Tanzania kwenda Gaborone, Botswana, funguo ya ofisi ya Posta, flash disk tatu na manukato chupa moja vyote vikiwa na thamani ya Sh milioni 7.5.
Hata hivyo, mshitakiwa alikana shitaka, Mwendesha Mashitaka alidai kuwa hana pingamizi la dhamana dhidi ya mshitakiwa huyo.
Hakimu John Msafiri wa Mahakama hiyo, alimtaka mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili na kila mmoja na kusaini mkataba wa Sh 500,000 na Mahakama.
Mshitakiwa alitimiza masharti hayo na yupo nje hadi Machi 25, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.
Source: Mtanzania