Mkurugenzi mtendaji wa NBC Lawrence Mafuru asimamishwa kazi

Nimesikitika sana maana Mafuru is hard worker and strict na wafanyakazi wa ngazi za juu hawakumpenda maana zile mwanya za mapanga aliziziba sana hivyo wanaweza kufanya kitu kumtega ili aonekane hafai. The next person will be Mchechu wa NHC maana kuna mabosi pale hawataki kumsikia sana. So be careful Mchechuu wahindi mjini wapo tayari kufanya kila mbinu uondoke NHC. I think you know what I mean!!!
Mafuru ninakuombea sana, Mungu akutangulie uonekane innocent na endelee na kazi yako hata kama si hapo ili tu matokeo yasichafue reputation yako nzuri.

Board ya NBC imeona kuna jambo linalohitaji kuchunguzwa. Na ili uchunguzi usiingiliwe, huyu bwana "ameombwa" aende likizo. Wewe unathibitisha hapa kwamba huyu bwana hahusiki kwa kuwa ni "hardworker na strict". Na unadhani kama kuna chochote, basi ni "set up". Na unamuomba Mungu ili huyu bwana aonekane innocent (hapa ni kama unaruhusu uwezekano wa huyu bosi kuwa na hatia, hivyo unamuomba Mungu aonekane safi). Siamini kama Mungu atabadili fact; either ana kosa au hana. Period. Mungu hahusiki.

Kwa kuwa unaamini dhahiri kwamba huyu bosi ameonewa, ina maana unazifahamu vizuri tuhuma zinazomkabili huyu (na pengine utakuwa ni member wa board NBC). Ninaomba utufahamishe tuhuma hizo, kama hutajali.
 
Whatever the case, ni baadhi ya vijana wa bongo ambao wametokelezea na ninawaangalia kama kioo cha mabadiliko ya uongozi na utendaji bora ndani ya Tanzania wakiwa vijana walioweza kuonyesha kuwa vijana wanaweza.. Wengine ni Mchechu(NHC),Mafuru(SBL),Imani Kajula(NBC),,Ms. Mwambapa(CRDB),Singano(BoA?),Hon. Zitto Kabwe,Kipanya(KP Wear) to name a few.
Eti unasemaje!!?????? Hapo kwenye wekundu,Huyo jamaa kumuweka kwenye hilo kundi umemdhihaki. Ni sawa umemlinganisha Prof. Shaba na Albert Einstein. Au Mwigulu Nchemba na Baba wa Taifa,labda utanielewa vizuri hapo.
 
Eti unasemaje!!?????? Hapo kwenye wekundu,Huyo jamaa kumuweka kwenye hilo kundi umemdhihaki. Ni sawa umemlinganisha Prof. Shaba na Albert Einstein. Au Mwigulu Nchemba na Baba wa Taifa,labda utanielewa vizuri hapo.

FLIGHT OF IDEAS = SCHIZO!! ha ha ha ha hahahaa


utupu
 
Huyu jamaa nimesoma naye shule pale IFM ni one of the best properties katika bongo hii. Hope hajaharibu chochote.

kama ulisoma nae miaka 10 iliyo pita then out of date mkuu,maana ndani ya miaka 5 watu hubadilika kabisa kulingana na nafasi zao na mianya inayo jitokeza.
 
Whatever the case, ni baadhi ya vijana wa bongo ambao wametokelezea na ninawaangalia kama kioo cha mabadiliko ya uongozi na utendaji bora ndani ya Tanzania wakiwa vijana walioweza kuonyesha kuwa vijana wanaweza.. Wengine ni Mchechu(NHC),Mafuru(SBL),Imani Kajula(NBC),,Ms. Mwambapa(CRDB),Singano(BoA?),Hon. Zitto Kabwe,Kipanya(KP Wear) to name a few.

