Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,027
NEW UPDATE - ALHAMISI, 15/12/2016

Taarifa mpya ni kwamba, Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo mpaka muda huu bado anashikiliwa na polisi na hajafikishwa Mahakamani kama sheria inavyotaka.

Alifanyiwa mahojiano jana usiku kwa muda mrefu na faili lake linaandaliwa ili lifikishwe kwa DPP.

Bado mashtaka halisi yanayomkabili hayajawekwa wazi.

Taarifa zaidi kukujia...
=======

05b14de8-1084-4a06-8886-ca3d0fcf786b.jpg

Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo, ameitwa na baadaye kuwekwa ndani, Central Police.

Polisi wanaeleza muda huu kwamba Jumanne ya leo atalala ndani hadi kesho Jumatano atakapofikishwa mahakamani.

Maxence Melo anakamatwa huku kukiwa na Kesi ya Kikatiba dhidi ya taarifa ambazo Jeshi la Polisi wanazitaka, kesi namba 9 ya mwaka 2016 dhidi ya Jamii Media dhidi ya polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kesi ambayo mahakama kuu itatolea hukumu, tarehe 20 Februari.

=====================MKURUGENZI Mtendaji wa Jamii Media na mwanzilishi wa mtandao maarufu wa JamiiForums, anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo kuu cha polisi, Dar es Salaam, kwa madai ya kugomea agizo la muda mrefu la jeshi hilo.

Polisi wamekuwa wakiagiza na kuamuru kupewa taarifa za watumiaji wa JamiiForums bila mafanikio.

Maxence alipigiwa simu leo akiwa ofisini kwake asubuhi akitakiwa kufika kituoni hapo na alitekeleza mwito huo.

Baada ya kufika polisi kati, akiwa ameongozana na mhariri na mwanaharakati wa uhuru wa mawasiliano, Simon Mkina na mwanasheria, Nakazael Tenga, Maxence alinyimwa dhamana ya polisi.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa Maxence atafikishwa makahamani kesho asubuhi kujibu mashitaka ya kuzuia upelelezi wa polisi dhidi ya makosa ya mtandao.

JamiiForums imekuwa na msimamo wa kutotoa habari za wachangiaji wake kwa yeyote, kwani kufanya hivyo ni kuingialia uhuru na faragha ya wateja wake.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006, msingi mkuu wa mtandao wa JamiiForums umekuwa kulinda faragha ya watumiaji wake.

Watumiaji wa mtandao wa JamiiForums wako huru kuweka mijadala, kuanzisha mijadala, kuchangia chochote pasipo kuvunja sheria za nchi au kuhatarisha usalama wa taifa.

Kampuni ya Jamii Media, inayoendesha mitandao ya JamiiForums.com na FikraPevu.com imejijengea heshima na umaarufu kwa muda mrefu kutokana na namna inavyoendesha na kusimamia shughuli zake ambazo kwa kiwango kikubwa ni za kimtandao.

Mtandao wa JamiiForums ni mtandao mkubwa wa Kiswahili kwa Afrika Mashariki na duniani ukiwa na wasomaji wasiopungua Milioni 2.5 kwa mwezi ambapo kwa mwaka 2016, mtandao huu unatimiza rasmi miaka 10 tangu uanzishwe.

Mtandao huu unasifika kwa kutoa fursa ya kipekee kwa watumiaji wake kutoa yaliyo mioyoni mwao huku wengine wakijifunza mbinu kadha wa kadha za kijasiriamali, afya, elimu na hata kuibuka wanasiasa wapya waliofundwa na wanajumuia ya JamiiForums.

Pamoja na kuendelea kutoa huduma hata katika nyakati ngumu, mtandao wa JamiiForums unakumbana mara kwa mara na changamoto nyingi zinazosababisha waanzilishi na waendeshaji wake kuwa katika misukosuko mara kwa mara, hasa na polisi.

Kwa muda mrefu tangu kuanzishwa kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, Jeshi la Polisi limekuwa likiushinikiza mtandao wa JamiiForums (kwa njia ya barua rasmi) kutoa taarifa za baadhi ya wateja wake.

JamiiForums katika kuhakikisha inasimamia usiri wa wateja wake, imekuwa ikihoji shinikizo kutoka Polisi yanazingatia sheria gani na kutaka kujua ni vifungu gani vya sheria ambavyo wadau wa mtandao huo wamevivunja bila kupewa maelezo yanayoridhisha zaidi ya kuelezwa kuwa hatua zaidi zitachukuliwa kama ushirikiano hautatolewa kwa Jeshi la Polisi.

Tayari Jamii Media imefungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania (Kesi namba 9 ya mwaka 2016); kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinapelekea kuvunjwa kwa haki za msingi za watanzania watumiao mitandao ili kulinda maslahi ya umma kwa kuzingatia vifungu 26(2) na 30(3) vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Baada ya kufungua kesi hiyo Serikali, kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliweka mapingamizi sita ikitaka kesi nzima ifutwe na Jamii Media walipe gharama zilizoingiwa.

Lakini mnamo tarehe 4, Agosti 2016 Mahakama Kuu ya Tanzania baada ya kuzipitia hoja zilizowasilishwa na Serikali na Wanasheria wa Jamii Media iliamua kuwa mapingamizi yote sita ya Serikali hayana mashiko na hivyo kesi ya msingi itaendelea kusikilizwa.

