Mkurugenzi mwingine PSSSF ajikopesha Tsh. Milioni 200 kinyemela

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,370
8,107
Mkurugenzi wa Mifumo ya TEHAMA katika Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Gilbert William Chawe tarehe 16 Septemba, 2022 alifikishwa mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili ikiwa ni pamoja nakukopa kiasi cha shilingi 200,765,838.00 kinyume na utaratibu wa Mfuko.

Akisoma mashtaka hayo Wakili wa Serikali Bw.Hassan Mayunga alisema kuwa Bw. Chawe alitumia fedha za umma katika mfuko wa PSSSF kiasi cha shilingi 135,630,448.00/=, bila kufuata utaratibu, kwa kuzikopa na kununua gari binafsi hali akijua kuwa fedha hizo hazikutengwa kwenye bajeti ya mwaka 2020/2021.

Aidha, wakili Mayunga aliongeza kuwa katika shitaka la pili, mlalamikiwa akitekeleza majukumu yake ya kikazi kati ya mwaka 2020 na 2021 alipokea na kutumia bila kufuata utaratibu fedha za umma kutoka PSSSF kiasi cha shilingi 65,133,390.00 kwa ajili ya kulipia kodi ya ununuzi wa gari binafsi ambao haukufuata utaratibu.

“Kitendo hicho Mwenyekiti ni kinyume cha kifungu cha 6(1)(a),(b) na (f) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995 kikisomwa pamoja na Kanuni ya 3(2)(a) na (e) ya Kanuni za Udhibiti wa Mgongano wa Maslahi na Kanuni 7(d) na (e) ya Kanuni za Ahadi ya Uadilifu,” alisema.

Shtaka la tatu alilosomewa ni kupokea fedha kiasi cha shilingi 65, 133,390.00 kutoka PSSSF kwa ajili ya kulipia kodi ya ununuzi wa gari binafsi, lakini kiasi hicho kilitumika kinyume na utaratibu na pia hakikutumika kama ilivyokusudiwa.

Mlalamikiwa amekana malalamiko yote matatu.

Ilidaiwa mbele ya Baraza kuwa mlalamikiwa alipata mkopo huo kinyume na sera ya mikopo ya PSSSF na kuwa mkopo huo haukupita kwenye kamati ya mikopo ya taasisi.

Upande wa mlalamikaji uliliambia Baraza kuwa, “Sera ya mikopo ya PSSSF ya tarehe 1/11/2018 kipengele cha 4.2.(b)(viii) kinasema kuwa mfuko utalipa asilimia mia moja ya kodi kwa Mkurugenzi mkuu na wakurugenzi wengine kwa gari jipya, lakini gari alilonunua mlalamikiwa halikuwa jipya bali ni garichakavu.”

Aidha upande wa mlalamikaji uliwasilisha vielelezo mbalimbali ikiwemo mkataba wa mkopo uliosainiwa Aprili 24, 2021, orodha ya wanufaika wa mkopo na hati ya malipo ya tarehe 29 Aprili, 2021.

Hata hivyo, ushahidi kutoka Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) unaonyesha kuwa gari alilonunua Bw. Chawe lenye nambari za usajili T607DTQ lilisajiliwa kwa mara ya kwanza na mamlaka hiyo tarehe 12/6/2020 na mmiliki wake wa kwanza ni Bw. Kipemka Msemembo Musa.

“Mnamo tarehe 4 Mei, 2021 umiliki wa gari hilo ulihamia kwa Bw. Chawe kutoka kwa Salim Cars wa Dar es Salaam. Salim Cars alilinunua kutoka kwa Jaji Musa wakati gari hilo lilisha lipiwa kodi na Serikali,” ulieleza upande wa malalamiko.

Serikali ilinunua gari hilo na kumpa Jaji Musa kama stahiki yake alipostaafu.

Mlalamikiwa amekiri mbele ya Baraza kuwa mmiliki wa kwanza wa gari hilo ni Jaji Musa.

“Ni kweli gari hilo alipewa Jaji Musa kama stahiki yake, lakini aliliacha Toyota kwa lengo la kutafuta mnunuzi mwingine,” alisema Bw. Chawe.