Pata nakala ya raia mwema wiki hii..soma makala ya Ulimwengu "Nakisi ya usaili, mtaji wa ushirikina" itakusaidia kujua tatizo ulilo nalo!ili usiposti upuuzi km huu tena
 
Hizi ni habari nzuri saana kwa wafanyakazi wa kawaida wa NBC na chama cha wafanyakazi wa Mabenki FIBUCA, huyu bwana kiutendaji hakuwa mtanzania hata kidogo hasa kwa upande wa maslahi ya wafanyakazi, amefukuza mpaka kiongozi wa wafanyakazi, na NBC ni kati ya benki zinazolipa mishahara midogo zaidi tanzania kwa wafanyakazi wake, Kimsingi iko haja ya kufanya sherehe na Cheo ni Dhamana 2 jamani



Hapo kunaukweli mkuu...kuna dada mmoja anafanya nbc nakaa nae jirani leo asubuhi wakati tunaenda kazini ndio akaanzisha hizo habari za MD wao kusimamishwa kazi nilikua cjazisikia....kasema wazi wafanyakazi kwao ni sherehe kwani jamaa alikua hovyo kwao na alishawaambia wafanyakazi kama mtu hayuko comfortable kufanya kazi nbc milango iko wazi...ukweli mdada huyo aliongea mengi abt Mafuru na alikua so excited njia nzima...kuna mengi hapo
 
Huyu bwana ni active member humu, ila hajachangia chochote so far. Ila NBC mmmh! Ni benki ya hovyo. Nilikuwa mteja, no more now.
 
Akisha simamishwa wewe kinakuuma au? Au ulikuwa unategemea akuingize kazini? Let us know that...

Acha kwamwaga upuuzi wako hapa wewe, au unaathirika na maamuzi hayo nini? Unajua kwamba pesa za watanzania ziko pale? au unafikiri waathiraka pekee wa Bank failure ni shareholders? Njaa yako itakudhalilisha.
 
Lawrence Mafuru ni mmoja ya vijana wenye uwezo mkubwa wa kiuongozi lakini kubwa zaidi ni mwaminifu sana,nafahamu na natambua kwamba kutakuwa na mchezo mchafu unafanywa dhidi yake lakini naaamini Mungu atakuwa upande wake na atarejea akiwa stronger zaidi na kusaidia kufanya kile ambacho waswahili wengi hawawezi ku-run benki kubwa ya saizi ya NBC.

Kitendo cha ABSA kukubali inadhihirisha wewe ni mtu wa kiwango gani na ninaamini you will get through this.
Nakuombea ushinde mtihani huu.

Kama unalielewa sakala la YUDA na Mwalimu wake YESU, usingethubutu kumsemea Mwanaadamu yoyote yule kwamba ni Mwaminifu. Kweli nakuambia, tuache uchunguzi ukamilike.
 
Mimi nasubiri taarifa za uchunguzi kwanza, lakini ntaendelea kujiuliza swali moja tu mpaka uchunguzi utakapokamika. Nasikia Jamaa take home yake ilikuwa ni 40M hivyo kama kuna tamaa yoyote ile ilimuingia na kumfikisha hapa sidhani kama itakuwa imetoka kwa shetani huyu naemjua mimi.
 
Hawa MD wa mabenki wote wezi, bora nbc wameamua kuamka lkn hawako wenyewe crdb, stanbic?? Na wao waamke and do what nbc have done.
 
kuna jamaa mmoja yuko nbc ni mmoja wa watu waliotoka vodacom yeye ndio anaiharibu nbc. Jina lake maharage chande watu wamuangalie sana jamaa ni mafia sana. Inawezekana zengwe ndio kaanzisha yeye.

nakuunga mkono asilimia 100% mkuu,jamaa anaiua bank taratibu
 
Huyu bwana ni active member humu, ila hajachangia chochote so far. Ila NBC mmmh! Ni benki ya hovyo. Nilikuwa mteja, no more now.

huyu jamaa nasikia amesimamishwa na bosi wa barclays africa ambae alikuwa hapa jana na juzi, kuna issue za kuwapa washikaji zake vyeo na kuwalipa bonasi kubwa sana (hundreds of millions noma) wakati banki inafanya viabaya sana, tokea ameshika madaraka benki haija improve hata kidogo...

kuna issue za kuwapa mademu zake u branch manager na mishahara ya ajabu wakati branch managers wengine hawapewi hiyo mishahara

halafu kuna swala tete la uniform za wafanyakazi wa NBC, mke wake ndio supplier - utata mtupu

kwa kweli huyu jamaa ame behave kama wale ma ceo wazee wa zamani, amearibu jina sana kwa ma ceo wa TZ... its a shame
 
Back
Top Bottom