Mkurugenzi PSSSF afikishwa mbele ya Baraza la Maadili

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,799
Mkurugenzi wa Mifumo ya TEHAMA katika Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Gilbert William Chawe tarehe 16 Septemba, 2022 alifikishwa mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili ikiwa ni pamoja nakukopa kiasi cha shilingi 200,765,838.00 kinyume na utaratibu wa Mfuko.

Akisoma mashtaka hayo Wakili wa Serikali Bw.Hassan Mayunga alisema kuwa Bw. Chawe alitumia fedha za umma katika mfuko wa PSSSF kiasi cha shilingi 135,630,448.00/=, bila kufuata utaratibu, kwa kuzikopa na kununua gari binafsi hali akijua kuwa fedha hizo hazikutengwa kwenye bajeti ya mwaka 2020/2021.

Aidha, wakili Mayunga aliongeza kuwa katika shitaka la pili, mlalamikiwa akitekeleza majukumu yake ya kikazi kati ya mwaka 2020 na 2021 alipokea na kutumia bila kufuata utaratibu fedha za umma kutoka PSSSF kiasi cha shilingi 65,133,390.00 kwa ajili ya kulipia kodi ya ununuzi wa gari binafsi ambao haukufuata utaratibu.

“Kitendo hicho Mwenyekiti ni kinyume cha kifungu cha 6(1)(a),(b) na (f) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995 kikisomwa pamoja na Kanuni ya 3(2)(a) na (e) ya Kanuni za Udhibiti wa Mgongano wa Maslahi na Kanuni 7(d) na (e) ya Kanuni za Ahadi ya Uadilifu,” alisema.

Shtaka la tatu alilosomewa ni kupokea fedha kiasi cha shilingi 65, 133,390.00 kutoka PSSSF kwa ajili ya kulipia kodi ya ununuzi wa gari binafsi, lakini kiasi hicho kilitumika kinyume na utaratibu na pia hakikutumika kama ilivyokusudiwa.

Mlalamikiwa amekana malalamiko yote matatu.

Ilidaiwa mbele ya Baraza kuwa mlalamikiwa alipata mkopo huo kinyume na sera ya mikopo ya PSSSF na kuwa mkopo huo haukupita kwenye kamati ya mikopo ya taasisi.

Upande wa mlalamikaji uliliambia Baraza kuwa, “Sera ya mikopo ya PSSSF ya tarehe 1/11/2018 kipengele cha 4.2.(b)(viii) kinasema kuwa mfuko utalipa asilimia mia moja ya kodi kwa Mkurugenzi mkuu na wakurugenzi wengine kwa gari jipya, lakini gari alilonunua mlalamikiwa halikuwa jipya bali ni garichakavu.”

Aidha upande wa mlalamikaji uliwasilisha vielelezo mbalimbali ikiwemo mkataba wa mkopo uliosainiwa Aprili 24, 2021, orodha ya wanufaika wa mkopo na hati ya malipo ya tarehe 29 Aprili, 2021.

Hata hivyo, ushahidi kutoka Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) unaonyesha kuwa gari alilonunua Bw. Chawe lenye nambari za usajili T607DTQ lilisajiliwa kwa mara ya kwanza na mamlaka hiyo tarehe 12/6/2020 na mmiliki wake wa kwanza ni Bw. Kipemka Msemembo Musa.

“Mnamo tarehe 4 Mei, 2021 umiliki wa gari hilo ulihamia kwa Bw. Chawe kutoka kwa Salim Cars wa Dar es Salaam. Salim Cars alilinunua kutoka kwa Jaji Musa wakati gari hilo lilisha lipiwa kodi na Serikali,” ulieleza upande wa malalamiko.

Serikali ilinunua gari hilo na kumpa Jaji Musa kama stahiki yake alipostaafu.

Mlalamikiwa amekiri mbele ya Baraza kuwa mmiliki wa kwanza wa gari hilo ni Jaji Musa.

“Ni kweli gari hilo alipewa Jaji Musa kama stahiki yake, lakini aliliacha Toyota kwa lengo la kutafuta mnunuzi mwingine,” alisema Bw. Chawe.

Alipoulizwa kama Salim Cars anayedaiwa kulinunua kutoka kwa Jaji Musa alimuonyesha hati za malipo ya kodi, mlalamikiwa ameshindwa kulithibitishia Baraza.