Alipoulizwa kama Salim Cars anayedaiwa kulinunua kutoka kwa Jaji Musa alimuonyesha hati za malipo ya kodi, mlalamikiwa ameshindwa kulithibitishia Baraza.

“Mfuko wa PSSSF ulimlipa fedha za kodi Salim Cars, sio mimi, malipo haya yalilipwa baada ya kujiridhisha na kiasi cha kodi kilichotakiwa kulipwa,’ alisema.

Hata hivyo mlalamikiwa alipoulizwa mbele ya Baraza kama kiasi cha shilingi milioni 13.6 ambayo ni asilimia 10 ya Tsh 135 milioni iliyotakiwa kulipwa TRA kama gharama ya uhamisho wa umiliki wa gari ililipwa ameshindwa kulithibitishia Baraza malipo hayo.

Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma lililokuwa chini ya Mwenyekiti wake Jaji (Mst.) Ibrahim Mipawa limehitimisha vikao vyake vya uchunguzi vilivyoanza Septemba 6 kwa kusikiliza malalamiko tisa (9) ya ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Waliofikishwa mbele ya Baraza ni pamoja na Bw. Geofrey Chibulunje, aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. Hoseah Kashimba Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bi Beatrice Lupi, Mkurugenzi wa Fedha wa PSSSF, Bw. Ernest Khisombi, Mkurugenzi wa Ugavi na Ununuzi wa PSSSF na Bw. Peter Martin Sulle, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu.

Wengine ni Bi. Kapwete Leah John, Mkurugenzi wa sheria wa EWURA, Dkt. Ayoub Chacha Rioba, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Jerome Philip Kamwela, Mkurugenzi wa Tathimini na Ufuatiliaji wa TACAIDS na Bw. Gilbert William Chawe, Mkurugenzi wa Mifumo ya TEHAMA wa PSSSF.

Vikao vya Baraza la maadili ya viongozi wa Umma ni utekelezaji wa matakwa ya Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kuhusu kusimamia tabia na mwenendo wa viongozi wa umma waliotajwa katika Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Chanzo: OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA
 
Mkurugenzi wa Mifumo ya TEHAMA wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Gilbert Chawe, amefikishwa kwenye Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili na kukopa Sh. milioni 200.7 kinyume cha utaratibu wa mfuko.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya baraza hilo mwishoni mwa wiki, Wakili wa Serikali, Hassan Mayunga, alidai mkurugenzi huyo alitumia fedha za umma za mfuko wa PSSSF Sh. milioni 135.6 bila kufuata utaratibu kwa kuzikopa na kununua gari binafsi, ilhali akijua fedha hizo hazikutengwa kwenye bajeti ya mwaka 2020/21.

“Katika shtaka la pili, mlalamikiwa, akitekeleza majukumu yake ya kikazi kati ya mwaka 2020 na 2021, alipokea na kutumia bila kufuata utaratibu fedha za umma kutoka PSSSF Sh. milioni 65.13 kwa ajili ya kulipia kodi ya ununuzi wa gari binafsi bila kufuata utaratibu,” alidai.

Wakili huyo alidai kitendo hiko ni kinyume cha kifungu cha 6(1)(a), (b) na (f) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya Mwaka 1995, kikisomwa pamoja na Kanuni ya 3(2)(a) na (e) ya Kanuni za Udhibiti wa Mgongano wa Maslahi na Kanuni 7(d) na (e) ya Kanuni za Ahadi ya Uadilifu.

“Shtaka la tatu ni kupokea fedha Sh. milioni 65. 13 kutoka PSSSF kwa ajili ya kulipia kodi ya ununuzi wa gari binafsi,

lakini kiasi hicho kilitumika kinyume cha utaratibu pia hakikutumika kama ilivyokusudiwa,” alidai.

Wakili Mayunga, alidai mlalamikiwa huyo alipata mkopo huo kinyume cha Sera ya Mikopo ya PSSSF na haukupita kwenye kamati ya mikopo ya taasisi.

Upande wa mlalamikaji ulidai mbele ya baraza hilo kuwa kipengele cha 4(2)(b) cha Sera ya Mikopo ya PSSSF ya tarehe 1/11/2018 kinasema mfuko utalipa asilimia 100 ya kodi kwa mkurugenzi mkuu na wakurugenzi wengine kwa gari jipya, lakini gari alilonunua mlalamikiwa halikuwa jipya, bali gari chakavu.