Maxence Melo anakamatwa huku kukiwa na Kesi hiyo ya Kikatiba dhidi ya taarifa ambazo Jeshi la Polisi wanazitaka, kesi ambayo mahakama kuu itatolea hukumu, tarehe 20 Februari.


Chanzo: FikraPevu
=====

Taarifa zaidi..

Maxence Melo alitarajiwa kufikishwa mahakamani leo(Jumatano) asubuhi lakini hilo halikufanyika.

Wakili wa Bw. Melo anatafakari uwezekano wa kuwasilisha ombi kortini kupinga kuzuiliwa kwa mteja wake kwa zaidi ya saa 24 bila kufikishwa kortini.

Kwenye audio hapo chini, Mike Mushi ambaye ni Mwanzilishi mwenza wa mtandao wa JamiiForums, anaelezea mwanzo wa kesi hiyo.
======

MPYA: Breaking News: - Jeshi la polisi latinga ofisi za JamiiForums na kufanya upekuzi
 

Attachments

  • Mike afafanua kukamatwa kwa Max.mp3
    1.7 MB · Views: 230
Naona sasa malaika kashaanza kushushwa kuifungia mitandao ya kijamii.

Iwa hao malaika na aliewatuma afahamu kuwa ni ngumu sana kuzuia mafuriko kwa mkono.

Nao hao malaika wanahitaji pia social media kusemea mema yao.

Yanamwisho.. ila huwezi zuia mafuriko kwa kutumia kiganja cha mkono.
 
Since the beginning of the 21st Century, authoritarian regimes have been shaking in their pants from a looming danger. Don’t think that the danger has anything to do with “Nuclear stockpiles” or “Dinosaur apocalypse”. The danger is in “you”: Social Media users, for instance JF in our context. Why? Because social media is a powerful tool that can invoke “synchronized public actions, resulting from “synchronized public awareness.” This is why so much time and resources is often spent on controlling the Media. Daunting challenge however arises from the fact that unlike traditional media, social media is much more unpredictable, hence uncontrollable. For instance, passing of information via ‘JF’ has freed many Tanzanians from relying on traditional media outlets, which are increasingly becoming state controlled. Also with the advent of ‘JF’, the influence of State Propaganda is becoming severely limited as vast sources of information which are beyond government’s control are now easily accessible by ordinary Tanzanians.

You are a nightmare to the regime.
 
Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo, ameitwa na baadaye kuwekwa ndani, Central Police.

Polisi wanaeleza muda huu kwamba leo atalala ndani hadi kesho atakapofikishwa mahakamani.

Kosa ni kuwanyima Polisi taarifa binafsi za wateja wa mtandao wa JamiiForums zilipohitajika. Maxence ameendelea kushikiria msimamo kuwa ni uvunjwaji wa sheria na haki za wananchi kufanya hivyo.

Taarifa zaidi baadaye


JF ina rensponsibility kubwa sana, kama vivlivyo vyombo vingine vya Habari, kuna mambo mengi ya uongo na uzushi huletwa humu na kuachwa, ikumbukwe kwamba nchi nyingi kama Kenya, Rwanda, Burundi n.k Vita ililetwa na Vyombo vya Habari kama redio na TV, hivyo JF ina jukumu la kulinda amani ya nchi, kama ni kweli amekamatwa, na kama siyo kweli basi wajifunze na wabadilike, watambue jukumu lao kwenye Jamii!

CEO wa JF asipumbazwe na watu wanaosapoti kwenda kinyume na Serikali hapa, wengi wao wana maisha yao na wala hawaishi TZ, na JF ikifa kesho, au ofisi ya JF kunyimwa kibali cha kufanya kazi TZ hawana cha kupoteza, zaidi ya kuhamia kwenye mtandao mwingine na kuendeleza wanayoyafanya, hivyo angalia maisha yako na familia yako, fanya lililo sahihi na jinsi Serikali inavyokutaka kwani mwisho wa siku Serikali ndiyo yenye nchi, watakushauri wanachama wa JF wanavyotaka lkn Serikali ndiyo wasimamizi wa hii nchi!
 
Melo yuko salama..wala hakuna jambo jipya kaitwa kuhojiwa tuu.
Lakini walio sababisha kuitwa kuhojiwa ni wale waleta habari za uzushi ambazo serikali inalazimika kuhangaika kuzikanusha kila leo...
sheria ile ya mitandao ina ipa mamlaka polisi kupata taarifa za mtu kutoka kwa mtu na inawezekana hata kuchukua vifaa husika...
Melo yuko salama salimini.
 
Hivi atakubali kweli tumbadilishe mwingine baada ya miaka yake mitano? Naona kama sasa amezidi, hataki kukosolewa, kusemwa vibaya, mbona katika jamii zetu sijawahi kuona mtu anasemwa kwa mazuri tu, hata ufanye mazuri mwingine anaweza kuona ni mabaya kwa mtazamo wake, yani leo wote tuwe na mtazamo sawa inawezekana kweli? Mbona mke kila mtu anachagua anayempenda iweje kwa kiongozi kulazimishana kumpenda wote?!!!! anyway duniani kuna kuzaliwa na kufa, yote ni maisha, hakuna atakayeishi milele, Hitler alikua mbabe kweli lakini mwisho wa siku alikufa.
 
Back
Top Bottom