Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro aenguliwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Kayombe Masoud Lyoba kutokana na usimamizi usioridhisha wa miradi ya maendeleo

Moja ya usimamizi mbovu anaodaiwa kufanya ni usimamizi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na ni kutokana na ununuzi wa dawa ya mchwa kwa gharama kubwa ya Tsh. Milioni 66 kinyume na gharama halisi

Pia, kutozingatia taratibu za manunuzi na miongozo ya matumizi ya fedha za ujenzi wa hospitali za Halmashauri na kufanya ununuzi wa kokoto kwa gharama kubwa ya Tsh. Milioni 45 na kuzisafirisha kwa Tsh. Milioni 42

Kutokana na hayo, Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Mhandisi Godfrey George Mlowe atakaimu nafasi ya Ukurugenzi wa Halmashauri hiyo
0B7A5979-1CEE-449D-A6FE-EAF6ECF53C46.jpeg
 
Kutokana na hayo, Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Mhandisi Godfrey George Mlowe atakaimu nafasi ya Ukurugenzi wa Halmashauri hiyo


Hongera GGM ila uwe mwangalifu na makini
 
Hizi tumbua tumbua zina double standard sana, Mbona Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Shinyanga ni fisadi sana

Na kapoteza mamilioni ya fedha lakini bado anadunda?

Mradi kama huo wa Ujenzi wa kituo cha Afya, ujenzi wa Chinji la kisasa, Ujenzi wa Dampo na ujenzi wa Barabara kote ni hivyo tu lakini yupo tu? Kilikoni who is behind this man.

Maana hat juzi 29.07.2019 Baraza la Madiwani liliazimiankutukoa na imani nae kutokana na kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo.

Anyways time will tell Wananchi wanaona na wataganya maamuzi.
 
Huyu jamaa si aliteuliwa juzi juzi tu hapa hata mwaka hajamaliza katenguliwa. Hakika magufuli alisema kweli kwamba akikuteua usifurahi wala kufanya sherehe.
Sasa na yeye kwanini anateua mapoyoyo. Huoni kuna tatizo kwenye mambo ya uteuzi?
 
Mzee wa teua tengua ,anaacha kiini cha tatizo anafuta dalili badala ya kujitengua mwenyewe maana yeye ndio tatizo .
 
Pia, kutozingatia taratibu za manunuzi na miongozo ya matumizi ya fedha za ujenzi wa hospitali za Halmashauri na kufanya ununuzi wa kokoto kwa gharama kubwa ya Tsh. Milioni 45 na kuzisafirisha kwa Tsh. Milioni 42
YEYE UWANJA WA CHATO, NDEGE, SGR AND MANY MANY MANY OTHERS ALIFUATA TARATIBU ZIPI ZA MANUNUZI!
 
Ndiyo matatizo ya kupeana vyeo kiundugu na urafiki, vyeo hivi vilikuwa vinatolewa kwa kupanda ngazi kielimu na kiutendaji
 
Mnunuzi wa kivuko mv bwagamoyo hayuko salama, atie maji kwa nywele kichwani.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom