Mkurugenzi NHIF anavyoibia wanachama kwa kushirikiana na Agha Khan hospital

Danniair

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
360
66

Hivi karibuni nilipata malazi yaliyonifanya nimtafute daktari mtaalamu pale Agha Khan Hospital. Nilichoshangazwa nacho ni utaratibu mpya nilioukuta pale. Baada ya kupokelewa nilitia sahihi ktk karatasi mbili tofauti. Moja ilionyesha malipo ya Tsh. 40,000 na nyingine Tsh. 29,000/=

Baada ya kuzisahini nilirudishiwa ile ya 40,000 na nyingine ikabakia pale. Baada ya kumwona Dkt aliniandikia dawa za mwezi mzima. Ktk dirisha la dawa nilipewa dawa za juma moja tu, maelezo ni kuwa bima yetu hakubali dawa za kiasi hicho kutolewa kwa pamoja. Nikapewa ushauri wa kurudi hospitali mara dawa ziishapo.

Dawa zilipokwisha nikarudi. Yaliyojitokeza; Ili kumuona dkt ye yote asiyemtaalamu ili aweze kuniandikia mwendelezo wa dozi Nilisahini kiasi cha Tsh. 20,000 karatasi moja na Tsh 19,000 karatasi nyingine, jumla Tsh.39,000!!!

Ajabu ni hivi dawa zenyewe zinazochukuliwa ni Vitamini C!!! Za siku saba tu.Ambazo kama nikinunua duka la dawa haifiki Ths 1,000/= La kusikitisha ni kuwa mchezo hata NHIF wanaujua kuwa AKH wanafanya hivi kwa wagonjwa bila kujali ugonjwa na umri wa mtu, lakini hakuna hatua yoyote inachukuliwa hata NHIF wanalijua jambo hili kuwa AKH wanafanya hivi kwawagonjwa bila kujali ugonjwa na umri wa mtu, lakini hakuna hatua yoyote inachukuliwa.

Lakini nilipofanya uchunguzi wa haraka haraka nikagundua kuwa ikiwa dkt wa mf. Mwananyamala Hosp akikuandikia kiasi hicho hicho cha dozi na ukienda ktk famasi zilizohakikiwa na NHIF, basi unapewa dozi kamili bila ya kukatwa katwa kama hapa AKH.

Pia hata NHIF wanalijua jambo hili kuwa AKH wanafanya hivi kwa wagonjwa bila kujali ugonjwa na umri wa mtu, lakini hakuna hatua yoyote inachukuliwa. Je, huu si mradi ndani ya mradi? Naomba maoni yenu

ushaanza na dili unategemea nini
labda nikuongezee kama ukabahatika kulala pale hata kwa wiki uliza payment unayotoa mfukoni 25.000 per day ati ni kwa ajili ya chakula na NHIF Awahusikli usione jamaa wanaendesha Range channels zinaongea mpwa we nenda kanisani tu ukamuondoe kwenye cheo uingie wewe
 
Naomba kwanza unieleze unajua maana ya kuweka sahini? Utakubalije kusaini karatasi mbili?wote wawili mnatiwa hatiani?Hata siku moja usikubali kuweka sahini yako kwa kitu ambacho hukielewi na unakiona kinautata utakuja kufungwa.Lazima sahini yako uiheshimu sana na unaweka tu pale unapokua na uhakika wa kitu bila mashaka yoyote na nilazima usome hiyo document uliyopigishwa sahini uwe na uhakika ni halali ndio usain.Next time be very carefully ama sivyo utakuja kufungwa na watoto wa mjini.Kwanza siku likibumbuluka wewe utakua mmoja wapo wa washtakiwa.
Watanzania jamani tuamke tujenge confidence incase kitu hujakielewa na unaona kina utata tuhoji na ikiwezekana twende mpaka uongozi wa juu bila woga topate maelezo ya kurizisha.
 
tafadhali elewa kuwa kwa sisi wanachama wa NHIF hupewi matibabu popote bila kusahini karatasi za NHIF pamoja na zile za mtoa mtoa huduma. Lakini kinachofanyika AKH ni wizi wa kimacho macho tunaofanyiwa sisi wanachama. Tsh 69,000/= consultation na bado utaendelea kulipia 39,000/= kila wiki kwa ajili ya dawa ambazo hazitolewi ktk utaratibu ambao umekwisha lipia Tsh 69,000/= yaani kumwona daktari na kukuandikia dozi ya mwezi mzima, ambayo AKH famasi wanakupa kwa mafungu ya siku 7,7, kinyume na maelekezo ya Daktari. FIKIRIA Vit C vidonge 14 kwa gharama ya Tsh. 39,000/=!!!!!
 
Back
Top Bottom