“Mfuko wa PSSSF ulimlipa fedha za kodi Salim Cars, sio mimi, malipo haya yalilipwa baada ya kujiridhisha na kiasi cha kodi kilichotakiwa kulipwa,’ alisema.

Hata hivyo mlalamikiwa alipoulizwa mbele ya Baraza kama kiasi cha shilingi milioni 13.6 ambayo ni asilimia 10 ya Tsh 135 milioni iliyotakiwa kulipwa TRA kama gharama ya uhamisho wa umiliki wa gari ililipwa ameshindwa kulithibitishia Baraza malipo hayo.

Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma lililokuwa chini ya Mwenyekiti wake Jaji (Mst.) Ibrahim Mipawa limehitimisha vikao vyake vya uchunguzi vilivyoanza Septemba 6 kwa kusikiliza malalamiko tisa (9) ya ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Waliofikishwa mbele ya Baraza ni pamoja na Bw. Geofrey Chibulunje, aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. Hoseah Kashimba Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bi Beatrice Lupi, Mkurugenzi wa Fedha wa PSSSF, Bw. Ernest Khisombi, Mkurugenzi wa Ugavi na Ununuzi wa PSSSF na Bw. Peter Martin Sulle, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu.

Wengine ni Bi. Kapwete Leah John, Mkurugenzi wa sheria wa EWURA, Dkt. Ayoub Chacha Rioba, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Jerome Philip Kamwela, Mkurugenzi wa Tathimini na Ufuatiliaji wa TACAIDS na Bw. Gilbert William Chawe, Mkurugenzi wa Mifumo ya TEHAMA wa PSSSF.

Vikao vya Baraza la maadili ya viongozi wa Umma ni utekelezaji wa matakwa ya Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kuhusu kusimamia tabia na mwenendo wa viongozi wa umma waliotajwa katika Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Sekretarieti.PNG


Chanzo: Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
 
Mkurugenzi wa Mifumo ya TEHAMA katika Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Gilbert William Chawe tarehe 16 Septemba, 2022 alifikishwa mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili ikiwa ni pamoja nakukopa kiasi cha shilingi 200,765,838.00 kinyume na utaratibu wa Mfuko.

Chanzo: Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
Huyu ndie mpwa wa Mkapa?
 
Mheshimiwa Waziri wa Afya, Ummi Mwalimu,
Napenda kukusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Naamini kwamba bado uamuzi haujafikiwa kuhusu "Universal Health Insurance Fund" ambayo itajumuisha watanzania wote.
Nafahamu pia kuwa yapo mapendekezo ya kuanzisha "regulator" wa huduma za afya. Kwa upendo nilionao kwa taifa langu, napenda kutoa ushauri wa bure.
Utaratibu wa kuanzisha uchangiaji wa mfuko wa huduma za afya kwa watanzania wote usianze kabla ya kuanzisha "REGULATOR" wa huduma za afya nchini. Hii ni kwa sababu bila kurekebisha tatizo la awali, matatizo yatahamia kwenye mfuko huo mpya. Tukirudi nyuma, wakati wa maboreresho ya huduma za serikali (Public Service Reform Program) miaka ya 2005 mpaka 2010, serikali kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ilipendekeza kuwepo kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Afya ambao ungesimamia na kuratibu huduma za afya zinazotolewa na taasisi zote (Serikali, Binafsi, NGOs, Mashirika ya Umma, Taasisi za Dini nk). Kwa bahati mbaya jambo hilo halikufanyika. Ni maoni yangu kuwa ni muhimu kwanza iwepo taasisi ya usimamizi wa huduma za afya ili wasimamie bei elekezi, hadhi za vituo vya huduma za afya na rasilimali watu zinazohitajika katika vituo hivyo, halafu ndipo Mfuko wa Bima ya Afya kwa Wote uanzishwe. Tusipofanya hivyo tutarudia makosa.
 
Hii mifuko ndio tunaambiwa inafilisika? SSH fukuza Mkurugenzi Mkuu
 
Duuuuh nimewaona maboss zangu Wa Zamani wa2 Electrical Eng. Chibulunje aka Chibu na Boss Wangu Wa Sheria Adv. Kapwete. Daaaah Ila Ewura Watu wanakula Sana Pesa Wazee.
.
Pale Ewura salary ya Office attendant Tu Ni 2.3m per month. Wanawake wengi Wa Ewura hawajaolewa Maana Wana Hela Chafu
.
Legal officer anakunja Zaidi ya 8m basic salary per month
 
Back
Top Bottom