Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya METL unawanyonya watanzania wenzako

BABA KO

Member
Sep 25, 2014
43
9
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Metl hivi Ni kwamba hufahamu Hali za watumishi wako hasa watanzania au n kwamba umeamua kufumbia macho unyonyaji unaofanywa kwao kwao,??

Inasikitisha Sana kwa kampuni yenye jina kubwa Kama hii na inauoheshimika Sana hapa Africa kutojali maslahi ya wafanyakazi wake hasa wenye asili ya kitanzania na badala yake imekuwa ikikumbatia wahindi licha ya ukweli kwamba hawana elimu kubwa Wala ujuzi wakutisha.

Uchunguzi mdogo niliobahatika kuufanya ndani ya kampuni hii n kuwa watumishi wa kila idara wanalalamika kwa maslahi madogo kwao ukilinganisha na kiwango Chao Cha elimu na ujuzi (si Jambo la kustahajabu hata kidogo ndani ya kampuni hiyo kukuta mtu anaelimu ya PhD au master kukuta analipwa laki 4 au 5,wakati huo Kuna wahindi wenye certificate bila ujuzi wakilipwa mamilion ya shilingi n maslahi mengine mengi.

Jambo Hilo limekuwa likiwatesa watumishi hao na kushindwa kuwekeza akili Yao kwa ustawi wa kampuni ndio maan hata ubunifu ndan ya kampuni hii umekuwa wa kiwango Cha chini Sana.
Rai yangu;jaribu kuondoka kero hizo kwa kuimalisha kipto Cha watumishi wako kiendan n kiwango Chao Cha elimu.

Wahindi wapunguzwe Kwani kazi zao n wazi zinaweza kufanywa na wazawa hasa wale wenye sifa ambao kimsingi wengine tayari n watumishi ndani ya kampuni yako Ila tu wamefichwa na wahindi.
 
Unawanyonya hadi wanatengeneza bidhaa zisizo na ubora.

Wamejaribu kuja na juisi ya ukwaju ila badala yake wametengeneza dawa ya ngiri.

Ukwaju una vumbi chini!!
 
elimu ya wabongo hata kama ana PHD ni elimu ya darasani. Kwenye matendo hamna kitu. Ndiyo maana hao wenzetu uliowasema wanapendelewa huwa hatuonani nao vyuoni. Wao wanatengenezwa kuendesha na kusimamia biashara kwa matendo. Knowledge ya Certificate kwao ni tosha kabisa.
 
We nawe hebu acha upumbavu. Yaani uwe na elimu ya PhD halafu uwe unatumwa na wauza ukwaju unakuwa umerogwa au una taahira ya tangu kuzaliwa?

Elimu, elimu...kama una elimu huwezi kuajiriwa kijinga jinga. Yaani umekuja kuwasemea wenye PhD
 
Watanzania tuna njaa boss, wewe ukiona wananyonywa (kunyanyaswa, maslahi madogo)
Yupo raia anatamani akanyonywe zaidi hata maslahi yakipunguzwa zaidi.

Japo si jambo zuri, ila iko hivyo!
Tatizo njaa!
 
Back
Top Bottom