Upande wa mlalamikaji pia uliwasilisha vielelezo mbalimbali ikiwamo mkataba wa mkopo uliotiwa saini Aprili 24, 2021, orodha ya wanufaika wa mkopo na hati ya malipo ya Aprili 29, 2021.

Vilevile, ushahidi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) unaonyesha kuwa, gari alilonunua Chawe lenye namba za usajili T 607 DTQ, lilisajiliwa kwa mara ya kwanza na mamlaka hiyo Juni 12, 2020 na mmiliki wake wa kwanza ni Kipenka Musa.

Mnamo Mei 4, 2021, umiliki wa gari hilo ulihamia kwa Chawe kutoka kwa Salim Cars wa Dar es Salaam ambapo Salim Cars alilinunua kutoka kwa Jaji Musa wakati gari hilo lilishalipiwa kodi na serikali na ililinunua gari hilo na kumpa Jaji Musa kama stahiki yake alipostaafu.

Mlalamikiwa huyo alikana mashtaka hayo yote lakini akakiri mbele ya baraza kuwa mmiliki wa kwanza wa gari hilo ni Jaji Musa.

“Ni kweli gari hilo alipewa Jaji Musa kama stahiki yake, lakini aliliacha Toyota kwa lengo la kutafuta mnunuzi mwingine,” alisema Chawe.

Alipoulizwa kama Salim Cars anayedaiwa kulinunua kutoka kwa Jaji Musa, alimwonyesha hati za malipo ya kodi, mlalamikiwa alishindwa kulithibitishia baraza.

“Mfuko wa PSSSF ulimlipa fedha za kodi Salim Cars, siyo mimi, malipo haya yalilipwa baada ya kujiridhisha na kiasi cha kodi kilichotakiwa kulipwa,” alidai.

Mlalamikiwa alipoulizwa mbele ya baraza kama Sh. milioni 13.6 ambayo ni asilimia 10 ya Sh. milioni 135 iliyotakiwa kulipwa TRA kama gharama ya uhamisho wa umiliki wa gari ililipwa, alishindwa kulithibitishia baraza malipo hayo.
WAACHENI WALE KWA UREFU WA KAMBA ZAO KAMA MAMA ALIVYOSEMA
 
... huyo Mkurugenzi Mkuu (MM) yupo tu anaangalia yote hayo yakitendeka? By the way, MM si yuko kwenye mnyororo mzima wa kuidhinisha hiyo mikopo? Huyo MM alichukua hatua gani kuzia hayo yasitokee? Naye ni jipu!

Wazee wetu wanadhalilika hawalipwi haki na jasho lao huku kuna wapuuzi wachache wanachezea fedha za wastaafu hawa!

Lengo la kuunganisha mifuko ile na kuja na mfuko mmoja lilikuwa nini? Kulea ufisadi? Badala ya kuboresha imekuwa kinyume chake!
 
Hawa dawa yao kuwalawiti hadharani tu .Mifuko haina hela kumbe wanaleta uchoko wao wa kuchezea hela tu.
 
Sasa hv nafuatilia hizi kesi ili nijue kozi muhim za kusoma hii nchi. Ili hata wanangu wasome waje kula hii keki ya taifa maana its obvious hakuna supervision
 
... huyo Mkurugenzi Mkuu (MM) yupo tu anaangalia yote hayo yakitendeka? By the way, MM si yuko kwenye mnyororo mzima wa kuidhinisha hiyo mikopo? Huyo MM alichukua hatua gani kuzia hayo yasitokee? Naye ni jipu!

Wazee wetu wanadhalilika hawalipwi haki na jasho lao huku kuna wapuuzi wachache wanachezea fedha za wastaafu hawa!

Lengo la kuunganisha mifuko ile na kuja na mfuko mmoja lilikuwa nini? Kulea ufisadi? Badala ya kuboresha imekuwa kinyume chake!
Hawa hawa utawasikia vijana siwakupewa Ofisi kubwa...Calagabhao Maifume Gatororo Njaukenyo
 
Back
Top Bottom