Mkurugenzi Muhimbili azomewa mbele ya waziri..........


Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,612
Likes
626,587
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,612 626,587 280
Mkurugenzi Muhimbili azomewa mbele ya waziri


na Mariam Mtikita


amka2.gif
KAIMU Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Mwakaiya Makanye, jana alionja joto la jiwe baada ya kuzomewa na wafanyakazi wa hospitali hiyo mbele ya Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda. Tukio hilo lilitokea jana wakati waziri huyo mpya alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa hospitali hiyo mara baada ya kutembelea wodi mbalimbali.
Sababu ya kuzomewa kwa kaimu mkurugenzi huyo ni kuficha uozo unaotendeka hospitalini hapo ambapo wafanyakazi hao walidai kuwa waziri amedanganywa kwa kutembezwa sehemu nzuri wakati kwenye uozo hakupelekwa.
Uozo unaodaiwa na wafanyakazi hao ni ule ulioko kwenye wodi za wazazi, uchunguzi na nyingine kadhaa ambazo zinakabiliwa na uhaba wa vitanda na dawa na mafaili ya kutunzia kumbukumbu za wagonjwa.
Kadhalika, wafanyakazi hao walifikia hatua ya kumzomea mkurugenzi wao pale alipojaribu kutetea madai ambayo wafanyakazi wanadai hawajatekelezewa.
Hayo ni pamoja na kutolipwa mishahara kwa takriban miezi mitatu hadi sita, kutopatiwa mkurugenzi kwa muda wa mwaka mzima na kwamba nafasi hiyo imekuwa ikikaimiwa katika kipindi hicho chote.
Hali hiyo ilijitokeza baada ya wafanyakazi hao kutoa hoja zao kwa Waziri wa Afya ili wapatiwe ufumbuzi na kabla waziri hajafanya hivyo Makanye alionekana kutaka kuzima hoja zao kwa kutamka kuwa suala hilo linafanyiwa uchunguzi.
“Kero yetu kubwa ni kutolichukulia uzito suala la madai yetu ya kujiongoza wenyewe kwa kutokuwa na mkurugenzi kwa muda wa mwaka mzima bila kupatiwa sababu za kueleweka,” alisema mmoja wa wafanyakazi hao Primansi Saidia.
Pia walidai kuwa fedha za posho zilizotengwa kwa ajili ya wafanyakazi hao (PPM) hazitumiki kwa kuangalia maslahi yao badala yake zinatumiwa kwa shughuli zinazohusu hospitali hiyo.
Mbali na hayo pia wafanyakazi hao waliitaka serikali kuangalia suala la ajira kwa wafanyakazi waliostaafu wakiwa bado na nguvu, kuajiriwa kwa mkataba hata wa mwezi mmoja hasa kipindi hicho wanachokabiliwa na uhaba wa madaktari na wauguzi.
Akijibu hoja hizo, Waziri wa Afya, Dk. Mponda, aliahidi kushughulikia hoja hizo kwa uangalifu kulingana na uzito wa majukumu yanayowakabili.
 
Lekanjobe Kubinika

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2006
Messages
3,065
Likes
30
Points
135
Lekanjobe Kubinika

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined Dec 6, 2006
3,065 30 135
Patamu hapo. Kwani Mkurugenzi akimwonyesha waziri maeneo mabovu ili naye afikirie namna ya kutatua anaona ni mzigo gani? Alichukiwa bure "Becharm" ambaye alibadilisha kabisa maisha ya wafanyakazi MNH, alichukiwa sababu tu alikuwa nesi akiwaongoza madaktari. Tatizo letu watanzania hatujiamini. Lema alipoingia alionekana kama mkombozi, lakini aliposhikilia hatamu akaweka mikwara kiasi cha kupiga ngumi "Tyson" mtu yeyote asiyekwenda kwa kufuata mdundo wake hata ofisini, aliwadhibiti wafanyakazi kiasi kwamba mambo yakalala kabisa. Baadaye katoka, wafanyakazi walidhania Swai ndiye mkorofi lakini wote hawapo pamoja na Lipyoga lakini kuna mpwayo mkubwa sana. Inaelekea kwa sasa uo ngozi wa hospitali uko mikononi mwa Nyoni ambaye anashinda Muhimbili kimwili na kiakili. HUyo naye hasikii la mwadhini wala la msoma sala. Anachotaka ni mapenzi yake kutimia na ufalme wake kuja.

Wizi mtupu. kila mahali. Kweli IPPM haina maana tena MNH, watu wamepoteza hamasa nayo tangu ilipoanza kupigwa kodi ilhali daktari anapata chini ya robo ya anachozalisha, wenye kunufaika ni viongozi wenyewe kwa maposho kibao nwanayojipa kutokana na pesa hiyo. Nayo kuipata inachukuwa muda mrefu tofauti na malengo ya awali kumsaidia mfanyakazi na kumzuia asimezee mate vishughuli vya kimachinga huko nje. Hakuna duniani penye madaktari masikini kama Tanzania, ndio maana watanzania wanatimkia nje. Wakifika huko wanajituma kwelikweli kwa sababu nao nwanathaminiwa vilivyo. Daktari mmoja aliyeko kusini alitamba kabisa kwamba yeye hajiulizi atakula nini mwezi huu, bali niwekeze kwenye nini, maana swali la kula halina maana kwake, take home inamwezesha kula kumzidi kiwavi kwa miezi miwili mbele angalau. Anajiuliza awekeze kwenye nini ili akirudi TZ aendelee kutojiumiza kichwa juu ya familia kula nini. Fully balanced diet imehakikishiwa mbele yake tangu siku ya kwanza, usafiri anakopeshwa kama sharti na samani za ndani kadhalika na hukatwa pasipo kuathiri morari ya utendaji kazi. Kwa nini haiwezekani Bongo?

Watendaji wetu ni wanafiki mno TZ pengine kuliko hata majirani zetu. Uswahili kedekede. Mtu akipata nafasi hujitahidi kudhibiti wengine wasifanane naye. Hata Rwanda na Burundi na Msumbijni wenye vita kila mara wanatuzidi?? Shame to you Tanzanians. Sasa waliokuwa wanatusaidia kutusemea wamepewa viti jikoni kina Mwakyembe naSitta. Haingii akilini na kwa kweli sipati picha kama kina Tundu, Mnyika na wenzake wataweza kufua dafu chini ya Makinda ambaye kawekwa makusudi kabisa kuhakikisha hakuna kelele zinazoinyima usingizi serikali. Kina Zitto ndio hao wanaoanza kujichanganya tena kwa sana mapema hivi. Nchi nyangu TZ nakulilia!!!!
 

Forum statistics

Threads 1,235,773
Members 474,742
Posts 29,234,949