Shigganza
Senior Member
- May 24, 2018
- 160
- 412
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu ya Vodacom Hisham Hendi amerejea kazini wiki hii baada ya kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inamkabili kuisha kwa kukiri kosa na kukubali kulipa. Ikumbukwe kwamba wakati Hisham hakuwepo kazini bodi ya kampuni hiyo ilimteua Jacque Marais kukaimu nafasi hiyo
Hendi na maofisa wengine 8 wa vodacom waliachiwa Aprili 18 mwaka huu na Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu baada ya kampuni hiyo kulipa fidia ya sh. bilioni 6 ilizokuwa imeshitakiwa katika kosa la uhujumu uchumi, Malipo hayo yalikuwa ni matokeo ya majadiliano kati ya Vodacom na ofisi ya Mwendesha mashitaka(DPP)